Matatizo ya choo kidogo na vijiwe katika figo

Matatizo ya choo kidogo na vijiwe katika figo

rajabumahede

Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
6
Reaction score
21
download.jpg

MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA VIJIWE KATIKA FIGO
Figo ni kiungo muhimu katika uchujaji wa Damu na kuondoa sumu na uchafu mwingine na kuutoa nje kupitia mkojo. Kiungo hiki kinakabiliwa na hatari nyingi kama hakitatunzwa vyema. Miongoni mwa athari hizo ni vijiwe vya kwenye figo. Endapo hivi vitatokea afya ya mtu katu haitakuwa salama. Mfumo wa mkojo utaweza kusumbua na maumivu kamali kumpata Mtu. Makala hii fupi itakwenda kukupa somo hili kuhusu vijiwe hivi, namna gani vinatokea na nini tufanye.

NI NINI VIJIWE HIVI?
Hivi ni vitu migumu vilivyo vidogo mithili ya vijiwe ama vi changarawe vidogo vilivyotengenezwa na kemikali za
mwilini kama chumvi na madini ya calcium. Vijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibofu ama mirija ya kupitisha mkojo.

Vijiwe hivi hutokea pale mkojo unapojikusanya kwa muda mrefu na hivyo kemikali hupata muda wa kujikusanya na kutengeneza vijiwe.

Vijiwe hivi badala ya kitengenezwa vinaanza kukuwa na kuwa vikubwa kiasi kuweza hata kuleta shida katika kutoka kwa mkojo. Wakati mwingine mtu anaweza akawa na vijiwe hivi na akaviona wakati akikojoa baada ya maumivu makali vinaweza kutoka.

Ikishindikana kutolewa kwa njia ya mkojo mgonjwa atahitajika afanyiwe upasuaji ili kuviondoa.

DALILI ZA VIJIWE VYA KWENYE FIGO
1. Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa
2. wakati mwingine mtu anaweza kupata maumivu upande mmoja wa kwenye mgongo na chini ya mbavu
3. Pia kukojoa mara kwa mara inaweza kuwa dalili ya kuwa na vijiwe hivi
4. Ijapokuwa atakojoa mara kwa mara lakini Mgonjwa atapata mkojo kidogo sana
5. Kupata kichefuchefu
6. Pia mgonjwa atapata homa

SABABU ZA KUTOKEA KWA VIJIWE HIVI
1. Ulaji anaokula Mtu unaweza ukawa ni sababu ya kutokea kwa hali hii. Kula vyakula vyenye chumvi nyingi mara kwa mara ama madini ya calcium, ama kula vyakula vyenye protini kupitiliza mara kwa mara. Vyakula hivi vinaweza baadaye kusababisha mrundikano wa hizi kemikali zinazotengeneza vijiwe hivi

2. Mashambulizi ya vimelea vya maradhi kama bakteria. kwa mfano mashambulizi ya UTI (Urinary Track Infection) iliyo sugu na ya mara kwa mara na kwa muda mrefu huweza kusaleta athari hii

3. Staili za maisha anazoishi mtu huweza kuwa ni sababu ya vijiwe hivi. kwa mfano kutokuwa na mazoeaya kunywa maji ya kutosheleza mara kwa mara. Hali hii huweza kutengeneza mazingira ya kemikali hizi kujirundika na kutengeneza vijiwe.

4. Pia inaweza kuwa mtu amerithi baadhi ya hali kutoka katika familia yake. Mtu anaweza kurithi hali za kiafya ambazo zinaweza kupelekea kutokea kwa vijiwe hivi.

NINI TUFANYE: VIPI TUTAZUIA AMA KUPUNGUZA TATIZO HILI:
1. kunywa maji mengii na ya kutosheleza mara kwa mara
2. Epuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi mara kwa mara
3. Hakikisha una uzito wa kawaida.
4. Punguza ulaji wa baadhi ya vyakula hasa vyenye protini na vyenye madini ya Calcium kwa wingi.

NI IPI TIBA YA TATIZO HILI?
Kwanza tambua kuwa tatizo hili linatibika wala hakuna tatizo kwenye hilo. Mgonjwa afike kituo cha afya anaweza kupewa dawa ama akapatiwa tiba kulingana na tatizo
lake.

Chanzo: https://bongoclass.com/magonjwa/figo.html
 
Back
Top Bottom