Matatizo Ya Magari na Mfumo/Automotive, Plant & Equipment

Matatizo Ya Magari na Mfumo/Automotive, Plant & Equipment

Styvo254

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
246
Reaction score
227
Hbr za leo wanaJF
Naomba mda wenu kidogo ili niwaeleze mambo mawili matatu hivi kuhusu hivi vyombo vya moto/machine/mitambo n.k. hulsusan matengenezo, marekebisho na matunzo.

Vifaa hivi ni muhimu sana kwetu kwa kua vinatumika katika nyanja na wakti wote maishani mwetu katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Hata asiyemiliki chombo chake binafsi anategemea kwa njia nyingi vyombo hivi kw kukodi, abiri na pia kuhimiza vitumike katika kuangalia maslahi yake na jamii - gari atembealo nalo Rais ni kwa sababu yako.

Mashine ni kiumbe kilichotengenezwa - artificial. Hakiwezi kujifanyia mambo kama kusafisha/kuzalisha(regenerate) vitu kama oili yake, mafuta breki na hata pia kuzalisha kawi toka kw vyakula/mali ghafi kama binadamu au viumbe asilia. Ni kwa sababu hizo basi inabidi mifumo ifanyiwe maboresho/matengenezo maalum kwa mda wake, mfn. oili lazima ibadilishwe baada ya umbali(gari) au mda(mifumo) uliopendekezwa na muunda chombo au aina ya oili; ni muhimu kukumbuka magari pia lazima yafate maagizo ya mda pale yanapokua yanatumika kwa safari ndogo ndogo na baada ya mda - ijapokua gari halijasafiri umbali uliopendekezwa, baada ya mwaka mmoja hivi ni lazima mafuta/oili yabadilishwe, hii ni kwa sababu yanazorota kwa ubora na hali.

Lingine la kuweka maanani ni kwamba chombo hakiwezi sisitiza - ila vya kisasa vina miundo mbinu ya kuashiria na kuzima pale maboresho yanapohitajika na yanapokiukwa. Hapa basi lazima mtumizi - awe dereva, opareta au mwangalizi awe na taarifa kukihusu chombo na matunzo yake, hii sio kusema lazima awe na uwezo wa kufanya maboresho yale au hata kuelewa kwa kina kinachoendelea ndani ya mashine.

Vyombo na mifumo hii upata hitilafu na shida tofauti katika matumizi yake. Hapa ndipo ufundi na utaalamu unapohitajika SIO TU kurekebisha bali pia kulielewa ili kukinga tatizo kutokea tena. Katika shughuli hii kuna mambo na mipangilio tofauti ambayo inafaa kuzingatiwa ili kufaulisha zoezi.

Kila mfumo, mashine au chombo kina ramani yake ya kiufundi - blueprint, kuna pia vielelezo vya kiufundi - workshop manuals, ambazo ufatiliwa na taarifa za kiufundi - technical service bulletins na hatimae kuna vielelezo vya matumizi na madumisho - operator and maintenance handbook. Kama vile anayemjua mwana ni mama, muunda mfumo ndiye anayeuelewa kwa kina, hata pale unapotumika hua anakagua na kuchunguza mapungufu ili kutoa zile taarifa za kiufundi na hata kufanya mabadiliko ili kuuboresha mfumo.

Kwa kweli si vyote vimeremetavyo ni dhahabu! Pia mifumo hua ina tofautiana. Kama wanavyosema wataalam, mambo uhojiwa kwa case by case basis au pia don't judge a book by its cover! Ni wajibu wa fundi kutafuta na kutumia taarifa, maagizo na vipuri vinavyofaa kw mfumo. Hapa ndipo unga uzidi maji!! Kuna sababu kadha wa kadha zibatilishazo mambo. Ya kwanza ni rasilmali - hii yaeza kua hela au mda; kila jambo uhitaji kujitolea flani kw hali, mali au zote pia. Taarifa na nakala zingine za kiufundi uuzwa kw bei ya juu hasa za mifumo ya kisasa, hii huadhiri gharama za kazi. Mda ni issue pia, mazoezi mengine uhitaji mda kweli - muulize aliebadili turbo ya Landrover Discovery 3 TDV7 au kuitoa engine, zoezi liliendelea vipi?!?!? Time is Money!! Vipuri maalum ni ghali pia, lakini lazima tujikumbushe kua kinachostahili ndicho kinachofaa na sio kinachofaa ndicho kinachostahili.

Kuna faida kibao za kufata maagizo/kanuni! Utulivu wa akili ni mmoja na ya muhimu kwangu kama fundi; nikifanya jambo inavyofaa, me hua sina wasiwasi kuhusu marudio au swala lolote kikazi au kiufundi labda kuwe na hitilafu isioonekana ni ikapita ukaguzi wa juu zoezini, na hili utokea kwa sababu zake pia. Lingine ni uimara wa marekebisho au maboresho; jambo likitekelezwa kwa njia iliyotambulika kua ya uhakika pale kuna usalama na imani. Warranty (tofauti na Guarantee) ni aina ya bima hivi atoayo muunda kifaa dhiidi ya kasoro au mapungufu ya kile kifaa kutokana na muundo, matengenezo au mauzo NA SIO matumizi au ufundi; mfn. kifaa cha dongo chuma(cast iron) chaweza kua na ufa kwa ndani na ikadhihirika kwenye matumizi na SIO kusababishwa ma matumizi yale.

Nikimalizia ningependa kuhimiza uadilifu kwa kuinua taaluma na utaalam. It takes a conscious effort to be a professional but nothing to be mediocre.
 
Back
Top Bottom