Binafsi matokeo ya mtoto wangu yana walakini hasa somo la HISABATI. Nitapenda kuona karatasi zake zilizosahihishwa. HISABATI wamempa maksi 50 kati ya 100. Kwa jinsi alivyo na alivyofanya Mtihani naamini kuwa alipata alama 100 katika HISABATI. Haingiii akilini kuwa eti alishindwa kuvuka maksi 50 katika HISABATI.