MATARAJIO YA WATANZANIA KWA MHE SAMIA, RAIS WA JMT NI MAKUBWA
Na Elius Ndabila
0768239284
Jana Mhe Samia Samia Rais wa JMT amefanya mabadililo madogo kwenye Baraza la Mawaziri yaliyotanguliwa na uapishwaji wa Makamu wa Rais. Katika kuendelea kuhakikisha matarajio aliyonayo ameendelea kupanga safu ambayo anaamini itampa matokeo. Hotuba yake fupi ya jana kama ushauri wa Mawaziri kuheshimiana inanikumbusha kwa Waziri Mkuu wa Ungereza Mwanamke aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa Margaret Thather.
Margaret Thather aliitwa "Iron Lady" kwa matukio yake ya kisiasa yenye maamuzi magumu bila ya kuyumbishwa. Ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu nchini Uingereza kuanzia mwaka 1979 mpaka 1990 katika kipindi ambacho Dunia ilikuwa inapitia katika kipindi cha vita baridi.
Anajulikana kwa misimamo yake iliyomfanya wengi wamchukulie kama mwanaume, ameshika wadhifa wa Uwaziri mkuu kwa muda mrefu zaidi katika karne ya 20. Licha ya Vita baridi iliyokuwepo kati ya Kambi ya Mashariki (Urusi) dhidi ya Magharibi (Marekani, Uingereza, Ufaransa), Margaret Thatcher katika uongozi wake alikumbwa na Vita ya kugombea Visiwa vya Falkland dhidi ya Argentina. Lakini chini ya uongozi wake imara aliibuka na ushindi katika vita hiyo.
Katika utawala wake alijenga urafiki wa karibu sana na Rais wa Marekani wa kipindi hicho ndugu Ronald Reagan na ushirikiano wao ulifanikwa kuiangusha USSR katika vita baridi. Mwaka 1990, Iron Lady alijiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu wa nchi hiyo pamoja na ile ya Uongozi wa chama chake cha Conservative.
Alicho fanya Mhe Rais ni jambo la kawaida kwenye utawala. Kwa mfano Kocha wa mpira anapoingia uwanjani lazima uwe na timu ya uhakika. Ni kawaida kwa kila kocha kuwa na mfumo wake wa uchezaji anaodhani utampatia matokeo uwanjani. Wapo Makocha wanaamini katika mfumo wa 4:3:3, wapo wanaamini katika 4:4:1 na wapo pia wanaamini katika 4:5:1. Makocha wote hawa wanataka matokeo na maelezo ya namna ya kucheza uwanjani kocha anawaelekeza.
Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wengi wanapopata nafasi ya madaraka makubwa hufanya kazi vizuri na kuacha matokeo makubwa. Wanawake kwenye uongozi wanaamini katika matokeo chanya na ndiyo maana jamii zinaamini kuwa ukimuelimisha mwanamke mmoja umeelimisha jamii yote. Mama Samia ukifuatilia historia yake ni Mwanamke mahiri, shujaa na Hodari ambaye hajawahi kufanya vibaya kwenye nafasi aliyowahi kufanya. Kuna video moja ya Mhe Rais amekuwa ikitembea ambayo anasimulia Maisha yake. Inaonyesha wazi kuwa alianza kuwa na Kariba ya kuongoza toka akiwa kwenye nafasi ndogo kwa kuwa anasema kila nafasi aliyokuwa anapata basi alikuwa anakuwa mfano wa kufanya kazi kwa bidi katika eneo hilo. Hii inaonyesha ana haiba ya uongozi ndani yake ndiyo maana nafasi zake ni za kupanda. Taswira ya Mhe Rais inanirudisha kuwatazama wanawake wengine ambao baada ya kupata nafasi kubwa basi waliweza kuacha historia chanya.
Ipo mifano mingi ya wanawake duniani ambao wananipa nguvu kuwa Mama SAMIA ataingia kwenye historia kubwa ya kuijenga Tanzania, hasa kutokana na mwanzo alioanza nao. Katika afrika mwanamke wa kwanza kushika nafasi kubwa ya Urais na kufanya vizuri ni Rais wa Liberia Mhe Ellen Johnson Sirleaf kuanzia mwaka 2006 mpaka 2018 akiiongoza nchi ya Liberia. Anajulikana kama Indira Gandhi wa Afrika akifananishwa staili yake ya uongozi na aliyekuwa kiongozi mahiri wa nchi ya India. Mtetezi mkubwa wa haki za wanawake barani Afrika hali iliyompelekea kutwaa Tuzo ya Amani ya Nishani ya Nobel kwa mchango wake huo. Uongozi wake ulileta umoja wa kitaifa katika nchi hiyo iliyopitia kipindi kigumu cha vita ya wenyewe kwa wenyewe kabla ya hapo.
Hakuupata Urais kirahisi, kwani mwaka 1980 alilazimika kukimbilia Uhamishoni chini ya utawala wa Dikteta Samuel Doe. Bibie Ellen alikimbilia Marekani kabla ya kurudi tena nchini Liberia na kugombea Urais mwaka 1997 na kuishia kushika nafasi ya pili nyuma ya Charles Taylor. Hakukata tamaa na hatimae mwaka 2005 akashinda Urais.
Mifano hii duniani ipo mingi, lakini pia unaweza kuangalia kiongozi aliyeijenga Ujerumani na kujipatia umaarufu mkubwa ni mwanamke. Angel Markel Ndiye Kansela wa sasa wa Ujerumani, mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo. Anatajwa kama mwanamke jasiri na mpambanji na mwenye nguvu duniani kwa sasa. Ameshika wadhifa huo toka mwaka 2005.
Aliolewa na kuachika mwaka 1982 na mwanafizikia Ulrich Merkel kabla kuolewa na mumewe wa sasa Mkemia Joachim Sauer. Licha ya kuachika na mumewe wa kwanza mwaka 1982 bado ameendelea kutumia jina la mumewe huyo (Merkel) mpaka leo.Angela Merkel hajawahi kupata mtoto katika maisha yake.
Yote haya yanathibitisha nguvu ya mwanamke katika kuibadilisha jamii. Katika mabadiliko aliyoyagusa jana ni pamoja na Wizara mhimu kabisa ya mambo ya nje. Wizara hii ni mhimu na ndiyo moyo wa diplomasia ya uchumi (soma Makala yangu ya jana jtano kwenye gazeti la Afrika Leo). Mabadiliko haya mhimu na kwenye Wizara mhimu ni dira tosha kuwa Mhe Rais anahitaji kukimbia na si kutembea na zaidi kuendelea kuimalisha mahusiano katika uhusiano wa Kimataifa yaliyoasisiwa na hayati Baba wa Taifa.
Ninamuona Mhe Samia anayeenda kuvunja historia ya wanawake kama akina Golda Meir, Indira Gandhi, Benazir Bhutto, Condoleezza Rice n.k, kubwa tumpe ushirikiano mkubwa ili yale anayoyakusudia kufanya aweze kuyafanya. Asiwepo wa kumkwamisha. Amewapa heshima wanawake kwenye Wizara nyeti ni matarajio yake anawaamini, nendeni mumsaidie.