Naomba msaada wenu wa ushauri au sememu nzuri ya kupata matibabu. Mimi nina tatizo la kuwashwa mguu wa kushoto mara kwa mara. Sehemu inayowasha ni chini ya goti ila juu ya kifudo cha mguu. Hamna kovu, upele wala nini, panawasha sana kuzunguka mguu, ila nikijikuna baada ya mda kwa ndani panabadilika rangi na kuleta uweusi kwa mbali. Nimejaribu kwenda pale Mikochi Hospital kumwona mtaalamu wa ngozi akanipima mzio ila sikua nao, akanipa dawa ya kupaka siku 14 haikuleta mafanikio. Siku zinavyozidi kwenda kuwasha kunazidi kwa hiyo nitashukuru sana kwa mwongozo wenu ili nitatue hili tatizo kabla halijawa kubwa zaidi