Matatizo ya Afya ya Akili sio Ukichaa

Matatizo ya Afya ya Akili sio Ukichaa

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Nimeona kuna hajanya watu kuelewa vizuri ili suala la afya ya akili ambalo watu wengi wamekuwa wakidhani matatizo ya afya ya akili ni ukichaa.

Matatizo ya Afya ya Akili inaweza kuwa Phobias za Aina zote, Depressions, Stresses nk ambapo sio lazima uwe ukichaa

Nimeshangazwa na mtu mzito kama Pascal Mayalla hajui hili kiasi cha kuuliza kama wanaokataa chanjo ni vichaa kwenye uzi alianzisha leo


Matatizo ya Afya ya akili huweza kuleta matatizo mbalimbali ikiwemo kujiua, kutokana na shida ya uelewa wengi huwa na hali ya kukataa kwa kuwa wote hudhani ni ukichaa

Hali ya kukataa huleta shida katika kutafuta suluhu, lakini ukataaji hutokana na namna jamii inavyoamini, wengi huogopa kuambiwa una matatizo ya afya ya akili kwa kuwa wanaona wametukanwa kwa kuambiwa chizi au namna nyingine mbaya

Jamii iamke, mambo ya watu kupiga watoto, wapenzi hadi kuua mara nyingine husababishwa na shida hizi.

Tusiendelee kudhani shida za afya ya akili ni ukichaa... ni sawa tu kusema huyu anashida kiafya moja kwa moja ukadhani ana UKIMWI

The same issue ilionekana kwenye gazeti ambalo liliandika ile ratio kwamba wenye matatizo ya afya ya akili ni 1:4 ambapo gazeti likaandika kati ya watanzania wanne mmoja kichaa, and it went on kwa kuwa wote hawakutaka kujifunza zaidi

Change the mind set


Signed OEDIPUS
 
Back
Top Bottom