Salaam team. Maswali wanayouliza waandishi wa habari baada ya mechi kwa makocha wa kigeni hiyo ndiyo taswira halisi ya Elimu yetu hapa Tanzania. Kwanza utakuta mwandishi wa habari anauliza swali kwa kiingereza ambacho ni "broken " , pili utakuta swali linaloulizwa ni "irrelevant", tatu mwandishi anauliza swali ambalo wenzake wameshauliza na limeshapatiwa majibu. Hii ndiyo taswira halisi ya Elimu yetu ya kibongobongo. Imagine waandishi wamemaliza vidato vyote wakaenda vyuo mbalimbali diploma Hadi degree, wamefanyiwa usaili kabla ya kuajiriwa, wanasililizwa na maelf ya watu mbalimbali kila siku lakini bado wanaliaibisha taifa kwa kuuliza maswali ya siyo na maana mbele ya makocha wa kigeni. Unategemea Hali ipoje kwenye fani nyingine ambazo hatupati wasaa wa kuwaona na kuwasikia? Kiufupi Hali ni mbaya na ndiyo maana ni ngumu kwa wasomi wa kizazi Cha Sasa kushindana na wasomi wa nchi za jirani katika soko la ajira kwa sababu Kama hizo.