G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Hili suala la COVID 19 kabla halijaanza kusambaa huko kwa majirani sisi huku tulipiga kelele sana. Tulipiga kelele tukabezwa, tukadharauliwa, tukatukanwa. Kumbe waliokuwa wakitutukana walikuwa hawajui chochote kuhusu huu ugonjwa. Aibu!
Kikundi cha sisi wa kwenye mtandao tumeonyesha mapenzi mema na hii nchi na zaidi tunaonekana kujua mambo kwa usahihi sana kuliko CCM na serikali yake. Tupo imara.
Hatimaye mataifa jirani yanathibitisha leo kuwa Tanzania ni epicenter kwa maambukizi ya Corona. Hilo kwa sasa halina mjadala tena.
Tutamuhukumu Rais Magufuli kwa wakati sahihi. Vifo hivi lazima vije kutolewa maelezo tena kwa usahihi. Hii ni nchi na kinachofanya nchi iwepo cha kwanza kabisa ni binadamu walio hai. Uongozi unaopuuzia uhai wa binadamu kamwe usipewe nafasi, huo ni uongozi wa maafa.
Tunaridhishwa na hatua wanazotuchukulia wenzetu. Nilionya kuwa wakati utafika nchi yetu itatengwa kwa kupuuzia hatua zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya COVID 19. Tunaelewa kuwa zipo hatua kali zaidi zitafuata. Tuwe tayari kutumikia ukaidi wetu!