nyunyizia mafuta kidogo
Mafuta gani hayo?
Pole sana..tafuta mafuta ya mlonge (pure), kuna jamaa yetu alipata matatito kama hayo na fizi kutoa damu, akakutana na Doctor mmoja kutaka nairobi anatengeneza dawa za asili akampa hayo mafuta, yamemsaidia, unatakiwa kutumia dawa ya colgate na kunyunyizia mafuta kidogo na kuswaki kutwa mara tatu. Huyu Dr. huwa anakuja Dar anapatika nyumba ya sanaa Makumbusho. Jaribu kupita pale kumwulizia
pole sana
Pole,
Daktari wa hospitali gani? Tatizo lako inaelekea kuwa la fizi...waweza google..periodontal disease/periodontal conditions...na linasababishwa na bakteria waliopo kinywani. Tiba ni kumuona dentist atakae kufanyia uchunguzi na kukupa tiba ambapo mara nyingi ni kuondoa "calculus" ambayo huwa inakuwa imejengeka kati ya fizi na jino na vile vile kuangalia hali nzilma ya usafi wa kinywa chako kwani watu wana "susceptibility" zinazotofautiana...na vile vile kuna magonjwa na hali nyingine ziongezazo kiwango cha ugonjwa..kama vile uja uzito na kisukari....
Nina matatizo ya meno yananiuma sana, hayajatoboka ni mazima kabisa yanauma tu na wakati mwingine nasikia yanatingishika nimeshamuona daktari akaniangalia angalia hapo, akanishauri dawa za kupigia mswaki lakini kila mara tatizo linajirudia mwenye kujua naomba anisaidie, pia nimeshatumia dawa ya maji za kupigia mswaki za gnld
Pole sana, inaonekana tatizo lako ni la Fizi zaidi na tatizo hilo na mambo mengi lakini zaidi ni kutokana na Uchafu uliyokaa muda mrefu kwene kwnye meno hasa uchafu wenye vimengenya vya sukari, ambavyo hupenya mpaka kwenye fizi na kuanza kushambuali bones za kushikilia meno hivyo bones hizo kulegea na mara nyingi meno huanza kulegea.
Mara nyingi kama dalili zimeshafikia hatua ya meno kulegea ni vema ukapata matibabu ya kitaalamu kwani kuna dawa za kalsium na dawa ambazo zitaimarisha kwanza mifupa ya meno na ndipo waanze kusafisha na kuondoa uchafu uliyoganda.
Kunakliniki yameno ni nzuri sana kwa matatizo hayo ya meno , kama wewe ni mkazi wa dar wapo mtaa wa jamuhuri karibu na masumini au wapigie no hii 0753 077 076.
asante kuna dokta wa meno yuko pale moroco karibu na hospital ya dr, masawe ndo alinifanyi uchunguzi akanisafisha akasema hamna kitu nitumie sensodaine dawa ya meno, kususu usafi wa kinywa nazingatia hilo sana pia fizi zinaniuma, ila sina ujauzito wala kisukari.
kacheki pia na ngoma. Ina tabia ya kula mishipa ya meno
pole sana. Vile vile unaweza kusukutua na mwalovera unaukatakata vipande vidogodogo unaweka kwenye mji ya moto inakaa kama dakika tano halafu utumia kusukutua. Hii inasaidia