cabo
JF-Expert Member
- Jun 15, 2016
- 4,756
- 5,250
Habari za muda huu waungwana, kutokana na ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara kutoka Ubungo mpaka Kimara mwisho haya mataa ya hapa Korogwe, Bucha (kwa Thomas) nasikia hili jina lilikuja kutokana na huyo mzee yeye ndio alikuwa anauza mdudu pendwa yule kwa wale wenzetu wasiopenda kumla KUMRADHI ila kwa wanaomla mjitahidi kumla ili mnenepe muepuke kutekwa kama MOSHA.
Hili eneo lipo Dar es Salaam imekuwa ni kero sasa mataa hayafanyi kazi kwa muda sasa wamewekwa wale waongoza magari na malifleta yao lakini bado watu hawafuati wanayoelekezwa na hao watu yani ni changamoto sana pia hawa ndugu zetu wa nyeupe na suluali za bluu kwa wanawake na wanaume nyeupe tupu wanashinda tu Korogwe stendi pale ambapo hakuna kitu chochote badala waje waongoze magari hapa kwenye mataa unakuta wako wanne watano eneo moja halafu kwa mataa hakuna hata mtu mmoja aiseeee,
Napaongelea maana ni njia yangu ya kila siku ninayopita tunapata changamoto sana tukiwa tuna cross kuelekea maji chumvi nimekoswa koswa mara kadhaa mpaka naamua badala ya kwenda ninapoenda nipite kwanza kanisani hapo Korogwe kwanza kutoa sadaka kwanza ndio niendelee na safari hebu wahusika walishughulikie hili maana litaleta maafa makubwa.