Matambiko ktk mapenzi: Hii iko sawa kweli!

Matambiko ktk mapenzi: Hii iko sawa kweli!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Jamaa alikorofishana na mkewe na mke akaamua aende akakae
kwa ndugu yake kwa muda wa zaidi ya
mwezi mmoja. Baada ya kusuluhishwa na ndugu, tofauti
miongoni mwao ikaondolewa na wakakubaliana kurudi kukaa pamoja.

Ila wameelekezwa 'wasikaribiane' hadi hapo watakapoenda
huko kwao kutambika ndipo mke arudi kwa mumewe na
kuendelea na maisha yao kama kawaida. Kwa sasa jamaa wako
kwenye maandalizi ya kwenda 'huko kwao' kufanya tambiko la mapenzi yao.

Hiki kisa ni cha kweli na kimemtokea rafiki yangu mkubwa sana
(kabila lake silitaji ng'oooooo nachelea kubadili hali ya hewa humu MMU).

My take: Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao; Kumbe kina Profesa Maji Marefu wako wengi
sema tu wengine wana-operate kwa kificho.
 
Kwangu sioni connection ya tambiko na huo mgogoro wa hao wanandoa. Inawezekana wahusika pia ni waumini wa mambo ya imani za jadi ndiyo maana wanajiandaa kwa hilo tambiko. Kwangu ni ni NO kubwaaa! Siwezi kuendekeza mambo yasiyo na tija.
 
hizi nchi masikini ushirikina sijui utaisha lini,makazini, majumbani hadi kwenye mapenzi ni ushirikina khaaa! hizo ni imani zinatumiwa na uncivilized people!
 
Tuombe neema ya Mungu ushetani huu kwenye mapenzi uondoke

Maana Watu sasa wanategemea ndumba mpaka kwenye mapenzi

HATARI SANA
 
kuna mada ililetwa humu jana ya watu flani kutoka na ndugu zao,hii ni muendelezo?
 
hizi nchi masikini ushirikina sijui utaisha lini,makazini, majumbani hadi kwenye mapenzi ni ushirikina khaaa! hizo ni imani zinatumiwa na uncivilized people!

Ila nikikutajia wahusika na maendeleo ya watokako utashangaa!
 
sasa wanatambika nini??

Hana haja ya kumkaribia mkwewe
amle tu.
 
Ila nikikutajia wahusika na maendeleo ya watokako utashangaa!

sitashangaa sana ukiniambia maendeleo yao,siku hizi watu wenye imani ndio wale wanaochinja albino na kuuwa mama zao ili wawe matajiri..
 
Back
Top Bottom