Mataa ya kuongoza magari yanasababisha foleni

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Mataa yaliundwa ili kuongeza usalama kwenye makutano ya barabara. Lakini yana athari moja mbaya. Yanaleta foleni mijini.

Utafiti umefanyika umeonyesha kuwa roundabouts ni salama kuliko mataa na pia hazileti foleni.
Mfano hai: Zamani Mbeya kulikuwaga hakuna foleni. Lakini tokea waweke mataa eneo la mafiati kila mwaka nikienda nakuta foleni imeongezeka. Gari kwenye mataa lazima zisimame kusubiri zamu yao. Kwenye roundabouts hakuna hicho. Muda wote gari ipo kwenye mwendo.

Bahati mbaya wabongo na ushamba wetu tunadhani kuwa na mataa ni maendeleo!! Tuachane na habari ya mataa ya kuongozea magari. Tukomae na roundabouts
 
Mkuu samahani siulizi kwa ubaya, wewe una gari?

Mataa hayana shida kabisa. Tatizo ni pale trafiki wanapoyaingilia na kuanza kuoendelea upande mmoja

Kwenye round abouts nakuunga mkono. Huwa ziko bomba sana
 
Niliwahi kuwashauri DTO fulani na wadau wake RSA Tanzania kwamba round about ni nzuri.

Wazo langu lilitokana na round about ya muda iliyowekwa pale Ubungo wakati wa ujenzi wa lile Daraja la Kijazi, ambapo foleni iliisha kabisa, ila baada ya daraja kukamilika, foleni ikerudishwa na mataa.

Ipo shida mahali!
 
Mkuu samahani siulizi kwa ubaya, wewe una gari?

Mataa hayana shida kabisa. Tatizo ni pale trafiki wanapoyaingilia na kuanza kuoendelea upande mmoja

Kwenye round abouts nakuunga mkono. Huwa ziko bomba sana
Sina mkuu, ila ni abiria mzoefu.
 
Mkuu samahani siulizi kwa ubaya, wewe una gari?

Mataa hayana shida kabisa. Tatizo ni pale trafiki wanapoyaingilia na kuanza kuoendelea upande mmoja

Kwenye round abouts nakuunga mkono. Huwa ziko bomba sana
Mfano ile ya Moro Msamvu.
 
Uko sahihi but sio sahihi sana.
Naunga mkono usahihi wako kuwa round obout is better kutokana na ushaidi nilionao kupitia Round about ya Msamvu Morogoro.
Livha ya makutano ya barabara 4 zenye magari mengi ya aina tofautitofauti but still yote yana-move na jam hamna.
Pale Mbeya mataa(Mafiati) ni papana sana, So wangejaribu kuweka mzunguko kuliko Yale Mataa
 
Mataa yaliundwa ili kuongeza usalama kwenye makutano ya barabara. Lakini yana athari moja mbaya. Yanaleta foleni mijini.

Utafiti umefanyika umeonyesha kuwa roundabouts ni salama kuliko mataa na pia hazileti foleni.
Mfano hai: Zamani Mbeya kulikuwaga hakuna foleni. Lakini tokea waweke mataa eneo la mafiati kila mwaka nikienda nakuta foleni imeongezeka. Gari kwenye mataa lazima zisimame kusubiri zamu yao. Kwenye roundabouts hakuna hicho. Muda wote gari ipo kwenye mwendo.

Bahati mbaya wabongo na ushamba wetu tunadhani kuwa na mataa ni maendeleo!! Tuachane na habari ya mataa ya kuongozea magari. Tukomae na roundabouts
Foleni inaongezeka kutoka na kuongezeka kwa idadi ya vyombo vya moto( magari , pikipiki , bajaji).

Taa haziwekwi kama urembo , zinawekwa kwa kuwa round about inakua imezidiwa. Na taa zikizidiwa ndio kunafanyika grade separation,

Traffic light nyingi za Tanzania hazipo efficient kwa sababu hakuna regular optimization, yaani temesa wakishaweka cycle kwa Kila phase wanaondoka, hawarudi kufatilia efficiency ya signal phase walizoweka .

Round about utafanya vizuri kwenye traffic volume ndogo,
 
Back
Top Bottom