Jamani msisingizie wahindi au mmsahau kuwa reli tulivyoirithi baada ya kuvunjika kwa EAC? Reli ya TZ ndiyo ilikuwa inalipa kweli na tulisaidiwa sana kuiimarisha lakini matokeo yake tuliiua wenyewe. Huwezi kuamini lakini kama mashirika mengine ya SU yalivyokwisha basi na reli ni hivyo hivyo. Enzi za EAC ilikuwa vigumu sana kuiba hata senti 5 maana ilikuwa ni kufukuzwa na kupoteza haki zote.
Baada ya kuwa yetu ubadhirifu uliongezeka wafanyakazi waliajiriwa karibu mara 2 kuliko ilivyokuwa wakati wa TRL matokeo tuliua mtaji ndiyo maana ikatushinda.
Ilivyotangazwa tenda kila aliyekuja na kuona hali ilivyo alichomoa ndiyo maana tukapata hawa ndugu zetu wa india. Huwezi kuamini hata wafanyakazi wenyewe ndiyo wahujumu wakubwa unadhani kuna kitu hapo?????
Hili ni fupa ambalo sijui nani ataliweza maana ni WIZI MTUPU kuanzia kwetu wazalendo hadi wageni hawa. Jee nani wakulaumiwa? kama sisi wenyewe tumekosa uzalendo nani atakua nao?