Miaka mitatu mbona mapema? Yatakuja kuisha yenyewe tu naturally unless kama ana kilema kabisa. Mtoto wa dada alikuwa na matege ya kutisha mpaka tuliogopa. Daktari hata hivyo akituhakikishia kuwa akifikisha miaka mi5 yatakuwa yamekwisha. Na kweli ikawa hivyo.
Kuna vile viatu wanavalishwaga ya kunyoosha mifupa pia
Heshima kwenu wakuu! Kuna dawa au aina ya chakula chochote kinachoweza kupoteza matege kwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 3?
Nina dada yangu wenye mtoto wa tatizo hilo. Maana nimesikia CCBRT wanaweza kuinyosha kwa njia ya upasuaji, lakini dada yangu anaigopa njia hiyo.
Mwenye kujua njia zaidi ya hiyo tafadhari.
Vinapatikana wapi?..