Matapeli wanaotumia kivuli cha maneno ya Mungu

Matapeli wanaotumia kivuli cha maneno ya Mungu

mwagito25

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
633
Reaction score
352
Habarini wadau.

Leo nimeona nitoe maoni yangu kuhusu watu hawa wanajiita mitume na manabii na masheikh.

Mtu anatumia mafuta, maji, chumvi nk. Wanajiita ni mitume na manabii; je, Biblia inasema hivyo? Ingawa sina rejea ya vifungu moja kwa moja lakin matendo ya Yesu akiwa duniani alifanya miujiza kwa mbinu tofauti ambayo haikuwa kama kanuni. Alimfufua lazaro kwa maneno, aliponya vipofu kwa matope, alimfufua Dorcas kwa maneno nk. Hii inamaanisha nguvu za mungu kumponya mtu hazina kanuni moja.

Hawa watu wanatumia kanuni kuwasaidia watu ni matepeli na nachelea kusema kwamba kuna nguvu ambayo sio ya Mungu wanaitumia ili kujinufaisha.

Nasema hivi kwa sababu, kama wanatumia nguvu za Mungu, biblia inasema "MMEPEWA BURE TOENI BURE", sasa kwanin wao wanazuga kwa kugawa hayo mafuta, chumvi au maji bure kwa wachache kisha wanaanza KUYAUZA. Je, tangu lini NGUVU ZA MUNGU HUWA ZINAUZWA? Sama sio utapeli ni nini?

Lakini naenda mbali kidogo kama kweli wao ni wajumbe wa Mungu Kwanini wasitufundishe sisi wenye shida namna ya kukaa vizuri na Mungu ili hatimaye, watufundishe kuyaombea hayo maji, chumvi na mafuta ili vitufae kwa shida zetu? Kama sio mfumo wa kutuibia na kututapeli ni nini?

Nawaonea huruma watu ambao wanzidi kudanganywa na kuibiwa. Kwa wanaomwamini Mungu wanajua kuna maisha mengine baada ya hapa duniani. Hawa mabwana huwa hawahibir hizi habari zaidi ya kuzungumza kuhusu mafanikio tu. Kwanini wasijadili na kesho yetu pia?

Kwa leo tuishie hapa lakin huu ni uzi huru. Mawazo huru yanakaribishwa.

ITAENDELEA
 
Hivi binadamu wa kawaida unawezaje kuwatapeli watu wengi kama wale wa kwa mwamposa??!???..yule jamaa ana nguvu gani?..hata kama ni uchawi,inawezekanaje kuroga watu wote wale?
 
Hivi binadamu wa kawaida unawezaje kuwatapeli watu wengi kama wale wa kwa mwamposa??!???..yule jamaa ana nguvu gani?..hata kama ni uchawi,inawezekanaje kuroga watu wote wale?
Kuna mjadala hapo kwenye hoja yako, hebu tuchukulie dsm ina watu wenye shida mbalimbali wanaofika labda 5M, hawa mabwana wa miujiza tufanye wapo watatu. Je tangu wameanza kuwaponya hawa wenye matatzo hawaishi tu?
 
Upo sahihi kabisa mtu wangu,ulichosema ndicho kinachoendelea. Nina shangazi yangu hawa wanaojiita watumishi wanamfilisi kila uchao.
Ni kweli kabisa mkuu. Hata Mimi Nina shemeji yangu sasa hivi hana hamu tena na hawa jamaa, wamempiga pesa nyingi mpaka katosha mwenyewe, kwa sasa hataki hata kuwasikia yaani
 
Back
Top Bottom