Maswali Yangu kwa TFF, Yanga na Simba

homeless1

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2020
Posts
427
Reaction score
950
Kulingana na mtafaruku uliotokea leo baada ya sintofafaham iliyoletwa na bodi ya league haya ni maswali ambayo nimejiuliza nakosa majibu na nimeamua kuyaleta kwenu wadau wa Soka na hasa mashabiki wa Yanga,Simba na TFF

Najiweka wazi mi nishabiki wa Simba nilieunga mkono 100% maamuzi ya Yanga


NAANZA NA WATANI ZANGU YANGA

1.Hivi kweli Yanga angekuwa muandaaji wa mechi kwa maana ya kwamba angekuawa home team angekubali kufanya uamuzi alioufanya na kuacha mapato yapotee bila kujua yanaenda wapi au wamefanya sababu walikua hawana cha kupoteza


2.Je kama Yanga angekua yupo kwenye fomu nzuri kwa maana ya kwamba anaongoza ligi,kikosi chake kipo sawa na anakaribia kubeba ubingwa angeingiza timu hio saa 1 au angefanya kama alichokifanya maana ukweli ni kua TFF na Bodi ya league wamekosea lakini watani zangu mmetumia huo mwanya kuchomoa betri na kiukweli hakuna wa kuwafunga sababu mmetumia kanuni zao wanaoongoza mpira wetu kuwageukia


3.Kama ni kweli Mechi yenu na biashara na mechi yenu na Azam iliahirishwa na yalikua masaa sita kabla na mlikubali kuicheza, Sasa je leo ni kweli mmechoka na uonevu au leo mmeona ni mechi muhimu iliyopaswa kueleza hisia zenu juu ya ubovu wa TFF au mliona haikua sawa kutengeneza uwiano mkubwa wa pointi kati yenu na Simba àmbae alionekana kua na nafasi nzuri ya kushinda pengine kuliko nyie na pengine ubingwa ungeanza kua ndoto inayotamaniwa kua kweli

HAYA MASWALI KWA TEAM YANGU SIMBA

1.Kwanini hatukuuungana na wenzetu Yanga hio saa 11 hata kama marefa wasingekua uwanjani kuchezesha hio mechi lakini tungekuwa na msimamo sawa labda hii sintofahamu isingetokea, kwa sababu kiukweli Yanga walituweka kwenye mtego ambao unafanya tuonekane sisi na TFF ni kitu kimoja, na hili ilikua na umuhimu kweli kwenda nao sawa hasa ukizingatia Yanga na Simba kitu kimoja kinatuunganisha kwa 100% nacho ni kua sisi ni team za mpira tunaponyanyaswa tunaungana kukemea hata kama ni mahasimu

2.Kwanin tumetaka huruma ya watu katika hili kwa sababu wakati Yanga anaonesha resistance ni wazi walikua na hoja tena yenye mashiko lakini sisi tulikuwa tunaendelea kujiaminisha as hakuna kitu kitatokea ili tupate pa kutokea na ikiwezekana kupata pointi tatu za mezani, namaanisha hapa viongozi wa SIMBA, wanaoendesha kurasa zetu mtandaoni na msemaji wetu Manara asingeonesha dalili yoyote kuwa Yanga wanakosea kwani hili lingeonesha ni jinsi gani tumewaacha mbali Yanga kisoka ndani na nje ya uwanja lakini manara umetaman hata bunge liingile kati huu upuuzi

MASWALI KWA TFF


1.Kwanini taarifa iliyotolewa kwenye taarifa ya kusogeza mechi mbele ilikua haina sababu maalum ya kusogeza mechi mbele, ikumbukwe kisoka sababu za msingi ni kifo cha raisi wa soka,kifo cha raisi au makamu wa nchi, bomu kutegwa uwanjani, usalama wa watu uwanjani kama haupo sawa, barafu au mvua kubwa itayoharibu eneo la kuchezea kwa kizungu pitch

2.Japo sababu hatujui lakini wapenzi wengi wa soka wamepata za chini chini kua sababu ilikua ni uzinduzi wa kitabu cha rais wa awamu ya pili, Kweli hii sababu ilikua ya kupuuza watu wote waliotoka mikoani na maeneo mengine mbali mbali wakiwemo walotumwa na kaizer chief kuangalia mbinu za simba , raia wetu alokimbia 1200km toka kigoma ili aone tukio hili muhimu na pekee kwake, walodai wametoka Zambia ili kuwaona bwalya na chama na wengine nimesikia walikua ni waandishi wa habari wa kimataifa walokuja kujionea na kuripoti taarifa zinazodai nchi yetu imeanza kukua kisoka kwa upande wa ligi na klabu zetu. Kweli sababu hii ilikua na mashiko yani tuache kuangalia burudani ya mpira tuangalie siasa na jinsi mwinyi anapewa gari sababu kwa miaka yake 97 hawezi panda gari za juu labda benzi, siasa na mpira wapi na wapi na ndio maana FIFA wanasisitiza tusiingize Siasa kwenye mpira

3.Je mnajua kua shirikisho la soka Afrika kwenye kurasa zao kwa mara ya kwanza toka mwaka uanze waliweka post inayoonesha hii mechi ya Simba na Yanga na kwa ujinga wenu wakifuatilia kwa undani watawashusha hadhi sana, Afrika japo kwa udogo ilikua na hii taarifa ya mechi na nyie mmeamua kwa makusudi kutuletea hii aibu

4.Je mnajua mashabiki wa Yanga wanasema huu ujinga mlipanga na Simba na taarifa mliwapa jana na mashabiki wa Simba wanasema mmefanya hili litokee ili kuwaokoa Yanga waepukane na kipigo cha mbwa koko

5.Je mnajua mmetoa taarifa bila kukubaliana na Simba na Yanga na kama mngekua mmefanya mazungumzo na klabu zote mbili lazima mngejua Yanga hakuwa tayari labda msingeleta hii sintofahamu na kubakisha mechi ya saa 11 au labda msingeleta taarifa kihunihuni kiasi hicho au labda mngetafuta sababu ambazo kila pande ya Simba na Yanga ingewaelewa kwa sababu binafsi natamani kuwalaumu Yanga lakini sioni makosa yao zaidi ya ujinga na upuuzi wa TFF

6.Kwanin tokea mwaka jana mnahairisha sana mechi ya Simba na Yanga kiasi kwamba mnataman tuone hakuna mechi kubwa duniani ila Simba na Yanga tu hivi kweli hii hili lipo Afrika achilia mbali duniani


7 .Je mnajua hili lazima lipite na mtu wa kuwajibishwa au nyie wenyewe kuwajibika kabla hamjaaribu soka la Tanzania ambalo limetoka mbali na gizani na walau tulianza kuona mwanga na kuinjoi soka



8 .Je mnajua Azam TV wamefanya kazi kubwa mpaka soka letu limefika hapa na kwa mechi hii walifanya maandalizi ya gharama kubwa na imekua rahisi kwenu kupuuza juhudi zao kiukweli leo nlikua au nilitoa machozi ambayo sijui hata yalitoka wapi


NB mmetutua aibu kubwa kama taifa
 
Mechi za yanga dhidi ya azam na biashara hazikuahirishwa saa 6 kabla acha kupotosha.

Mechi hizo ziliahirishwa kwa zaidi ya masaa 24 kabla ya muda uliopangwa awali.

View attachment 1778070View attachment 1778071
Sawa kaka ila leo TFF wamevunja kanuni hilo tuwekane sawa na leo Yanga wawe walikua wanatuogopa ama Lah ila walikua na haki ya kuchukua maamuzi yale na kiufupi wametumia kanuni zilizopo
 
Sawa kaka ila leo TFF wamevunja kanuni hilo tuwekane sawa na leo Yanga wawe walikua wanatuogopa ama Lah ila walikua na haki ya kuchukua maamuzi yale na kiufupi wametumia kanuni zilizopo
Kumbuka viongozi wengi wa yanga Wana migogoro na Tff. Wachache walishafungiwa tayari hivo hii ilikua nafasi ya yanga kuonyesha hasira zao na kutuma ujumbe kwa shirikisho kwamba wao sio wanyonge kiasi hicho.
 
Kumbuka viongozi wengi wa yanga Wana migogoro na Tff. Wachache walishafungiwa tayari hivo hii ilikua nafasi ya yanga kuonyesha hasira zao na kutuma ujumbe kwa shirikisho kwamba wao sio wanyonge kiasi hicho.
Na hakika wamejua kuwasilisha hasira zao
 
Yanga umewaswalika maswali ma3, simba mawili na tifutifu maswali karibi 7 hivi, hii inaonesha mshenzi ni tff hapa, klabu yangu simba sijaielewa elewa, hatuna weledi,bado tuna uswahili. Katika hili utopolo wako sahihi.
Hapo tupo sawa ilibidi hapa tuache Uswahili hata kama mtani kiuhalisia alikua na hasira na TFF ukichangia na uoga kwa simba
 
Hapo tupo sawa ilibidi hapa tuache Uswahili hata kama mtani kiuhalisia alikua na hasira na TFF ukichangia na uoga kwa simba
Hata kama mimi ningekuwa kiongozi wa yanga, kwa simba hii ningetumia hilo hilo kosa la tff kula kona. [emoji23]
 
Simba walivosikia yanga wako uwanjani kwanini hawakwenda muda ule ule wao waliogopa nn kama wanajiamin wangeshinda mechi
 
Simba walivosikia yanga wako uwanjani kwanini hawakwenda muda ule ule wao waliogopa nn kama wanajiamin wangeshinda mechi
Refa hakuwepo ila bora tungeenda kuungana sababu mbali na uhasimu sisi ni wamoja
 
Yanga umewaswalika maswali ma3, simba mawili na tifutifu maswali karibi 7 hivi, hii inaonesha mshenzi ni tff hapa, klabu yangu simba sijaielewa elewa, hatuna weledi,bado tuna uswahili. Katika hili utopolo wako sahihi.
Simba walitakiwa waingize timu saa 11 ili wasiipe nafasi utopolo
 
Update
9.Je haya maelezo mlotoa yana mashiko kweli au mmewapa Bodi ya ligi sababu


Anyway nilitegemea mpaka muda huu basi kuna mtu at least angekua kajiuzuru
 
uyu ndio yote aya kayataka wizara yake ndio imesogeza mechi mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…