Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MATATIZO YA AFYA YA AKILI.
-Shirika la Afya Duniani (WHO) linataja kuwa kabla ya janga la COVID19, takriban mtu 1 Kati ya 8 Duniani kote walikumbwa na matatizo ya kiakili, hata hivyo Msaada sahihi wa miundombinu na kiuchumi kwa ajili yao, ulikosekana
-Matatizo ya afya ya akili yapo katika maisha yetu, familia, sehemu za kazi na jamii, na kuathiri kila mtu.
Dalili za matatizo ya akili ni pamoja na:
•Kuwa na hasira kupindukia
•Kukosa furaha katika maisha
•Kuwa na wasiwasi wa kupindukia
•Kukosa usingizi
•Kuwa na msongo mkali wa mawazo
-Ni lazima tufanye kadiri tuwezavyo kuzuia magonjwa ya akili - kama watu binafsi na kama jamii.
-Ni muhimu kuendelea kutoa wito kwa serikali za kitaifa na za mitaa kuweka kipaumbele katika kupunguza mambo yanayojulikana kuwa hatari kwa afya ya akili ya watu Kama Ugumu wa Maisha, Migogoro ya Kijamii na Kimapenzi, Unyanyapaa wa Watu wenye Mahitaji Maalum pamoja na dhana au Mila potofu katika jamii.
-Pia kuimarisha wale wote wanashughulika na kulinda afya za akili kuanzia mtu Mmoja Mmoja hadi mashirika binafsi na kuunda nyenzo zinazohitajika kwa watu kustawi.
NJIA ZA KUJIKINGA NA CHANGAMOTO ZA AFYA YA AKILI
▪️Jikinge na changamoto za afya ya akili kwa kufanya mambo yafuatayo-
➖Husiana (Changamana) na wengine. Huongeza thamani yako na kufanya ujione ni sehemu ya familia yako, ukoo na jamii nzima kwa ujumla.
➖Mazoezi huwa hayaishii kwenye kuongeza utimamu wa mwili pekee bali huchangia mienendo chanya ya mihemko ya mwili. Shiriki mazoezi.
➖Kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Pia jifunze kuchukua likizo fupi pindi unapohisi kuwa baadhi ya mambo unayoona huko yamekuwa chanzo katika kukukosesha furaha.
➖Usiwe mgumu kuonesha hisia zako kwenye nyakati zote za maisha pasipo kujali jinsia yako. Penye changamoto vunja ukimya, eleza yanayokusibu.
➖Kuwa mkarimu. Aidha, tabia njema za kushukuru, kusamehe, kuomba msamaha wengine pamoja na kuridhika na mafanikio binafsi pasipo kujilinganisha na wengine husaidia kuilinda afya ya akili.
➖Jiepushe na matumizi ya dawa za kulevya.
NB:Kama unasumbuliwa na Ugonjwa wowote ule karibu upate ushauri na tiba lishe
Chanzo: WHO / Mental Health Tanzania.