Mandla Jr.
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 3,098
- 631
katika hali ya kawaida timu ya Taifa huwa ina kampuni au chapa inaitwa "National team kit sponsor",mfano Cameroon ni puma na south africa ni nike.Tanzania hatujawahi kuwa na kit sponsor.Kit sponsor anakulipa ufae logo/chapa yake kwenye jezi yake.Kimsingi ili upate kit sponsor inabidi timu yako ya Taifa ifanye vizuri.Kwa Taifa stars adidas kajitolea kutusaidia jezi bure kwa sasa hadi desemba mwaka huu.Swali: Ni utaratibu gani unatumika kupata jezi mpya za Timu ya Taifa??? Je hizi zilizotumika
Namibia ndio zimepitishwa kuwa jezi mpya ya Taifa Starz???
mkuu malinzi mimi bado sijakuelewa yaaniadidas kajitolea bure kuvalisha timu yetu ya taifa wakati anatangaza biashara yake pale,bado kuna sitofahamu juu ya hii mikataba.katika hali ya kawaida timu ya Taifa huwa ina kampuni au chapa inaitwa "National team kit sponsor",mfano Cameroon ni puma na south africa ni nike.Tanzania hatujawahi kuwa na kit sponsor.Kit sponsor anakulipa ufae logo/chapa yake kwenye jezi yake.Kimsingi ili upate kit sponsor inabidi timu yako ya Taifa ifanye vizuri.Kwa Taifa stars adidas kajitolea kutusaidia jezi bure kwa sasa hadi desemba mwaka huu.
mkuu malinzi mimi bado sijakuelewa yaaniadidas kajitolea bure kuvalisha timu yetu ya taifa wakati anatangaza biashara yake pale,bado kuna sitofahamu juu ya hii mikataba.
tunajua wewe ni mtu makini huwezi kupuuza hili swali kama hili
Mheshimiwa Rais unamaanisha kuwa Stars imekosa mdhamini kwa kuwa haifanyi vizuri?katika hali ya kawaida timu ya Taifa huwa ina kampuni au chapa inaitwa "National team kit sponsor",mfano Cameroon ni puma na south africa ni nike.Tanzania hatujawahi kuwa na kit sponsor.Kit sponsor anakulipa ufae logo/chapa yake kwenye jezi yake.Kimsingi ili upate kit sponsor inabidi timu yako ya Taifa ifanye vizuri.Kwa Taifa stars adidas kajitolea kutusaidia jezi bure kwa sasa hadi desemba mwaka huu.
Mheshimiwa Rais unamaanisha kuwa Stars imekosa mdhamini kwa kuwa haifanyi vizuri?
Hongera sana Jamal Malinzi kwakujali maoni ya watanzania kiasi hiki. Natumai utayafanyia kazi yasiishie hapa Jf pekee.
Uko sahihi ndugu, ya kuwa udhamini ni biashara na wadhamini huangalia jinsi gani bidhaa zao zitapata soko kutokana na udhamini watakaoutoa. Februari mwaka huu PUMA walisitisha mkataba wao na timu ya taifa ya Malawi kwa kuwa shirikisho lilishindwa kufika malengo ya kibiashara (kuuza uniti za jezi 10,000 kwa msimu) na sio kwa kuwa eti kiwango ni kidogo kama unavyotuaminisha. Malawi wako karibu nafasi sawa na sisi lakini bado walifanikiwa kupata mkataba na Puma, sawasawa na Guinea ya Ikweta ambao tumewazidi kwa viwango vya Fifa.Mphamvu udhamini wa jezi ni biashara,anayebandika chapa anaangalia chapa yake itaoneka maeneo gani na kuonwa na nani.Ndio maana udhamini wa Nike kwa christian Ronaldo unaweza kuwa mkubwa kuliko kwa timu nzima ya bafana bafana.Kwenye udhamini kuna kitu wanaita "mileage".Taifa stars bado haijawa na mvuto mkubwa kwa wadhamini.Tujitahidi angalau tuingie sabini bora duniani na sio mia naa ya sasa.Tukifika hapa sponsors watapigana vikumbo Dar es salaam.
mkuu kwa hili sizani kama uko sahihi azam wamejipinda wamejenga uwanja wao kwa manufaa yao sasa kwa mechi zao za nyumbani kuwapeleka taifa ni kuwapunguzia mapato kama azam complex ina uwezo wa watu elfu kumi kwanini siziuzwe tiketi elfu kumi tu? pili tiketi ziuzwe mapema kabla ya mechi ili asiye na tiketi asiruhusiwe kabisa kusogea eneo la uwanjaHofu ni usalama wa watazamaji kutokana na wingi wa watu maana capacity ya Azam complex haizidi watu elfu kumi. hata mchezo wa Azam vs Mbeya city uwanja ulifurika sana mpaka tukahofia usalama.Kimsingi TFF tumefurahia sana uwanja wa Azam complex kupewa hadhi ya CAF.
pachanya kuna kanuni imepitishwa na FIFA inaitwa "club licencing". Huko mbele tuendako reforms lazima zifanyiken ili vilabu vyetu viweze kupata leseni za kushiriki mechi za kimataifa.Mfano ni hilo la viwanja masharti ya club licencing ni kuwa kila klabu lazima iwe na access na uwanja wa mazoezi na wa mechi.Masharti mengine ni klabu kuwa na waajiriwa hasa watendaji muhimu,kuwa na youth programme n.k.Rais Jamal mpira wa miguu hauwezi kuendelea pasipo kuchezwa na kuendeshwa kisayansi,kimipango na kimikakati...lakini bado naona dhana hii inaendeshwa kisiasa tu hapa nchini...
SWALI; Kwa nini bado klabu zinazoshiriki ligi kuu Nchini hazina Viwanja vya kisasa inavyovimiliki? Je hamuoni ni wakati sasa wa kupitisha sheria ya kuvibana viweze kujenga viwanja vyao vya kisasa? Mbona Azam imeweza?
Ni aibu klabu kubwa za ligi kuu kutokuwa na viwanja na TFF Mkiona ni jambo la kawaida...
Kwanini msiwalazimishe kwa faida zao? (Ndani na nje ya uwanja)
Anayechagua uwanja wa kuchezea mechi za nyumbani ni timu yenyewe,TFF kazi yake ni kujihakikishia kuwa uwanja uliochaguliwa unatambuliwa na kukubaliwa na CAF/FIFA.mkuu kwa hili sizani kama uko sahihi azam wamejipinda wamejenga uwanja wao kwa manufaa yao sasa kwa mechi zao za nyumbani kuwapeleka taifa ni kuwapunguzia mapato kama azam complex ina uwezo wa watu elfu kumi kwanini siziuzwe tiketi elfu kumi tu? pili tiketi ziuzwe mapema kabla ya mechi ili asiye na tiketi asiruhusiwe kabisa kusogea eneo la uwanja
Ni kweli Kaitaba inawekewa nyasi bandia na FIFA.Rais wangu Malinzi nasikia uwanja wa kaitaba unawekwa nyasi bandia na FIFA kwa maombi ya TFF nakupongeza sana kwa hilo lakini usiishie kaitaba bukoba ambapo ni nyumbani kwenu vitendee haki na viwanja vingine kama jamhuri morogoro, mkwakwani tanga shehe amri abeid arusha na vingine vingi.
Ni kweli Kaitaba inawekewa nyasi bandia na FIFA.
kwa sasa kipaumbele chetu ni kuendeleza plot yetu TFF ambayo tumepewa na mamlaka za serikali Tanga. Ni kiwanja kikubwa kina eka 17,kipo eneo la Mnyanjani,Tanga.Kwa kuanzia tutajenga pitch ya nyasi za kawaida,jukwaa moja na ukuta ili ligi mbali mbali za mkoa wa Tanga zianze kuchezewa pale. Baadae tutazidi kupaendeleza iwe sports complex kamili ya kufundishia mpira wa awali na wa vijana.Kwa sasa tunaandaa michoro na kupima udongo.
Ndugu Rais, ninawashauri msiifanyie kazi ile ripoti ya kamisaa wa mechi ua Yanga na Mgambo. Ripoti ile unprofessiona na imejaa chuki. Waombe Azam Tv wakupatie kipande kile chenye vurugu na usikie maneno ya Refa kwa mchezaji wakati anatoka nje.
Kamisaa ameacha kwa makusudi vitendo vya kishirikina walivyo vifanya Ngassa, Kanavaro na Yondani vya kufukua hirizi uwanjani kabla ya kuanza kipindi cha pili. Wachezaji hao wakiongozwa na mashabiki waliokaa jukwaa la African Sport kama linavyojulikana.
Refa alimuahidi kumkomoa mchezaji kwa kutoa ligha chafu kwake.
Wachezaji wa Yanga walimhisi kuwa ana hirizi na wala siyo bisibisi. Hii ni lugha aliyoitumia akihofu kukosa ushahidi na kudharauliwa kama angeandika habari za hirizi.
Mkuu unajua ulichoandika? Kama wachezaji wa Yanga walifukua hirizi uwanjani kuna tatizo gani hapo? Je hirizi ni mahali pake uwanjani?
Hapakuwa na hirizi eneo walilokuwa wanafukua, walifanya hivyo kwa kuwa waliaminishwa na mashabiki kuwa eneo hilo lina hirizi wakati hakuna kitu.
Sijaiona ripoti hiyo mzee wa Yanga, lakini kitendo cha hao wachezaji kufanya kitendo hicho inaonyesha timu yako inavyoamini ushirikina.
Washauri wenzako kuwa soka ni mchezo wenye nidhamu.