Matangazo ya TPL ya TBC ni utopolo mtupu

Matangazo ya TPL ya TBC ni utopolo mtupu

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2021
Posts
1,061
Reaction score
2,477
Kwa kweli na miss sana Ufm kwenye kutangaza hizi mechi, bahati mbaya haya majamaa ya tbccm yameshinda tenda ya kutangaza ligi redioni.

Yaani kwanza mechi zote lazima dakika 5 zinapotea kwenye matangazo sijui wanashindwaje ku balance muda, ikifika half time uchambuzi ni hovyo kabisa ukitoa Jesse John kwa kweli hao wengine ni huruma kabisa pengo la kashasha lipo kabisa.

Ambiance siyo nzuri kabisa hata quality huwezi linganisha na ufm kabisaaaa

Kurudi kipindi cha pili lazima zipotee tena dak 5 nyingine ,kwa ujumla tbc wanatutangzia dk 80 tu
 
Na hapo bado kukiwa na tukio la kitaifa matangazo yatasitishwa ili twende mubashara kusikiliza viongozi wetu wa nchi wanasema nini [emoji28].
 
Mwl. Kashasha alikuwa ananogesha sana matangazo ya mpira ya moja kwa moja pale TBC! Apumzike kwa amani
 
Sasa we upo Dar halafu unasikiliza TBC kweli?

Hiyo ufm inasikika wapi kama sio Dar na Zanzibar?
Kwa kweli na miss sana Ufm kwenye kutangaza hizi mechi, bahati mbaya haya majamaa ya tbccm yameshinda tenda ya kutangaza ligi redioni...
 
Kusikiliza mpira kwenye radio inahitaji moyo Sana,unaweza sikia hataaaaari goooooooooo aaah anakosa paleeee...yaan unakuwa na pressure pressure kila mda...Sasa hiyo hatari anayosema mtangazaji kwenye radio ukiwa unatizama huioni hata.
 
Kumbe na Wewe umeliona hili
kuna issue zimenibana recently mechi kama 4 nimesikiliza TBC redioni ninayosema ni kweli nimei miss ufm sasa kuna wengine wanasema nawapigia promo,promo ya nini wakati wale wana azam tv tena yale matangazo yalikuwa clear zaidi cha muhimu hapa tbc wajirekebishe tu maan hiyo miaka 10 waliyopewa ni mingi sana kwa kweli sijawakubali bado
 
Sasa we upo Dar halafu unasikiliza TBC kweli?

Hiyo ufm inasikika wapi kama sio Dar na Zanzibar?
Yes niko dsm,sasa hivi hadi mwaka 2031 Tbc pekee ndiyo wenye haki ya kuatangaza kwa redio hii ligi
 
Kwa kweli na miss sana Ufm kwenye kutangaza hizi mechi, bahati mbaya haya majamaa ya tbccm yameshinda tenda ya kutangaza ligi redioni.

Yaani kwanza mechi zote lazima dakika 5 zinapotea kwenye matangazo sijui wanashindwaje ku balance muda, ikifika half time uchambuzi ni hovyo kabisa ukitoa Jesse John kwa kweli hao wengine ni huruma kabisa pengo la kashasha lipo kabisa.

Ambiance siyo nzuri kabisa hata quality huwezi linganisha na ufm kabisaaaa

Kurudi kipindi cha pili lazima zipotee tena dak 5 nyingine ,kwa ujumla tbc wanatutangzia dk 80 tu
Hongera kwa ujasiri wa kusikiliza TBC
 
TBC wapo nyuma sana, bado wapo zama za AM...
 
Back
Top Bottom