DOKEZO Matatizo wanayopitia watumishi wa umma Masasi, Nachingwea…

DOKEZO Matatizo wanayopitia watumishi wa umma Masasi, Nachingwea…

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Masasi, Nachingwea(MANAWASA) ni taasis ya serikali kama taasis nyingine lakini ni taasis ambayo inaendeshwa kwa matakwa ya mtu mmoja tuu ambaye ni Mkurungenzi mtendaji anaye fahamika kwa majina Eng. David Nntufye,

Mkurungenzi mtendaji huyu anaendesha hii taasisi kama yake, ndio maana imefikia hatua anafanya anachotaka bila kujali maslahi ya watumishi mfano.

1. Amechukua bomba za chuma kati ya (100-110) ambazo zilikuwa ofisi kuu ya Masasi na zilibebwa na gari ya serikali yenye namba ya DFP 7324 (Bombadier) iliyokuwa ikiendeshwa na dereva anayejulikana kwa majina ya Nicolaus Haule na kupelekwa kwake bila kibali chochote kisga kusafirishwa kwenda Dar es salama.

2. Kutokuwalipa watumishi stahiki zao kama vile muda wa ziada na nauli za likizo kwa kisingizio Mamlaka haina pesa huku hakuna siku vikao vya bodi vinakaliwa na kuambiwa kuwa hakuna pesa mfano wa kikao cha bodi ni cha tarehe 05.05.2023 watalipwa wajumbe wote vizuri ila watumishi watabakia wakiendelea kuambiwa hakuna pesa.

3. Watumishi kutopatiwa muda wa mafunzo ata kama wakiomba, Mkurungenzi mtendaji amekuwa akituambia mafunzo si haki kwa watumishi.

4. Watumishi kufukuzwa kazi bila kuzingatia kanuni za kiutumishi

5. Bodi inapewa thamani kubwa kuliko watumishi,ili kurahishisha katika maamuzi yao ya kuwakandamiza watumishi.

6. Tunaweza sema Mamlaka yetu hii haina Meneja utumishi kwani yeye ni mtu wa Mkurungezi mtendaji na sio daraja la kuonganisha watumishi na menejimenti. Meneja utumishi amekuwa ni mtu wa kukandamiza watumshi bila kujali sheria zinasemaje.

7. Tunaomba safari za Mkurugenzi mtendaji zichunguzwe kwani ana safari nyingi ambazo zinahisiwa ni hewa.

8. Pia kuna watumishi wapo kwenye adhabu za kinidhamu na bado wamepandishiwa mishahara hapa pamekaaje.
 
Back
Top Bottom