Mataifa yanayo ongoza Afrika kwa uchafu na ukosefu wa vyoo - hivi vipau mbele Afrika ni nini kwa kweli

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna ripoti nimesoma kwamba Ethiopia ndio inaongoza duniani kwa ukosefu wa vyoo kwa watu wake, hizi ni taarifa za 2018 nikashangaa sana ukizingatia wanavyong'ang'ania treni za umeme ambazo pia kutwa full matatizo maana kule hamna umeme wa uhakika, ni vigumu sana kuelewa vipau mbele vya viongozi wa Kiafrika.
Hawa hawa Ethiopia, raia wao hukamatwa kila siku wakijaribu kuitoroka nchi na kuzamia kwenye mataifa ya watu haswa kule Afrika Kusini. Ethiopians Less Likely To Have Access To Decent Toilets – Report – NewsPay.ng

Halafu hapa taarifa za 2017 za mataifa yanayo ongoza kwa uchafu na ukosefu wa vyoo


Countries With The Fewest Toilets Per Capital
Rank Country % of population with access to proper sanitation facilities
1 South Sudan 6.7%
2 Niger10.9%
3 Togo11.6%
4 Madagascar 12%
5 Chad 12.1%
6 Sierra Leone13.3%
7 Ghana 14.9%
8 Congo 15%
9 Tanzania 15.6%
10 Eritrea 15.7%
11 Liberia 16.9%
12 Papua New Guinea 18.9%

Countries With The Fewest Toilets Per Capita
 
Hiyo ni sawa kabisa kwa Tanzania sijui nchi nyingine, kwa mfano Wamasai wote hawana vyoo kwa standard ya Muzungu ambapo hizo statistics zimechukuwa kama kigezo, na siyo Wamasai tu jamii yote ya Wafugaji TZ pia hawana vyoo, TZ yetu hata safarini tu kwenye Mabasi njiani hamna vyoo tunaita kuchimba dawa maana yake kwenda porini, hivyo kwa TZ hapo ni sawa kabisa kama choo maana yake ni choo sijui hizo nchi nyingine!
 
Bus za wapi hizo za kuchimbishana dawa!!!
 
Tanzania kuwepo sijashangaa. Maeneo mengi nje ya mji hakuna vyoo kabisa
 
Matatizo yanaanzia kwenye usambazaji wa miundombinu. Kama hakuna uhakika wa maji ya bomba na umeme vitu vingine vitachelewa sana.
Kwa safari za Moshi-Arusha-Tanga kati ya Chalinze na Mbwewe kulitakiwa kuwe na Refreshing point ambayo ina vyoo kama 20 vya wanawake na 20 vya wanaume. Mgahawa wenye hadhi na hoteli za kupumzika. Pamoja na petrol station.

Hivi vinazalisha ajira kwa vijana na watu kuish kwa ustaarabu.
 
Tanzania tunsonewa
 
Why am I not surprised that Our dear neighbor never disappoints?
 
Kibera na flying toilet
 
Kibera na flying toilet
Kibera ukubwa wake hata sio 0.001% ya Nairobi nzima. Alafu ule mradi wa NYS 2015/16 wa uboreshaji wa miundo mbinu kama mabarabara, madaraja na usambazaji wa umeme kwenye vitongoji duni uliandamana na ujenzi wa vyoo vingi sana pia, vya umma.
 
Duh, hata hilo la kuchimba dawa unataka kuleta ligi kwamba halipo?
Siku hizi Barabara karibu zote mabus yanasimama kwenye restaurants au hotels maalum zilizopo highways kwaajili ya wasafiri, binafsi nasafiri sana, hilo la kuchimba dawa porini ni labda mtu kashikwa na tumbo katikati ya safari.
 
Bila Kunyaland hizo data ni fake! lazma iwemo top three ukizingatia ni nchi flying toilets zilibuniwa!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…