mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,773
- 2,183
Kila mwaka repoti za ukaguzi wa mahesabu ya serikali za mitaa zmekuwa zkionyesha mapungufu makubwa, yakiwemo kufanya manunuzi bila kushindanisha wazabuni, kufanya manunuzi ambayo hayakupitishwa na bodi za zabuni, kufanya manunuzi kutoka kwa wazabuni ambao hawakuidhinishwa, kufanya manunuzi na kupokea bila kukaguliwa na kamati za ukaguzi, kufanya manunuzi bila kuambatanisha nyaraka muhimu n.k. Thamani ya manunuzi haya ni mabilioni ya shilingi.
Nionavyo mimi mojawapo ya mapungufu ya usimamizi wa fedha katika halmashari zetu ni kuteua wakurugenzi kwa misingi ya kisiasa.
Uongozi wa serikali za mitaa (Local Government Administration) ni fani mahsusi katika utawala na inafundishwa katika baadhi ya vyuo vyetu.
Chuo Kikuu Mzumbe, kwa mfano kimekuwa kikifundisha fani kwa kipindi kipatacho miongo mitano. Watu waliopitia fani hii ndio wanatakiwa kuteuliwa kuwa wakurugenzi wa halmashauri za miji, majiji na manispaa.
Unapomteua mtu kuwa mkurugenzi ambaye sifa yake ni kada wa chama unakuwa mwanzo wa kupoteza mwelekeo. Tukiendelea na mtindo huu tutaendelea kuona madudu yanajirudia katika mahesabu ya serikali za mitaa mwaka hadi mwaka.
Muda umefika sasa wa kutambua fani ya uongozi wa serikali za mitaa na kuteua watu wenye sifa na kuachana na kuteus makada. Nawasilisha.