Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Salamu wote wanajukwaa kama kichwa cha habari hapo juu je kunatofauti Kati ya mataifa yaliyotajwa hapo juu? Je wakisema mataifa yenye nguvu ina maana ni Yale yenye uwezo wa kupiga kura ya veto huko UN? Vp kuhusu Japan na Ujerumani maana ni nchi tajiri utasema yana nguvu japo hayawezi kupiga Kura ya veto UN? Au nguvu ni kumiliki nyuklia tu basi Pakistan na India wana nguvu pia japo hapo UN hawana veto power na kiuchumi si sana? au nguvu ni kijeshi na kiuchumi pekee? Japo Japan haijawekeza sana kijeshi(japo wameanza kujihami dhidi ya China siku za karibuni) japo kiuchumi wako vizuri? Karibuni wadau mnipe ufafanuzi.