Matangazo ya Zanzibar Bwana utachoka mwenyewe!!


Kibandamaiti!
 

ndugu u made my dei, maana nimecheka mpaka machozi halafu kitu kingine hawawezi kutamka majina ya watu vizuri hasa wakiwa sio wazenji lazima watayakosea.
 

ahahahahahah, nimecheka leo mpaka nusura nife, nitazuka zenj one day nikacheke live..
 
Nilipokuwa nikifundisha sekondari niliwahi kukutana na majina yenye makwazo sana. Siku moja niliongoza msafara wa wanafunzi wangu kwenda kufanya 'debating' na shule nyingine, nikakuta mwalimu mwenyeji wangu anaitwa Mr Kasenge. Watoto wakawa wanafanyia utundu lile jina, mara kwa mara wakawa wanarudia "I thank Mr Kasenge for welcoming us....., as Mr Kasenge said during the introduction....!" Ikawa ni vicheko tu!

Pia tulikuwa na shule rafiki (sister school) ya UK ambayo wanafunzi wake walikuwa wanatutembelea kila mwaka. Siku moja nikapewa jukumu la kuwasindikiza safari ya Zanzibar kutembea, tukakutana na mwenyeji aliyejitambulisha kwa jina la Mr Dadi Faki Dadi, halafu akasisitiza aitwe kwa kifupi Faki! Wale watoto wa kizungu liliwasumbua sana hili jina!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…