Matatizo matatu makubwa kwenye Dira ya Taifa 2050

Suala la ukuaji wa demokrasia limezungumziwa kwenye hiyo dira?
 
Itikadi za Viongozi wa kisiasa,.Dira imejikita kwenye Uchumi utakaoongozwa na soko.lakini hii itategemeana na Kiongozi wa siasa za kipindi hicho ,usitegemee watu kama kina Mwendazake kufanikisha Dira.
Dawa ya Kuzuia hilo la wanasiasa kupangua au kufanya meddling katika hiyo dira ya ya taifa, ni kuandaa mazingira katiba itakayozuia hilo lisitokee...na kwa upande mwingine katiba hiyo kutoa mwongozo kwa vyama vya siasa kupanga sera zao kwa kwenda sambamba na dira ya taifa....na kimsingi chama kilichopo madarakani kinatakiwa kutekeleza dira kama ilivyopangwa,vyama vya upinzani vinatakiwa kufanya counter-check.....,kiufupi katiba haitakiwi impe uhuru na mwanya kwa rais kufinyanga anavyotaka.
Kuna jambo moja zuri...,hiyo dira yenyewe imefanya ukuzwaji wa demokrasia kuwa moja ya malengo yake makuu.....,na kutokana na hilo swali moja, ...midhali dira ya iliyopita iimeisha...,inaanza mpya 2025, kwa nini kusitengenezwe katiba mpya sasa ikiwa uboreshwaji wa demokrasia ni moja ya sehemu ya dira yenyewe? Na tukizingatia kwamba uwekezaji ni sehemu muhimu ya ukuzaji wa uchumi kwa vile hakuna wawekezaji watakaotaka eneo ambalo halina demokrasia au uongozi usiotabirika au usio na uwazi.
 
Angeitwa Lipumba hawa kwa hili ni wasanii halafu 2050 karibu wengi hawatakuwepo wangelenga ilani ya miaka 5 juu ya matatizo ya uchumi na ajira kwa vijana lakini huu ni usanii wa ajabu
Kuelekea maika 25 baadae dira inasemaje mwezi Agost 2025 maana we live once. Once you plan 25 years to come also plan 2 days to come. Tunahitaji kuishi miaka 25 iendane na kesho maana tulikuwa 2000- 2025 imeisha bado hali ni tetee kinachokuwa katika Nchi yetu ni DENI ila maendeleo ni chemichemi.
 
Kwa katiba yetu ya sasa ilivyo inampa nguvu kubwa rais kama msimamia mkuu wa dira ya taifa kwenye utekelezaji.

Kwaiyo rais wa nchi lazima awe na maono, mwenye uelewa mkubwa, msimamizi mzuri wa rasilimali za taifa na kichwani awe smart, je wa kwetu ana sifa hizo?
 
Kama kwa miaka 25 iliyopita uchumi umekuwa mara 6 maajabu gani unafikiria yatafanyika ukue mara 12 kwa miaka 25 ijayo??
Kilimo kinachangia robo tu(25%) kwenye GDP ya Tanzania.
Unatakiwa uangalie Growth ya hicho kilimo, on average kilimo kinakua kwa Asilimia 11% between 2005 na 2024 kwa mwaka, Gdp yetu ikifika pakubwa sana ni 8% ila most of time tunacheza humo 6-7.

So kilimo kinakua, Sometime Percentage ukiangalia inaweza kuku deceive, kilimo percentage ya Gdp imeshuka toka 28 hadi 25 ukaona kama kimeshuka, ila unakuta percentage imeshuka sababu kuna diversification ya Uchumi na sio kushuka uzalishaji.

Pia ukuaji uchumi unatakiwa upige hesabu kwa Compound as I told you asilimia 6-7 inatosha kukupa hio figure ya Serikali ya 500-700B, Asilimia 10-11 inakupa figure ya Rostam ya 1T, asilimia 6-7 ndio figure yetu ya sasa, any favourable Economic Condition ina maana tutazidi hio figure, unlikekly ila sio impossible kabisa.
 
Sisiemu haijawahi kuwa na Nia njema na watanzania
 
Kwanza iwe mwaka, mwaka. Raia hata hawajui watakachofanya kesho kutwa dira za miaka mi5 za nini?

Serikali kuu ipewe pesa za ulinzi na usalama itulinde maendeleo yawe kazi za mkoa husika tupeane dira za mwaka mwaka. Hahaha.
 
Walicho tambulisha leo ni muendelezo wa vichekesho vya bibi chaudere ametaka kutu changamsha tuu, Ni watu wachache tuu wamekaa waka tengeneza "script" ya futuhi wakaipachika jina hilo kanyaga twende
 
Uchumi nao una dira yake.Kuwafanya watu wachache ndiyo wawe na uchumi wa juu kuliko waliowengi.Na ndivyo ilivyo.Ukitaka kupunguza gap basi kuwe na uongozi bora wa kuaminika na wengi
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja inayoundwa na Tanzania Bara naTanzania Zanzibar, ikiwa na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba (km2) 948,740,zikiwemo km2 61,500 za maziwa na mito

wakuu ndo naanza kuisoma hii dira na nakutana na hali kama hiyo, hii inanipa wasi wasi kama imefanyiwa mapitio zaid na zaid na wataalamu/wasomi wetu kabla ya kutufikia sisi.
JE NI SAHIHI KUSEMA TANZANIA BARA NA TANZANIA ZANZIBAR?
 
Ili huo uchumi ufikiwe ni lazma ccm ienguliwe kwa sisiemu hii na mahakama hiizi. Narudia kauli zile zile za rostam akosema mahakama hazipo huru. Hakuna uhalisia
 
Kwann usiseme inayoundwa na Tanganyika ja zanzibar hakuna tanzania bara na tanzania zanzibar
 
Watu ambao kuanzia ‘Millennium Declaration’ mwaka 2000 wazungu wameona jamani enhe hawa wenzetu wana hali mbaya embu tuwasaidie kuondoa umaskini wa kutupa walionao.

Miaka 25 baadae baada ya kupewa ma trillion lakini maji bado hakuna maeneo mengi tu ya Tanzania na less than 10% ya graduates ndio wanao pata ajira.

Na pengine kwa takwimu sahihi ukute GDP per capita bado ipo kwenye number za low income country.

Hata msukuma mkokoteni wa aluminium akisoma hiyo ni dira atakueleza hii ‘pie in the sky’ Hakuna kingine.
 
Pesa zonaishia mikononi mwa wanasiasa
 
Hi ni wishes zao na sio mpango mkakati wa taifa.
 
Dira inatakiwa kuwekewa uzio kikatiba, maana tumezoea kila rais akiingia anatenda kulingana na maono yake.

Jambo la kustaajabisha ni kwa CCM kama chama tawala kuandika ilani yake kabla ya dira haijatoka!

Katiba inapaswa iseme kuwa vyama vitatengeneza ilani zao, sera zao kulingana na dira ya taifa ya maendeleo, lakini sio dira hii iliyozinduliwa.
 
Hao wakulima wapo vizuri kwenye makaratasi??
Mimi nalima pamba maswa, sijaona lolote zaidi nitaachana nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…