Matapeli wa mtandaoni

Kuna mmoja alinipigia simu, akaniambia kuna mtu amekosea kutuma hela ikaingia kwenye simu yako, baada ya hapo akaniuliza una salio kiasi gani kwenye simu....nikamjibu kuna bilioni 2; hapo hapo akanitukana na kukata simu
 
Kuna mmoja alinipigia simu, akaniambia kuna mtu amekosea kutuma hela ikaingia kwenye simu yako, baada ya hapo akaniuliza una salio kiasi gani kwenye simu....nikamjibu kuna bilioni 2; hapo hapo akanitukana na kukata simu
Yap, ukiwatajia kiasi kikubwa sana lazima anakutukana, likewise nina audio recorded kwa mmoja aliniona mkulima flani hivi, yaani kila anachoniuliza namjibu kwa heshima zote huku narekodi.

Karibia na mwisho yaani nimtumie pesa nikamwambie nimeona kuna salio limeingia sikujua limetoka wapi, ndiposa akasema ni huyo mteja alikosea tunakupa atakupigia umrudishie.

Hapa sasa; mteja wa kike akapiga, kifupi nikamwambia pesa yako nakutumia yote ila sina balance ya kutuma naomba nirushie 12,500 ili nitume pesa yako yote isikatwe.

Alichojibu after πŸ˜† ahahahahaaa...
 
Hata kuandika tu hawezi alafu anataka kutapeli.
Yaani huyu jamaa ni tapeli mjinga katika matapeli wajinga na hafai kupewa cheo cha utapeli.

Typically tapeli ni mtu smart ambaye anakuongopea mpaka unamuamini then baadae unakuja kushtuka kumekucha.
Hawa ni waganga njaa.
 
TCRA wapo?
Hivi simu zao hazikutani na kadhia hii?
Je ni kwamba kazi imewashinda?
 
Bi mkubwa wangu ana umri wa miaka kama 53 hivi ila zikiingia sms za matapeli anajua kabsa huyo ni tapeli na hata wakipiga simu anatambua na simu yake haikosi pesa mara Kwa mara

Wewe kijana mdogo hao wakutapeli si utakuwa na pesa za kuchezea

Ongeza umakini ikiwezekana umuibie yeye anayetaka kukuibia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…