Matatizo ya kukatika Internet nchi nzima alaumiwe Waziri Nape kwa kuikataa StarLink

Matatizo ya kukatika Internet nchi nzima alaumiwe Waziri Nape kwa kuikataa StarLink

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Waziri wa Habari na Mawasiliano, ndugu Nape Nnauye ndiye anapaswa kulaumiwa kwa kutokuwa na internet ya uhakika nchini kwani waziri huyu aliikataa kampuni ya Mmarekani tajiri zaidi duniani iitwayo StarLink ambayo ina satellite zaidi ya 10,000 angani.

Kampuni hiyo iliyowasilisha maombi ya kutoa huduma zake nchini mwaka jana ilikataliwa kuwekeza nchini na ndugu Napelape.

Uwekezaji huo ungeiwezesha Tanzania kuwa na internet ya kisasa zaidi duniani isiyotegemea cables kama ilivyo sasa ambapo nyaya hizo zilizolazwa baharini huleta hitilafu ya mara kwa mara.

Inasemekana makampuni ya internet ya hapa nchini yameshinikiza kukataliwa kwa StarLink kwani kungeleta ushindani mkubwa wa kibiashara.

====
Pia soma:

Vigogo wengi wastaafu na walio madarakani ndio wenye hisa kubwa kwenye makampuni ya huduma za simu sasa wanaanzaje kukubali ushindani?

nani asiejua mungu wa dunia hi ya anguko ni shetani na anafanya maamuzi kwa manufaa yake mwenyewe katika kila taifa na nchi na vibalaka wake wengi ndio hawa viongozi wa siasa

Ndio maana akitokea kiongozi akasimama kwenye haki Hawezi kua na MAISHA atapigwa vita sana..!

Ukitaka kuamini hili Cheki njia inayotumika kuwapata hao viongozi Kama ina haki au hizo teuzi za viongozi Kama zinazingatia weledi, HEKIMA na maarifa katika field husika ambayo kiongozi anachaguliwa

Wana wa MUNGU wa kweli na wa pekee tuwe na subira ufalme wa Baba yetu wa haki na mtakatifu umekaribia Sana kuja kutawala
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano ndugu Nape Nnauye ndiye anapaswa kulaumiwa kwa kutokuwa na internet ya uhakika nchini kwani waziri huyu aliikataa kampuni ya Mmarekani tajiri zaidi duniani iitwayo StarLink ambayo ina satellite zaidi ya 10,000 angani.

Kampuni hiyo iliyowasilisha maombi ya kutoa huduma zake nchini mwaka jana ilikataliwa kuwekeza nchini na ndugu Napelape.

Uwekezaji huo ungeiwezesha Tanzania kuwa na internet ya kisasa zaidi duniani isiyotegemea cables kama ilivyo sasa ambapo nyaya hizo zilizolazwa baharini huleta hitilafu ya mara kwa mara.

Inasemekana makampuni ya internet ya hapa nchini yameshinikiza kukataliwa kwa StarLink kwani kungeleta ushindani mkubwa wa kibiashara.
Viongozi wengi wa Ccm ni slow learners. Sasa uta wasikia wakija na hoja za kutaka mbadala. Wakati walisha shauriwa zamani waka puuza
 
Vigogo wengi wastaafu na walio madarakani ndio wenye hisa kubwa kwenye makampuni ya huduma za simu sasa wanaanzaje kukubali ushindani?

nani asiejua mungu wa dunia hi ya anguko ni shetani na anafanya maamuzi kwa manufaa yake mwenyewe katika kila taifa na nchi na vibalaka wake wengi ndio hawa viongozi wa siasa

Ndio maana akitokea kiongozi akasimama kwenye haki Hawezi kua na MAISHA atapigwa vita sana..!

Ukitaka kuamini hili Cheki njia inayotumika kuwapata hao viongozi Kama ina haki au hizo teuzi za viongozi Kama zinazingatia weledi, HEKIMA na maarifa katika field husika ambayo kiongozi anachaguliwa

Wana wa MUNGU wa kweli na wa pekee tuwe na subira ufalme wa Baba yetu wa haki na mtakatifu umekaribia Sana kuja kutawala
Sasa tutazame cha kufanya, yaani wapumbavu wachache watutawale vichwa sababu ya matumbo yao kama kalabashi? [emoji848]

Hebu tujadili nini cha kufanya, tusijidharau raia tuna nafasi ya kufanya jambo.

Pengine wanatest mitambo ili uchaguzi ukifika waaanze kuzima internet sababu wamejua internet ndio inayotuunganisha sisi kama raia na sio serikali wala chama chao kilicho jaa watu takataka.

Hebu tutazame na kuzungumza namna bora ya kuweza kupambana na hawa mumiani.
 
Viongozi wengi wa Ccm ni slow learners. Sasa uta wasikia wakija na hoja za kutaka mbadala. Wakati walisha shauriwa zamani waka puuza
Ukiongezea ni wengi wao wanatamaa za fisi juu ya mali za umma zisizowahusu.

Hawa tuwawahi kabla hawajafa waende segerea wakaonje kifungo na kufilisiwa. Tupambane ahadi itimie. Kitakachotibu maumivu na vidonda vya hili taifa ni machozi ya hawa mafisadi wa taifa.
 
Vigogo wengi wastaafu na walio madarakani ndio wenye hisa kubwa kwenye makampuni ya huduma za simu sasa wanaanzaje kukubali ushindani?

nani asiejua mungu wa dunia hi ya anguko ni shetani na anafanya maamuzi kwa manufaa yake mwenyewe katika kila taifa na nchi na vibalaka wake wengi ndio hawa viongozi wa siasa

Ndio maana akitokea kiongozi akasimama kwenye haki Hawezi kua na MAISHA atapigwa vita sana..!

Ukitaka kuamini hili Cheki njia inayotumika kuwapata hao viongozi Kama ina haki au hizo teuzi za viongozi Kama zinazingatia weledi, HEKIMA na maarifa katika field husika ambayo kiongozi anachaguliwa

Wana wa MUNGU wa kweli na wa pekee tuwe na subira ufalme wa Baba yetu wa haki na mtakatifu umekaribia Sana kuja kutawala
Wanakataa kampuni kama hizi, halafu wanakubali DP WORD
 
CCM huwa hawajui kitu kinaitwa plan B...ndio maana hata wao wanajiita chama tawala
 
Sasa tutazame cha kufanya, yaani wapumbavu wachache watutawale vichwa sababu ya matumbo yao kama kalabashi? [emoji848]

Hebu tujadili nini cha kufanya, tusijidharau raia tuna nafasi ya kufanya jambo.

Pengine wanatest mitambo ili uchaguzi ukifika waaanze kuzima internet sababu wamejua internet ndio inayotuunganisha sisi kama raia na sio serikali wala chama chao kilicho jaa watu takataka.

Hebu tutazame na kuzungumza namna bora ya kuweza kupambana na hawa mumiani.
Mbona watu wanatumia zao star link kimya kimya,ukisubiri ccm ikufanyie kila kitu utakufa maskini, hiyo pay pal mpaka leo bila bila lakini watu wanapambana hivyo hivyo.. Yani hii serikali inafanya vijana tushindwe kuwa competent kwenye soko la ajira la dunia sasa hivi mtu anaweza kufanya kazi na na kampuni yoyote duniani akiwa nyumbani tuu cha muhimu internet ya uhakika,wanadhani kila graduate anatakiwa kuwa machinga au winga
 
Tatizoo ni mfumo wa chama cha tawala ni mbaya na usio haki na bahati mbaya chama kimeshakita mizizi

Ndio maana akitokea kiongozi akasimamia haki mfumo unamkataa na kumtupa nje kwa njia mbalimbali

Mfano kuna watu kila rais atakae ingia ni Lazima awateue kwenye baraza la mawaziri ukiwaacha nje hao utapigwa vita Sana

Cha kufanya either watu walio NDANI ya CCM wale vigogo wote waondoke waje watu wengine watakaobadili mfumo wa chama au chama kishindwe katika uchaguzi vitu ambavyo vyote haviwezekani kutokea
Sasa tutazame cha kufanya, yaani wapumbavu wachache watutawale vichwa sababu ya matumbo yao kama kalabashi? [emoji848]

Hebu tujadili nini cha kufanya, tusijidharau raia tuna nafasi ya kufanya jambo.

Pengine wanatest mitambo ili uchaguzi ukifika waaanze kuzima internet sababu wamejua internet ndio inayotuunganisha sisi kama raia na sio serikali wala chama chao kilicho jaa watu takataka.

Hebu tutazame na kuzungumza namna bora ya kuweza kupambana na hawa mumiani.
 
Ni aibu tunaenda siku ya tatu bado internet ni ya kusuasua.

TCRA kama mambo yamewashinda, ombeni msaada kwa wajuzi waje wawatatulie.
 
Nape angekubali starlink ije Tanzania angekosa 1.2b anazopewa na Miatandao ya simu kila mwezi . "Nape ana watoto wanasoma shule"
 
Unamaanisha hao star...ndio waliohujumu cables Baharini?
 
Hapana. Ilaumiwe ccm.

Maamuzi yote ya kisekta ktk wizara husika huanzia ni lazima yapate baraka za baraza la mawaziri wa serikali ya ccm.
 
“Nape, unawaogopa StarLink. Kwanini?”

February 2023, Michael Coudrey (30), Mwenyekiti na CEO Pharos Investment Group kutoka USA alimtaka C.E.O wa StarLink, Elon Musk kuhakikisha Starlink inapatika Afrika Mashariki hususani Tanzania ili watu wapate huduma ya intaneti yenye kasi zaidi ili kupata habari, kujifunza na kujenga kesho kubwa.

Bilionea, Elon Musk, mmiliki wa Starlink akamjibu Mike Coudrey kwamba “tunapenda pia kuwekeza Tanzania. Tunasubiri uthibitisho wa serikali”. Elon aliposema hivyo akajibiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akajibu kwamba Starlink wanatakiwa kujenga ofisi zao Tanzania.

Rais wa Kenya, William Ruto, September 2023 akiwa Kenya amewaalika Apple, Google, Intel, Nike, Levi kuwekeza Kenya kwa kujenga viwanda. William Ruto amefika Hawthorne, Los Angeles, Califonia, USA makao makuu ya Space X/Starlink kuwekeza na kujenga miundombinu yao Kenya ili kurahisha utoaji huduma.

STARLINK wameingia Rwanda, na Rwanda Space Agency (RSA) wametoa vibali vyote na kuwapa StarLink leseni, kazi imeanza. Mnyarwanda anayetaka kasi kwenye data, anahamia zake Starlink Wanyarwanda hadi vijijini huko wanapata ‘Internet’ yenye kasi.

Elon Musk, mmiliki wa kampuni binafsi ya roketi na vyombo vya anga, SpaceX, wanaoendesha STARLINK anasema wametuma maombi ya kuingia Tanzania, na kwamba wanasubiri kukubaliwa na kupewa vibali na wenye mamlaka (serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Mawasiliano).

NAPE Nnauye, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari anasema STARLINK hawajakamilisha baadhi ya nyaraka ambazo wao kama wizara ya Mawasiliano wanazihitaji katika maombi yao na anasisitiza LAZIMA wakamilishe nyaraka hizo ndiyo mazungumzo yaanze.

Nyaraka hizo ni pamoja na masharti ya kuweka (Starlink) ofisi zao Tanzania na kwamba kama mamlaka za mawasiliano zikihitaji kupata taarifa zao, wazipate kwa wahusika. Bado wizara ya Mawasiliano inaishi katika karne ya 13 wakati Ulimwengu upo karne ya 21.

Google wanazo ofisi Tanzania? WhatsApp? Twitter? Facebook? Instagram? Tik-Tok? Yahoo? Vipi, mamlaka za mawasiliano zikihitaji taarifa zao, wanazipata kwa njia gani? Ujanja-Ujanja tu wa waziri na wizara katika hili, na unakera. Dunia inakwenda kasi, waziri anajivuta.

Ofisi za Netflix zimejengwa wapi Tanzania? Tunafanya subscription zetu kila mwezi, vipi, siku wakishindwa kutoa huduma tutakwenda wizarani kulalamika? Hoja ya Waziri ni hoja ya kupuuzwa tu. Waziri anatumia huduma za Google & Gmail, Yahoo, ofisi zao zipo wapi Tanzania? Au wao hawachukii taarifa za wateja?

Tunafahamu, kwa urasimu wa biashara ya watoa huduma za data waliopo Tanzania, STARLINK wakiweka miguu katika ardhi ya Tanzania, hii itakuwa ni mwisho wa biashara ya ujanja-ujanja ya tiGo, Vodacom, Airtel, TTCL kwenye data. Biashara ambayo inawanyonya watumiaji na kuwalipa vigogo.

Wakati watanzania wanatumia internet yenye kasi ya 2G hadi leo katika maeneo mengi na sehemu nyingine hakuna kabisa Internet ni kama upo kaburini, bado serikali ya Tanzania inaweka kauzibe kwa STARLINK anayekuletea INTERNET yenye kasi kubwa kuliko iliyopo sasa kwa bei nafuu.

Upatikanaji wa Internet hufungua ulimwengu katika njia nyingi. Burudani, elimu, kuwezesha biashara za malipo mitandaoni na hata kuimarisha demokrasia. Ndio maana maendeleo katika kutoa ufikiaji wa mtandao kwa watu barani Afrika yanafaa kusherehekewa.

Afrika inatakiwa kuunganishwa kwa njia ya internet. Nchi za Afrika nyingi zina miundombinu Dunia ya kidijitali. Gharama kubwa kuwekeza kwenye fibre optics cables au milingoti ya simu (mobile phone masts) hususani katika maeneo ya vijijini. Tanzania inakabiliwa na changamoto hizo.

Umoja wa Mataifa una mkakati wa kufikia upatikanaji wa huduma kwa wote barani Afrika ifikapo 2030, lakini hili halitawezekana bila mbinu bunifu. Starlink sasa ni kati ya ubunifu huo. Hakuna bajeti ya kusimika nguzo, hakuna fibre optic cables. Ni mwendo wa mawimbi tu.

Sehemu kubwa ya huduma ya internet kwa sasa inatolewa kupitia simu za mkononi, wireless Internet (mawimbi yake yanatumwa na kusafiri kwa kutumia minara iliyosimikwa ardhini). Hii ina ufikiaji wa taratibu na kwa eneo dogo tofauti na matumizi ya satellite.

Starlink ni mfumo wa satelaiti unaolenga kusambaza mtandao wa Internet kimataifa. Mfumo huu unafaa kwa maeneo ya vijijini na yaliyotengwa kijiografia ambapo muunganisho wa intaneti si wa kutegemewa au haupo kabisa. Tanzania inayo maeneo mengi yaliyotengwa kijiografia.

Kufikia December 2022, STARLINK ina zaidi ya satellite ndogo 3,300 zilizozalishwa kwa wingi katika Low Earth Orbit (LEO) ambazo huwasiliana na ground transceivers maalum. Hawa ni watu ambao tunaweza kuwatumia hata baadae kwenye masuala ya kurusha satelaiti yetu, tukipata akili.

Badala ya kutumia teknolojia ya cable (cable technology), kama vile cable fibre optics kusambaza Internet data, mfumo wa satellite unatumia mawimbi ya radio (radio signals) kupitia utupu wa nafasi (vacuum of space).

Vituo vya ardhini (ground stations) hutoa taarifa za mawimbi kwa satellite katika njia ya Orbits, ambazo hurejesha data kwa watumiaji wa Starlink Duniani. Kila satellite ina uzito wa 573 pounds (259.908kg) umbo tambarare. Roketi moja ya SpaceX Falcon 9 inatosha hadi satellites 60.

Starlink sio mshindani pekee katika mbio za anga za juu, ingawa kuna washindani wachache, pamoja na OneWeb, HughesNet, Viasat na Amazon. HughesNet inatoa mawimbi kutoka maili 22,000 juu ya Dunia tangu mwaka 1996, lakini Starlink inafuata mbinu tofauti kidogo na hawa HughesNet.

Starlink inatoa data ya kasi ya juu isiyo na kikomo kupitia satelaiti ndogo zinazotoa hadi 200 (Mbps) za kasi ya mtandao. Utafiti wa Speedtest uliofanywa na Ookla, Starlink ilirekodi kasi ya upakuaji ya wastani ya kasi zaidi katika ¼ ya kwanza ya 2022 katika 160Mbps Lithuania.

Starlink pia ilitumia kasi ya 91Mbps nchini USA, 97Mbps nchini CANADA na 124Mbps nchini Australia, na nchini Mexico kasi ya upakuaji ilikuwa 105.91Mbps. Hii ni kasi mara mbili au zaidi ya kasi ya mitandao karibu yote ya Tanzania. (Mbps - Megabits per seconds).

Utafiti wa Speedtest uliofanywa na Ookla kwa watoa huduma za mitandao Tanzania unaeleza kasi ya Halotel ni 18.57mbps, kasi ya Vodacom ni 16.38mbps, kasi ya tiGo 14.23mbps, kasi ya Airtel 13.11mbps, kasi ya Zantel ni 6.55mbps. Kwanini tuwakimbie Starlink ambao wanakupa 124Mbps?

Sehemu inayoweza kuleta wasiwasi ni kwenye gharama. Starlink nchini Nigeria, hugharimu takriban N276,000 (US$599) mara moja kwa ajili ya vifaa na kufunga hivyo vifaa, kisha hutoza ada ya usajili ya kila mwezi ya takribani N198,000 (US$43) = Sh107,715. Lakini unapata kasi ya 500Mbps.

Vodacom Unlimited internet kwa mwezi (fixed monthly charges); 20mbps kwa mwezi ni Sh115,000. 30mbps kwa mwezi ni Sh120,000. 50mbps kwa mwezi ni Sh150,000. 100mbps ni Sh250,000. 200mbps ni Sh400,000. 350mbps ni 600,000.

Nani bora? Starlink anayekupa 500mbps kwa Sh107,715 mwezi au Vodacom anayekupa 350mbps kwa Sh600,000 mwezi? Unahitaji akili ya kawaida kufahamu; Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari anaweza kuwa mnufaika wa magenge ya Mobile Network Operators (MNOs) ndiyo sababu hawataki StarLink?

Serikali inatakiwa kutambua kwamba uwepo wa Starlink haukusudiwi kuchukua nafasi ya watoa huduma wa mitandao waliopo nchini. Lakini badala yake kusaidia na kuimarisha huduma zao kwa kutoa huduma katika maeneo ambayo miundombinu isiyokuwa na uwezo mkubwa inakosekana.

Pia Starlink kwa ubora wao, mtandao wao unaweza kutumika kama mbadala wa watoa huduma wengine endapo kutatokea hitilafu au kukatika kwa primary network. Kuna wakati kuna ‘faults’ za mitandao Tanzania, kama Starlink wapo, wanaokoa huduma bila kusubiri primary network kutengemaa.

Rwanda ilikuwa miongoni mwa nchi chache zilizopewa fursa ya kujaribu muunganisho wa Starlink barani Afrika. Katika majaribio yaliyofanywa katika maeneo tofauti ya nchi, kasi ya Starlink ilifikia hadi 150 Mbps na utulivu (latency) chini ya 20 hadi 40 milliseconds (ms).

Kenya ni nchi ya sita Afrika kutoa leseni kwa Starlink baada ya Nigeria, Mozambique, Rwanda, Mauritius na Sierra Leone. Tanzania tunaogopa nini? Tunawalinda nani? TTCL? Hawa ambao wameshindwa hata biashara ya kutengeneza ‘vocha’ zao wenyewe? Zungumzeni na SpaceX.

MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Duh

Kama Musk amekataliwa basi ni Uamuzi wa Baraza la Mawaziri na siyo Nape peke yake 🐼
 
Tanzania Tubadilike ili twende na kasi ya maendeleo,kujenga SGR ni hatua kwa wizara ya uchukuzi je Habari wanatupa nini wananchi kimaendeleo,hawa internt providers wa hapa ndani ni michosho, they look for superprofits ebu Nape sikiliza kilio cha wananchi tumpate STARLINK tuone difference. Tupunguze urasimu wa uwekezaji, we need communication transformation per 4Rs
 
Back
Top Bottom