Matamshi yasiyokuwa sahihi yanaweza kudhoofisha vipi Lugha ya Kiswahili?

Matamshi yasiyokuwa sahihi yanaweza kudhoofisha vipi Lugha ya Kiswahili?

Mr. SADC_TZ

Senior Member
Joined
Nov 7, 2014
Posts
105
Reaction score
22
Heshima kwenu wakuu. Binafsi ningependa kujua swala moja tu, kila mtu humu ndani anajua jinsi lugha ya Kiswahili inavyo tumika (kutamkwa/kuzungumzwa) mara nyingi na makabira ya bara na baadhi ya nchi jirani. je matumizi hayo mabaya ya lugha yetu itasaidia kukuza, kusambaza au kuua lugha yetu...?

Mf:- SURA YAKO MUZURI/SURA YAKO NZURI.

TUSHAURIANE JAMANI....!
 
Wewe ni mswahili na gata kuandika shida.wakenya wanatangaza lugha hii.wana class hadi ulaya uk usa na kwingine.je wewe umejifunza nini hapo,
 
Ninahitaji kujua tu kama utumiaji wenu wa lugha hii unapotosha watu wengine wanaotaka kujifunza kiswahili sanifu yaani sahihi.
 
Aliyekupa wewe, au wengine wowote, mandate ya kuwa viranja wa kusimamia matumizi "sahihi" ya lugha ya Kiswahili ni nani?
 
kawashitaki wakili nipo hapa
 
Aliyekupa wewe, au wengine wowote, mandate ya kuwa viranja wa kusimamia matumizi "sahihi" ya lugha ya Kiswahili ni nani?

Pamoja na ukweli kwamba Kiswahili ni lugha yetu ya taifa na kwamba sisi tunapaswa kuongoza lugha hii kwa E.A ukweli ni kwamba kimataifa tunaburuzwa na Kenya na nchi zingine. Mikutano mingi ya kimataifa niliyohudhuria translators wa kiswahili siyo wa Tz. Pia juhudi zetu za kuinua kiswahili fasaha ni ndogo, angalia media,hasa radio zinavyopotosha na kuharibu kiswahili.
 
Inawezekana ni kweli, lakini kuna angalizo. Katika kutafiti kuhusu ukuaji, uhuishwaji na kufa kwa lugha utagundua kuwa zile lugha ambazo ziliwekewa "viranja" ama zimekufa tayari au kwa namna fulani zimedumaa katika ukuaji na ueneaji wake. Kiingereza ni mfano mzuri (au mbaya) wa lugha ambayo haina "kiranja", na kwa hili limekisaidia Kiingereza kukua kwa kasi kubwa na "kukubalika" zaidi, na hili utakubaliana na mimi, ni kwa sababu Waingereza wala hawataka kutulazimisha kufanya mambo kadiri watakavyo bali wanaiacha lugha ikue kwa namna yake, kwa mahali inapotumika. Na hapa ndipo mimi nina shida, je uTanzanzania wetu ndio unatupa hakimiliki ya Kiswahili? Na je Kiswahili kinachozungumzwa hapa ndicho sahihi zaidi? Kama ndio, tumetumia vigezo gani? Na ni kwa kiasi gani vigezo hivi tulivyovitumia (kama vipo) ni "universal"?
  1. Pamoja na kuwa inawezekana kuwa Kiswahili kinachozungumzwa na kutumika Kenya sio "kizuri" kama hiki cha hapa kwetu, bado haitupi mandate ya kujimilikisha lugha hiyo.
  2. Utakubaliana na mimi kuwa Kenya imefanikiwa zaidi katika kuelimisha watu wake (hasa kwa ngazi za juu za elimu) katika Kiswahili, mf. vyuo vikuu vya Kenyatta na Moi, tofauti na hapa Tanzania ambako utitiri wa vyuo ni siku za karibuni tu na bado hatujaweza kuwa na kada toshelezi ya wataalamu na wasomi wa Kiswahili.
NB: Mimi sio muumini wa lugha au matamshi "sahihi" (standard-anything) bali naamini katika "mutual intelligibility".
 
Heshima kwenu wakuu. Binafsi ningependa kujua swala moja tu, kila mtu humu ndani anajua jinsi lugha ya Kiswahili inavyo tumika (kutamkwa/kuzungumzwa) mara nyingi na makabira ya bara na baadhi ya nchi jirani. je matumizi hayo mabaya ya lugha yetu itasaidia kukuza, kusambaza au kuua lugha yetu...?

Mf:- SURA YAKO MUZURI/SURA YAKO NZURI.

TUSHAURIANE JAMANI....!

Ni vipi matumizi mabaya ya lugha yanaweza kuua lugha?

Na ni aina gani hasa ya hayo matumizi mabaya ya kiswahili tuliyonayo ambayo yanaweza kuua lugha yetu?
 
"accent" umewahi sikia kitu hiki? si kweli kuwa kiswahili cha Kenya ni kibaya na cha Tanzania ni kizuri.ukisoma lugha hakuna iliyo juu ya mwenzie zote ziko sawa.BrE na AmE zina tofauti nyingi mno hakuna neno center kwa muingereza kama muzuri inavyokoseikana kwa mtanzania.zte ni lugha moja but zina vary due t different reasons umbali baina ya wazungumzaji ukiwemo.kwa watu wa lugha wanajua ni nini naongea languages got dialects.......kwa mada yak kwanza futa swala la kusema kuna matumizi mabAya ya lugha......jaribu kuuliza watu juu ya Cockney
 
Heshima kwenu wakuu. Binafsi ningependa kujua swala moja tu, kila mtu humu ndani anajua jinsi lugha ya Kiswahili inavyo tumika (kutamkwa/kuzungumzwa) mara nyingi na makabira ya bara na baadhi ya nchi jirani. je matumizi hayo mabaya ya lugha yetu itasaidia kukuza, kusambaza au kuua lugha yetu...?

Mf:- SURA YAKO MUZURI/SURA YAKO NZURI.

TUSHAURIANE JAMANI....!

Anza kwa kurekebisha kiswahili chako kwanza makabira sio neno sahihi la kiswahili ila makabila
 
Back
Top Bottom