Uchaguzi 2020 Matatizo ya CCM kama chama yangevumilika, Magufuli havumiliki huo ndio ukweli

Kabisa. Hakuna mtanzania mwenye nia njema na nchi hii anaweza kumchagua Magufuli. Habebeki kwa chama Wala kwa wananchi.
Yani anachukulia watu hadaa ili tu akirudi amalizie yale yaliyojificha. "Sumu hajaribiwi mara mbili ukipona mara ya kwanza"
 
Mnyonge tumnyonge lakini haki yake tumpe. Kulingana na taaluma yake kama Mwanasayansi, amefanya yale ambayo mwanasayansi anatakiwa kufanya. Siku zote Mwanasayansi anajali kujenga, kuunda, kugundua, kutafiti nk.

Haya ndiyo anayoyafanya. Mafanikio ya Mwanasayansi ni ya Vitu na si Watu. Lakini mwisho wa siku vitu alivyofanikisha vitamsaidia huyo mtu. Tatizo ni kuwa vitu vinavyoshughulikiwa na Mwanasayansi , manufaa yake hayaji mara moja na yanawaumiza wale wanaoishi kipindi kile.

Mchumi, kwa sasa anasema kipato cha mtu moja moja au kipato cha kaya kimeshuka sana kulinganisha na wakati wa awamu ya Nne.
Lakini uchumi wa Taifa umepanda sana.

Pesa yote imehama toka kwa mwanainchi wa kawaida na kwenda Serikalini au matajiri wachache. Huyu ndiyo mfumo wa Kiuchumi ambao kama utazaliwa maskini, utakufa maskini.
 
Mnyonge tumnyonge lakini haki yake tumpe. Kulingana na taaluma yake kama Mwanasayansi, amefanya yale ambayo mwanasayansi anatakiwa kufanya....
Baada ya yote hayo unayojaribu kuyatetea kwa mgongo wa sayansi basi ANGETUMIA SAYANSI hiyo hiyo kuulinda UMOJA WETU, UTAIFA WETU NA KUHIMIZA UHURU NA MAENDELEO YETU.

KWA UFUPI MISINGI YA TAIFA

Simuoni Magufuli wa aina hiyo.

Havumiliki.
 
Ni ukweli mtupu. Wanachama na Wapenzi wa CCm waache ushabiki kama wa Simba na Yanga kwa kubadilika na kuikomboa nchi yetu. Kama atapita miaka mingine mitano hali itakuwa mbaya zaidi hasa kwao CCM wenyewe.
 
JPM anashinda ushindi mnono uchaguzi huu wa 2020.mpaka sasa akuna mgombea alimtikisa hata chembe.
 
umeongea ukweli mtupu, ila "vibaka wa lumumba watapinga"

maana upinzani wakipinga kwa "hoja" vibaka hawa hupinga kwa "uzoefu" bila mashiko.
 
Hakika huo kweli ndio ukweli! Binadamu asiye na ubinadamu hafai na wala hawezi kuongoza binadamu wenzie! Atawaswaga kama ng'ombe au kuku! Lazima mwaka huu tuchaguwe binadamu mwenye ubinadamu, miaka 5 ya kuswagwa imetosha!
 
Ikitokea watanzania wakamchagua Magufuli tena kwa miaka 5 si Mungu tu atatushangaa ila hata shetani atatushangaa sana!!...
Kwa taarifa yako huyu ndiyo Rais na ataendelea kuwa Rais hadi mwaka 2025 na baada ya hapo tuna mpango.wa kumuongezea muda.
 
Magufuli havumiliki, akipita miaka mitano ijayo wafanya biashara wajiandae kufa mno , hizi examination, verification na audit tena kwa miaka mingi ya nyuma ni balaa
 
huyu alitakiwa kuwa mnyampala wa barabara ,hiyo maneno ya kingnge ngombale mwilu
 
sera ya majimbo ni nafuu mara alfu 10 kuliko sera ya ccm ya kulundika madaraka yote ya nchi kwa mtu mmoja tu anayeitwa Rais. Baba wa Taifa alitahadharisha kuwa sera hii ya ccm ni khatari mno na kwamba chini ya sera hii akipatikana kiongoz dikteta watanzania tutakwisha..maguful amepatikana na kweli watanzania tumekwisha.

Baadhi ya viongozi wa ccm kwa kuiona khatari ya udikteta wa maguful walishtuka na kushauri katibaiandikwe upya ili ipunguze madaraka ya huyu mtu lakin maguful alikataa kata kata kwa kujijua yeye ni dikteta na katiba iliyopo ndo inayolinda udikteta wake. Leo hii maguful anamteua kila kiongoz kwenye nafasi ya maamuz nchi hii kuanzia ngazi ya kijiji mtaa hadi Taifa; hakuna hata chombo au taassisi yoyote inaruhusiwa kuhoji wala kushauri, si bunge si mahakama.

vivyo hivyo maguful anaweza kumfukuza kazi mtu yoyote kama mbwa saa yoyote ile, bila kujali utaratibu wowote wa kisheria wala kikanuni uliowekwa. Anaweza kuchukua pesa za taasisisi (mfano mifuko ya jamii) au mtu yeyote yule binafsi (maduka ya kubadilishia fedha za kigeni), mtu yeyote hata mwanaccm anaweza kukamatwa, akafungwa, akabambikiwa kesi, taasisi yoyote inaweza kufutwa na hata maisha ya mtu yanaweza kupotea na hakuna wa kuhoji.

Imefikia mahali nchi imekuwa na kundi ambalo halijujulikani lipo wap linaitwa "wasiojulikana", kundi hili limetuhumiwa kateka watanzania, kuwatia vilema, kuwatesa na hata kuwaua..watanzania hawana la kufanya, Rais amezifunga pingu mahakama, kalifunga pingu bunge na taasisi zote, yeye ni alfa na omega katika nchi ya watu zaidi ya milioni 55...naam, ni mungu-mtu chini ya sera ya ccm ya kulundika madaraka yote kwa mtu mmoja tu aitwaye Rais.

ni heri utawala wa majimbo mara alfu 10 kuliko utawala huu wa mtu mmoja. Chini ya sera ya madaraka yote kwa mtu mmoja hata wanaccm wamebatizwa kwa maji ya moto wakiwemo kina makamba, kina kinana, nape, membe na wengineo. Wastaafu wote kina mwinyi, kikwete nk wote wametiwa kelbu, yan kwa miaka mitano mwanaume nchi hii amekuwa ni mmoja tu...manguful

Kupitia chadema na ACT watanzania tuseme sasa baaaaas. Inatosha. Ni heri majimbo mara alfu 10. Uwe cdm, uwe ccm, chauma, nccr, TLP tuseme ni Lissu...tuseme ni NiYeye...TUJIKOMBOE.

Watanzania nafasi ni hii, haitakuja mara mbili mpaka miaka 5 iishe tena na kuna khatari ya huyu jamaa kung'ang'ania madaraka...tusipoangalia tutajitumbukiza kwenye shimo kwa mara ya pili ambako hatutokaa tupate nafasi ya kutoka tena mda wote jamaaa atakapokuwa hai...hata nyie ccm mtakuja kutamani kumtoa hamtoweza tena; mkihurumiwa sana mtabakia kupigishwa magoti na kuomba msamaha-rejeeni ya kinana.
 
Anachonikera zaidi ni tabia zake za udini uliokubuhu

Kwenye udini, Jiwe amepitiliza
Kateua waislamu kiduchu kupita kiasi katika teuzi zake zote alizofanya
 
TUNDU LISSU kila kunavyokucha ndivyo trend yake inazidi kupanda zaidi. Hadi kufikia 28/10/2020 sauti itakuwa ni moja tu ya kumchagua TUNDU LISSU
Mlimjaza Membe hivihivi sasa hivi mmemuacha apambane na hali yake nyie watu wa online mnazingua sana.
Membe kageuzwa Mange
 
Ameleta ukabila nchini hafai kabisa huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…