Mabibi na Mabwana habari zenu?
Niende mmoja kwa moja kwenye suala langu. Suala lenyewe ni kuhusu kiwango cha kasi katika kuongezeka watu wenye matatizo ya akili, binafsi nimejaribu kuwaza na kuwazua kujua mini haswa ni chanzo. Nimeshindwa kupata jibu kwa sababu:
Nimeishi mkoa wa Mara kwa mda, Kuna watu wengi wanamatatizo ya akili mkoa ule hususani wilaya ya bunda. Niliwauliza bahadhi ya watu waliniambia "Tatizo ni maisha magumu". Lakini vile vile niliwahi tembele wilaya ya urambo mkoa wa Tabora, nikakuta Kuna watu wengi wana matatizo ya akili, sababu nilizoambiwa ni kwamba "tatizo ni bangi zinapulizwa sana kule, jibu hili halina utofauti na sababu zinazotolewa na katika mikoa ya Dar es saleem na Arusha-Madawa ya kulevya kuwa ndiyo chanzo.
Lakini pia Kuna sababu zinazotolewa kwamba chanzo cha watu kwenye matatizo ya akili " machizi" chanzo ni "kutolewa kafala" au "ushirikina" kwa sababu mbali mbali kama vile bihashara, vyeo/madaraka, visasi n.k
Hizo ndizo sababu haswa zinazozungumzwa, lakini kwa mujibu wa sababu za wataaalamu mbali mbali wanasema chanzo kikuu ni MSONGO WA MAWAZO. Lakini msongo huo unatokana na mini haswa?
Watanzania Wengi Wana Magonjwa ya Akili
AFYA ni nini? -Afya ni ile hali ya kuwa na hali bora kimwili,kiakili na kijamii pasipo kuwa na namna ile yenye udhaifu.
'
Afya ya akili ni nini?' - Wote humu tupo na Afya ya Akili, kama ilivyo miili yetu kutokuwa sawa wakati fulani, akili zetu pia huwa zinakuwa hazipo sawa wakati fulani.
Msawazo kati ya afya ya kimwili,kiakili na kijamii ni muhimu sana kutosha kufikia ubora wa hali njema ya mtu mmoja mmoja,kifamilia na jamii kwa ujumla.
Afya ya Akili ni Uwezo wa kujikubali na kukubali wengine,kupokea na kuchukuliana na hisia , na kukabiliana na matatizo na changamoto unazokutana nazo maishani. Ni hali ya mtu kugundua na kutambua uwezo wake , anayeweza kuchukuliana na misongo ya maisha ya kila siku, anayeweza kuzalisha na kuweza kutoa mchango wake kwa maendeleo ya jamii yake.
Ni muhimu sana kuongea kuhusu maswala ya Afya ya Akili na muhimu sana kupata msaada mapema kama mabo hayaendi sawa sawa,kama jinsi inavyokuwa tufanyavyo kwa Afya ya Kimwili.
KWA KIASI GANI MATATIZO YA AFYA YA AKILI NI KAWAIDA SANA KUTOKEA? - Ni kawaida sana kwa wote, watu wazima na watoto kupitia huu uzoefu wa kuwa na matatizo ya akili kwa nyakati tofauti katika historia ya ukuaji wao. Wasiwasi,Sonona,kufurahi kupita kiasi au matatizo sugu ya maradhi ya akili huathiri sio tu familia na marafiki,lakini pia huleta athari ya kuhafifisha ubora wa maisha,hupunguza uzalishaji katika maeneo ya kazi au shule na hupelekea kuwa na madhara zaidi katika utu wa mtu , mfumo wake wa mawazo na jinsi anavyojihusisha katika jamii.
MARADHI YA AKILI YANASABABISHWA NA NINI? - Afya na Maradhi ni matokeo ya kibaiolojia,kisaikolojia na mazingira.(Biopsychosocial formulation). Badiliko la namna moja huweza kuathiri eneo lingine na vivyo hivyo kwa lingine pia. Hii modeli inaaminisha kuwa Afya ya Kimwili na Maradhi hutegemea mambo makubwa matatu kwa namna yanavyohusiana kwa namna zake. Upo udhaifu utokanao na namna ya kibaiolojia-kurithi vinasaba , upo udhaifu utokanao na namna ya kisaikolojia - mapito ya makuzi aliyopitia tangu mimba yake mpaka umri wa kubalehe au kuvunja ungo. Na hapa inategemea falsafa yake ya maisha imejengwaje,hisia zake zimejengwaje na utu wake pia umekuzwaje. Mwisho ni sababu ya ki-mazingira eeh,jamii yake aliyopo kwa wakati huo ipoje kulinganisha na jamii zingine ( social culture context )
Tabia za mtu mwenye Afya Njema Kiakili.
1. Huwa na amani na nafsi zao.
2. Anaweza kufikia mahitaji ya maisha vizuri.
3. Hujihisi amani hata miongoni mwa watu wengine.
4. Huwasilisha hisia zake katika namna yenye afya.
5. Ni mtu ambaye huona fursa njema kwa kila jambo mbele yake ( Optimistic )
6. Hutumia njia bora katika kushughulika na misongo,kufanya maamuzi,kutafuta suluhu,
7. Mtu wa kukubali mabadiliko hasa inapobidi.
8. Msikivu mzuri.
9. Anapenda kujielezea mwenyewe jinsi anavyochukulia mambo.
Tabia za mtu mwenye Afya mbovu ya akili/maradhi ya akili.
1. Hashirikishi watu / mtu hisia zake.
2. Huchukulia rahisi matatizo.
3. Hakubali mabadiliko.
4. Hukubali msongo uendeshe maisha.
5. Hisia huendesha maisha.
6. Mtu asiyeona fursa / jema machoni pake ( pessimistic )
7. Mtu wa kulaumu sana, kulaumu wengine au kujilaumu mwenyewe.
8. Mtu mwenye sononeko.
9. Hukimbia matatizo.
10. Akili mgando - hawezi kujiongeza.
Nia bora nane ( 8 ).
1. Ongea - Kuwa wazi kwa watu unaowaamini.
2. Mzoezi - Tunza mwili wako kwa njia ya mazoezi , ulaji bora kiafya.
3. Utulivu - Pata muda mzuri wa kupumzika , zima simu yako mapema , jaribu pia 'meditation'
4. Soma - Kujifunza na kufahamu mambo mengi mbalimbali huongeza namna ya kujiamini.
5. Mahusiano - Pata muda wa kukaa na watu unaowajali na kuwapenda. ( familia kwanza )
6. Ubunifu - Onyesha uwezo wako katika ubunifu wa mambo kadha wa kadha mfano. Uandishi, Mziki nakadhalika.
7. Jipongeze - Kuwa mwema kwa nafsi yako , andika mambo kadha wa kadha unayoyathamini.
8. Changia - Saidia wengine kufikia malengo yao , weka nguvu kutia shime mambo unayoamini yanapaswa kuwa kwa jinsi yanavyopaswa kuwa.