Matatizo ya kiafya.

Onguluo

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
406
Reaction score
116
Habari za leo wakuu, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya siku na masaa haya, Jina lake liimidiwe milele.
Jmn nmekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya Afya yangu kwa ujumla, awali nilikuwa nasumbuliwa na tatizo kushindwa kupumua vizuri hasa sehemu yenye hewa kidogo km Kwenye daladala au gari lenye AC kidogo, nilienda Hospitalini nifanyiwa check up,nikagundulika kuwa nina mafuta mengi Kwenye damu (cholesterol). Nilipewa dawa inayoitwa Atorin 20mg za kunywa mwezi mzima, nilipoanza kutumia hizo dawa baada ya siku 4 nikaanza kusikia isiyo ya kawaida mwilini, kwanza uchovu, kuwashwa koo, kichwa kuuma na misuli ya mwilini, viungo kulegea, mafua na koo kukauka, pia maumivu ya kifua na tumbo kuwaka moto hasa karibu na kifua.
Baada ya kuona dalili hizo, nilimfuata daktari nakumueleza lkn akaniambie kuwa ndivyo dawa zinavyofanya kazi, Charlie msingi ni kunywa maji mengi.
Niliendelea kutumia dawa hizo nikamaliza dose yote.
Shida ninayoipata sasa hivi ni ulimi kukauka na mdomo unauka sana utazani umeungua, maumivu ya koo, misuli ya shingo kukakamaa, pia napata maumivu ya kichwa na viungo vya mwili kulegea, yaani karibu kila sehemu mwili unauma.
Nimeenda kupima typhod,malaria na UTI zote hakuna kitu.
Sasa naomba Ushauri wako,nifanyeje ili nipone make nina mawazo sana,!!
Na Je, hizo dawa ndizo zimeniongezea matatizo hayo au ni maradhi mengine tofauti?? Naomba Ushauri wenu wakuu na wataalamu!!!!
 
Mkuu kwa viashiria hivyo...nenda tu hospitali ...hata nyengine uoneshe hivyo vyeti...
 
UKIMWI hutaki kupima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…