Matapeli hayaishi, kwanini upande ndege usiruke kwa miujiza ukawahi mkutano. Na " majitu" yanalisikiliza tapeli

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
"Juzi wakati tupo kwenye Ndege nikaona Ndege Ina tembea taratibu sana ikabidi nimfuate rubani kumuuliza nini shida?

Rubani akaniambia shida upepo unatokea Mbele yetu ndo maana unaona Ndege iko taratibu, pale pale nikauambia upepo uelekee tunapo elekea katika jina la yesu

Na kweli upepo ukaanza kutokea nyuma yetu na Ndege ikaanza kusukumwa na tukajikuta tumefika ndani ya wakati mana uwanja tulio kuwa tuna tua likisha ingia giza Ndege haziruhusiwi kutua"

🗣️ Amesema Mtume Mwamposa akiwaambia watu wawe na Imani Kwa Kila kitu.

#fbtanzania
 

Attachments

  • IMG-20261101-WA0016.jpg
    154.3 KB · Views: 5
😂😂😂😂😂 Mimi nikishamuona mtu naamini kwenye kwenda Kwa mwamposa nampunguza mapema sana hata kama ni ndugu yangu sitaki watu wajinga sana kwenye circle yangu.
 
Atuombee na samia afe mimi nitakuwa muumini wake hakika
 
Uzuri wa ishu kama hizi ni hata hao waumini wake wanajua ni uongo ila sasa ndo watafanyaje wakati tayar n mandondocha wa mwamposa
 
Labda hizi ndege za watu 12 ndio unaweza kupiga story na rubanin, ila kuanzia bombardier kwenda mbele huko thubutuuu uyo rubanin unamwona wapi kwanza
 
Ndege ikasukumwa na upepo, au rubani alipiga kofi ndege ikawa free akasevu mafuta!
 
Ya mwanzo mwanzo kabsaa we pekua utaiona
Nimeiona mkuu, mwamposa akipeleka hayo maombi kwenye mashirika ya ndege, atapiga pesa bila kukimbizana na pesa za wanyonge
 
Kuna siku mtume alisema kuna mama alkua anaumwa , kabla ya kuahirisha ibada wakat watu wanasali kuna mama alkua anaobserve steps zake alvokua anatoka, maana anatokaga watu wakiwa wanaomba, akazifatisha akapokea uponyaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…