Kichwa cha habari kinahusika.
Walau CCM kama chama pamoja na madhaifu yake mengi kuna mambo watanzania walikivumilia kutokana na mila zake. Licha ya chama kulea ufisadi na kuwalinda mafisadi kwa muda mrefu bado kiliishi kwenye misingi. Hatukuwahi kupata kiongozi mwenye madhaifu mengi yanayotishia hadi mustkabali wa chama cha Mapinduzi seuze nchi kwa ujumla.
Mtaniwia radhi kuusema ukweli huu mchungu. CCM kama chama kilithubutu kuwadhibiti wanachama wake pale wanapokwenda kinyume na misingi ya Taifa hili lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere na wenzake. Huyu Magufuli kuna kila dalili CCM imemshindwa.
Nasema pamoja na Madhaifu ya CCM bado kulikuwa na alama zile zile za kuimarisha UMOJA, MSHIKAMANO WA KITAIFA na AMANI YA KWELI.
Watanzania waliendelea kuvumilia hivyo hivyo. Awamu za CCM zilipita ikafika wakati CCM yenyewe ikahitaji mtu mkatili. Lakini sio ukatili huu wa UMOJA WETU, MSHIKAMANO WETU na UTU ambao chini ya awamu ya tano ya Magufuli imekubuhu.
Vuta picha, awamu zote uone kama watanzania walikuwa walivyo leo. Hapa pasilinganishwe mabara bara na mareli maana tokea wakati wa Mkoloni zilikuwepo.
MAGUFULI HAVUMILIKI.
Mnaoelewa muelewe wekeni siasa pembeni.
Hebu tafakari upendeleo wa wazi wa kikanda, ukabila na maneno ya kuudhi kutoka kwa mkulu. Yaani ndani ya miaka mitano imedhihiri kutumia rasilimali za Taifa kinyume na taratibu(Uwanja Chato, mbuga, teuzi n.k) Kwa kutumia madaraka yake hata mfumo wetu wa kupitishwa bajeti na kupata baraka za bunge kwenye mambo ya kibajeti yaliwekwa pembeni.
Hebu tafakari anavyoligawa Taifa na kuchochea ubaguzi kwa maeneo ya upinzani. Si mara moja, mbili wala tatu amenukuliwa kutoa maneno ya kuwatia adabu wananchi wa maeneo fulani kisa kuwachagua wapinzaniu. Hata kwenye kampeni zake zinazoendelea anadiriki kuwafokea wananchi na kutoa amri wasichague upinzani na kwamba yeye hajaribiwi. Hii ni hatari. Watanzania tutafanya makosa sana kumchagua mtu hatari namna hii kwa mustkbali wa Taifa hili. Anasahau kuwa Wapinzani ni watanzania na yeye kama kiongozi mkuu wa nchi anawajibika kuleta maendeleo kwa wote.
Hebu tafakari maamuzi yake mengi yanavyodhalilisha wengine kwenye teuzi. Hata wanachama wenzake wa CCM hawafurahishwi. Huo ndio ukweli. CCM inalazimika kumeza madhaifu ya mtu na chama kudhalilishwa mbele ya umma wa watanzania na kimataifa.
Hebu tafakari sheria nyingi kandamizi kuhusu habari, demokrasia na uwazi zilivyotamalaki kwa sababu ya mtu mmoja Rais Magufuli. Yaani madhaifu yake binafsi yamefanywa madhaifu ya Tanzania, CCM na weananchi wote. CCM kama chama kilijitahidi kuichora nchi kwa kubalance mambo. sasa Magufuli mizani yake imelala upande mmoja wa madhaifu kuwa ndio picha ya Tanzania nzima. Haya hayavumiliki.
Hebu tafakari mifumo yetu ya mahakama, vyombo vya kimkakati kama TAKUKURU, POLISI na taasisi zengine zinavyotumika vibaya zaidi kuliko wakati mwengine ule chini ya CCM ile ile. Hapa ndipo unapomuona Magufuli kuwa havumiliki. Vyombo hivi vinadiriki kubambikizia watu kesi na kuvuruga mifumo yetu. Vinatumika kuwashughulikia wote wanaompinga Magufuli iwe mwana CCm au mpinzani. Bila kujali legacy inayojichora , kwa kumfurahisha mtu mmoja tu, basi taswira ypote na dhamira ya kuanzishwa kwa vyombo hivi imepata doa baya zaidi kipindi hiki cha Magufuli. Nani atabisha?
Hebu tafakari uharibifu wa utaratibu wa Chaguzi zetu ulivyofujwa kuliko wakati mwengine wowote wa CCM. Tafakari chaguzi za marejeo na vimbwanga vya wakluirugenzi wa majiji na halmashauri walivyotumika. tafakari uchaguzi wa Serikali za mitaa na hadi sasa uchaguzi mkuu.
Magufuli ameasisi vitisho kwa wafanyakazi aliwateua na kupalilia woga na kutotendeka haki. Haya kayaasisi yeye tu ndani ya tawala zote za CCM zote zilizopita
Hebu tafakari namna Tanzania inavyotolewa matamko mengi na shutuma za kuminya haki za binadamu, demokrasia kuliko wakati wowote na kuiweka Tanzania pahala pasipo.
Kuliko yote tafakari anavyovuruga UMOJA WETU na MSHIKAMANO WA KITAIFA hadi kudiriki kuzigawa taasisi za dini na kuziingiza kwenye siasa mbaya za kusifu badala ya kuonya na kuimarisha haki.
Haya mambo hayavumiliki na Magufuli kwa haya tu basi havumiliki.
Kishada