Matatizo ya Network Marketing Tanzania

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Even if Network Market works…., Do you or are you prepared to do the work….

Network Market imepata sifa mbaya na watu kuiogopa na wapo waliojiunga lakini hawafanikiwi baadhi ya sababu nilizoziona na kama zifuatavyo:-

Watu wengi Wanajiunga Kutajirika na sio Kutumia Products
Kumbuka kwamba bila kutumia bidhaa hakuna atakayepata pesa. Sasa kama kila mtu yeye anajishughulisha kwenye recruiting na sio utumiaji wa bidhaa wengi wanajikuta wana team za watu wengi lakini mzigo hauendi. Hence na pesa haionekani.

Ulaghai na Over Expectations
Watu wanavyosajiri watu wanakuwa waongo, hawaelezi ukweli kwamba hii ni shughuli ngumu, unahitaji kuwa a good salesperson, matokeo yake wengi wanajiunga lakini ugumu wa shughuli unawafanya kuishia njiani na kuchoka.
Pia ili mtu aweze kusajiri watu sometimes inabidi hata appearance yake ionekane kwamba kapata sana pesa, kwahio sometimes mtu akikwambia kwamba hili gari au hii nyumba imetoka kwenye hii biashara huenda ni muongo.

Gharama ya Bidhaa
Gharama ya product nyingi hazilingani na kipato cha wananchi wa Tanzania sasa kama products majority ya wananchi hawawezi kununua hapo utaona kwamba shughuli ni pevu.

Oversaturation
Unapoingia mwanzo ni kweli kwamba kuna pool kubwa ya kusajiri watu ila watu wengi wanavyozidi kuingia ndio shughuli inazidi kuwa ngumu (ukizingatia watu wengi wanaojiunga sio kutumia bidhaa bali ni kusajiri watu) hivyo mwisho wa siku kampuni ikijulikana sana na ugumu wa kusajiri / kupata mtu mpya inakuwa kubwa

USHAURI
Kama kweli unaweza kuuza (good salesperson) basi jiunge ila angalia sana yafuatayo kwenye Kampuni
  • Good Products (ambazo unajua watu wataweza kuzinunua na kuzipenda)
  • Ni vema ingia kwenye kampuni ambayo haijawa oversaturated (kuwahi ni vema)
  • Pia kwenye malipo ni vema kama kwenye paying structure kutakuwa na overspill (Spill Over Matrix) kwenye kusajiri watu. (yaani hata kama wewe usipopata mtu ila mtu wa juu yako awe na limit ya kupata watu, yaani akipata watu zaidi waangukie kwenye level ya pili, hivyo ni kwamba team itafanya kazi kama group na hata wewe usipopata watu juhudi za wenzako zitakusaidia.

Mwisho kabisa ukitaka raha zaidi anzisha kampuni yako na ifanye MLM hapo utapata sales people wa kutosha hence avoid promotion and other costs of selling
 
Keysersoze umeelezea vizuri, kwa upande wangu nitasema hayo yote yanatokea kwa sababu moja kubwa ukosefu wa elimu ya biashara kwa wafanyao biashara na wale wapya.

Watu wakijifunza misingi ya biashara na hata misingi ya Marketing na wakajifunza pia namna Network Marketing inavyofanywa kwa usahihi kutoka kwa wale waliofanikiwa (si lazima Tanzania, hata sehemu nyingine duniani). Basi watafurahia matunda yake. Tofauti ya hapo ni hayo uyasemayo.
 
Nashukuru kwa aliye posti hii topic nadhani kuna mambo yapo sawa lakini mengine sio sawa na hii naweza kusema inatokana na kukosa elimu ya biashara hii. Hii ni biashara mpya huku kwetu, Ulaya na marekani ilianza miaka ya 50 na 60 kwa hiyo unaweza kuona tofauti yake. Ukisoma historia ya biashara hii utaona huko ilikoanza ilipingwa sana mwanzoni, wengi walikuwa na mawazo yanoyojitokeza hapa lakini baada ya muda yalibadilika.

Kuna vitabu, mafunzo, makala, na vifaa vingi vinafundisha jinsi ya kufanya biasha hii na namna ya kuchagua kampuni ya kufanya nayo biashara ya mtandao.Tatizo kubwa kwetu ni kuwa wengi hatupendi kusoma vitabu na makala ili kujua biashara hii na mbinu zake. Ukweli ni kuwa pamoja na magumu ya biashara hii watabiri wa mifumo ya biashara dunia na tafiti zinasema kuwa ndiyo biashara ya karne ya 21(Soma kwa mtandao the business of the 21st century), na itatengeza mamilionea wengi duniani, mfano USA peke yake watu zaidi ya 3500 huwa mamilione kila mwaka na hapa Tanzania nimefanya utafiti hilo limeanza kutokea pamoja na magumu na changamoto zake.

Tatizo linguine la watu wengi nchi zetu ni kama alivyoandika mmoja hapo juu wengi hatukufindishwa elimu ya biashara (business education) mashuleni tuliotoka. wengi tuna ujuzi hatujui namna ya kuuza na hivyo hata ukiwa na bidhaa zako hatujui kuziuza pia. mimi nimekuwa nikifanya kazi na wajasiliamali wengi wa bara hili na TZ pia wengi hatujui kabisa masula ya kutafuta masoko na namna ya kuuza. watafiti pia wanasema the most succesfull people in this world are good salers hapa selling ina maana pana hata mawasiliano (communication) ya faida na kuileza bidhaa au ujuzi wako.

Changamoto nyingine ya biashara hii ni kuwa watu wengi tumezoea kusukumwa sukumwa au kusimamiwa ili mamabo yaende. hii biashara waliofanikiwa ni watu wachapakazi,wanaofanya kazi bila kusimamiwa, wabunifu, wanopenda kujifunza, wanaopenda mabadiliko na wanaopenda kubadilisha maisha yao (wenye ndoto-dream). Ushauri wangu kwa wanaoifanya na wanaotaka kufanya biashara hii ni kwamba wafanye tafiti, wasome vitabu na kuhuduria mafunzo ya namna ya kufanya biashara hii na washikamane na waliofanikiwa nao watafanikiwa na wasiogope kudhubutu.
 
Kweli mkuu usemayo, elimu / ufahamu kwa kila unachokifanya ni muhimu.., sasa jukumu la kuwaelewesha hao watu si wale wanaofanya kazi hii tayari ? Sasa badala ya watu kusema ukweli na ugumu wa kazi wanapowapa watu false hope kwanza ni rahisi tu na kila mtu anaweza kufanya (hata wale wasiopenda kuuza) huoni kwamba wanaongeza tatizo badala ya kutibu tatizo ? Sababu ni kwamba kinachotokea mamia ya watu wanajiunga na mamia ya watu wanaondoka kila siku.

Pili watu wanasahau kwamba kuna product / bidhaa ambayo inabidi kutumiwa kwahio kabla ya kurukia kupata watu ili wapate wengine ni bora kuhakikisha hao watu unaowapata ni wale watuamiaji wa product. Ni bora wakafahamu Product ndio inayoendesha biashara na Watu peke yake bila Product haina tofauti na Ponzi Scheme na watu wanafaidika kwa entrance /membership fee.
 
Mkuu Mr II

Asante kwa mchango wako katika kuelimishana ni wapi watu tunakosea / wanakosea..., ni vema tukaweka wazi makosa yapo wapi katika hii forum ili kesho keshokutwa watu tujifunze....

Kwahio kosa kubwa ulilosema ni kwamba watu hawasomi (na hio ni kweli ni nature ya watanzania) ni vigumu kuwabadilisha leo..., you can force a donkey to the river, but you cant force it to drink water..., Hapo mimi naona kama hili ndio lingekuwa ni kosa pekee, basi kosa sio la wananchi kutokusoma na kuifunza bali kwa wale wanaowasajili kutowafundisha na kuwaelekeza.., information sio lazima usome unaweza ukatengeneza CDs au short clips watu waone na kujifunza.

Mimi naona tatizo kubwa ni Gharama ya Bidhaa kwa maisha ya mtanzania na hapa sababu najua soko lipo..., (angalia tu waganga wa kienyeji wanavyoibuka kama uyoga, au dawa za asilia zinavyoibuka kila leo)kwahio sababu hizi kampuni nyingi zinauza suppliments ambazo mtu anaweza akazimeza kama peremende bila kuwa na madhara watu wangekuwa wanazimeza kama zingekuwa zinauzwa kwa price ya kueleweka..., wewe huwezi kumwambia mtu ajali afya yake kwa kununua kachupa kwa maelfu ya pesa wakati mdau hata hajui buku la kula mchana atalitoa wapi.., au ataona si bora anunue parachichi au ndizi apate vitamins as well as tumbo kujaa ?

Kwahio mkuu tatizo la kwanza kubwa saana ni gharama ya hivi vitu haviendani kabisa na uhalisia wa Mtanzania Unless kama hii ni biashara ya walengwa wanaojiweza.. na kama ni hivyo sababu hii ni biashara inayoendana na word of mouth (mtu kuwaambia watu wake wa karibu) huoni kwamba kwa mtu kusajiri wasiojiweza kununua hizo bidhaa ni makosa sababu hata marafiki zao wengi hawajiwezi kununua hizo bidhaa ?
 
Last edited by a moderator:
Mimi nlikataa kuingia kwenye Forever mana nlitaka kupata faida lakin nkawza mbona kama faida haipo na kam ipo itachelewa . Nlikuwa na lak 6 nkanunua laptop ambyo ndo nafanyia kazi zangu mpak leo badala ya kupewa cheo cha assistant supervisor ambayo ckuon faida yake ." if you fail to plan then your planning to fail"
 
asante kwa ushauri wako ndugu ningeomba uniorodheshee hapa hivyo vitabu vya networking marketing ili nami nisome na nianze kuthubutu kufanya biashara za mtandaoni

 
entrance /membership fee ni ada ya aina gani kwa mm ninayetaka kufanya biashara ya networking ?
nifahamishe ili nipate kufahamu vyema au waweza kunitumi tips za somo hilo?

 
entrance /membership fee ni ada ya aina gani kwa mm ninayetaka kufanya biashara ya networking ?
nifahamishe ili nipate kufahamu vyema au waweza kunitumi tips za somo hilo?

Biashara hizi nyingi mfano (GNLD, Tianshi, Forever n.k.) ili uweze kuwa member inabidi utoe membership fee (yaani pesa ya wewe kuwa member) au wengine wanaiita Starter Pack, ambayo ni information jinsi ya kufanya biashara na products za kuanzia.

Sasa point yangu hapo juu kama watu wengi wanajiunga kwa sababu ya kutengeneza pesa peke yake na sio kutumia products unakuta kwamba kinachotokea pesa inayopatikana kwa mwezi inakuwa intoka sana kwenye hizi membership fee, ingawa ingekuwa bora kama watu wanatumia sana products pesa nyingi zingekuwa zinapatika kila mwezi kutoka kwa watu wa chini yako, na sio kutegemea new members waje ili ipatikane membership fee ili mgawane.

Na kama nilivyosema Network Marketing (Biashara ya Mtandao) bila product haina tofauti na Ponzi Scheme / Pyramid Scheme / DESI
 
Naona thread hii inafurahisha sana. Asante sana KeyserSoze kwa kuanzisha hii mada.

Kutokana na takwimu za Direct Selling Association (DSA), inaonesha kuwa Zaidi ya 90% ya wanaofanya biashara ya mtandao wanatengeneza chini ya $10 kwa wiki katika hiyo biashara.

Sababu kubwa ya watu wengi kutofanikiwa katika biashara hii ni:
  1. Get Rich Quick Syndrome: Kutegemea kutajirika kwa haraka bila kufanya kazi (inawavutia watu wa kina desi type)
  2. Kutojuwa wanatakiwa kufanya nini ili waweze kufanikiwa. Na wasipoona matunda kwa muda mfupi hukata tamaa.
  3. Kutotaka kukuza ujuzi wa kuweza kujenga biashara yao.
  4. Na sababu nyenginezo nyingi.

Faida ya Network Marketing:
Ingawa biashara hii ina asilimia ya watu wachache wanaopata mafanikio makubwa, watafiti wa finance (kama Robert Kiyosaki na wenzake) wanashauri watu kujaribu hii biashara kwani utakuwa na matumaini ya 60% ya kuwa Millionaire kwenye biashara ya mtandao kuliko kwenye ajira kutokana kwa sababu zifuatazo:
  1. Hakuna limit ya kiasi gani unayoweza kutengeneza katika hii biashara.
  2. Unapata kukuza taaluma yako ya mauzo (sales techniques)
  3. Unapata kukuza taaluma yako ya kuongoza watu (leadership skills, ambayo ni taaluma muhimu katika ujasiriamali)

Hasara Ya Network Marketing:
  1. Mafanikio yako ya kipato chako yataongezeka endapo mtandao wako utakuwa mkubwa. Huwezi kutengeneza pesa nyingi sana kwa kufanya mauzo wewe kama wewe. Hata kama wewe ni mzuri zana wa kufanya mauzo, kama huna network nzuri ya watu wenye kipaji kama chako, hutotengeneza pesa nzuri sana (labda kampuni iwe inalipa 70% na zaidi ya mauzo ya kila bidhaa kama kamisheni za awali (direct sales commision) [Makampuni machache sana yanafanya hivyo].

Network Marketing Inamfaa mtu wa namna gani?
Network Marketing inamfaa mtu mwenye moyo wa chui (a.k.a hustlers). No cry babies allowed. Kama wewe ni mwoga wa ku fight kujenga ndoto zako kwa moyo thabiti, hii biashara sio yako. Rudi kwenye ajira. Utapoteza muda tu hapa. Vile vile elewa kuwa Network Marketing ni profession kama udaktari, uhandisi etc. Inabidi uwe na nia ya kufanya biashara hii kwa taaluma ya hali ya juu. Hii sio biashara ya kutafuta watu kama watu wengi wanavyofikiria. Tembelea networkmarketingpro.com kujenga taaluma ya kufanya hii biashara.

Jinsi gani ya kuchagua biashara nzuri ya Network Marketing: Soma Hapa

Jinsi gani ya kujenga biashara hii kwa mazingira ya Tanzania: Soma hapa

Jinsi gani ya kujenga biashara hii kwa kupitia mtandao (kuwavutia watu kwako badala ya wewe kuwafukuzia): Tazama hii video

Vitabu muhimu vya kusoma:
  1. Think And Grow Rich (Utaelewa sifa 13 matajiri wote wanayo)
  2. Rich Dad Poor (Upate kujua tofauti kubwa ya maskini na matajiri)
  3. Business School (jinsi gani unaweza kujifunza taaluma biashara kupitia Network Marketing)
  4. Business of the 21st Century
  5. My first year in Network Marketing (jinsi gani ya kufanikiwa kujenga biashara ya Network Marketing katika Mwaka wa mwanzo)
  6. Psychology of Network Marketing
  7. How to win friends and influence people (hapa utajifunza vizuri jinsi gani ya kufanya mauzo. Powerful Sales techniques)
  8. Magnetic Sponsoring (Hiki kitabu kitakufundisha some Ninja Techniques za kuwafanya watu wakung'ang'ania kujiunga katika biashara yako bila ya wewe kuwafata. Best Network Marketing book I've ever read)

Natumai mmenufaika. Kama mna swali lolote mnaweza kuuliza hapa. Kwa information zaidi kuhusu jinsi ya kujenga biashara kutoka nyumbani kwako unaweza kuenda kwenye blog yangu Earn Money From Home — Earn Money From Home Guide For Beginners.

God Bless you,
Dr. Said
 
Dr. Said

Ni kweli umeeleza vizuri na kuwapa watu nyenzo za kuweza kunuifa pamoja na kuweka vitabu vinavyoweza kusaidia watu hata kama sio kwenye hii biashara na pia kuwapa motivation.., ila nadhani utakubaliana na mimi bado issue ya gharama ya hizi bidhaa ni kikwazo kikubwa..., sababu hizi suppliments kwa wabongo wingi wa waganga inaonyesha kwamba wateja wapo na watu wanajali afya, tatizo its just affordability.

Alafu issue nyingine ni kwamba wajanja hata huko ulaya mtu akishatengeneza downline yake anatumia hiyo fursa na yeye kutengeneza products zake, mfano info-products, vitabu, cds as well as kufanya seminars na hizi hazitoi bure anakuwa anaziuza, hence anatumia downline yake kujiongezea kipato sio kutegemea tu kampuni husika kutoa commissions. Kwahio people never stop working.

Pia nadhani utakubaliana na mimi kwenye hizi MLM Spill Over Matrix ni bora kuliko matrix nyingine sababu watu wanafanya kazi kama team na kusaidiana hata wale wavivu wanapata faida ya wachapa kazi...., ingawa wale ambao matrix zao hazipo hivi watakwambia hii matrix ni mbaya sababu wavivu wanafaidika kwa kazi ya wachapa kazi.
 
Last edited by a moderator:

Kuhusu gharama za bidhaa ni kitu ambacho ni subjective (kila mmoja ana muono wake). Kuna msemo maarufu wa mwanafalsafa na mfanyabiashara maarufu Jim Rohn, anasema "Don't say it's expensive. Say I can't afford it"

Ingawa mara nyingi tunahisi tunanunua bidhaa, lakini ukweli kitu tunachokinunua ni faida (value) inayopatikana kutokana na bidhaa hiyo. Kama mimi ningekuwa nina uzito wa kilo 200 na nikaamua kununua vidonge vya kupunguza uzito. Na vidonge hivyo vikafanya niweze kupunguza kilo 50 ndani ya mwezi, hata kama ile bidhaa ingekuwa inauzwa 300,000/- nisingesema ni ghali kutokana na faida itokanayo na hivyo vidonge.

Ila kama faida hainokeni, bidhaa ningeiona kuwa haistahili kuuzwa kwa bei hiyo. Na katika biashara ya Mtandao (Network Marketing), wanachama wengi kwa bahati mbaya wanashindwa kueleza faida za zile bidhaa (na wengine hata kutia chumvi) kuwafanya watu wengine wasione kuwa watafaidika na wengi wao wanaojiunga wanafanya hivyo kwa ajili ya biashara tu bila kujali kama bidhaa itawanufaisha au la.

Sisemi kuwa bidhaa za makampuni yote ya Network Marketing ni nzuri na thamani ya bidhaa zake ziko sawa, ila kwa makampuni mengi, bidhaa za Network Marketing zina quality nzuri zaidi kuliko bidhaa zinazouzwa kwenye makampuni ya kawaida. Kuna DVD ya Brilliant Compensation inaelezea zaidi hii concept.

Kuhusu viongozi kutengeza information products kuwasaidia downlines wake kufanikiwa haina tofauti na mwalimu mzoefu kuanzisha tution nje ya saa zake za kazi. Kama yale mafunzo yatazaa matunda kwa wanafunzi wale, basi ni bora afanye hivyo kwani wengi unaowaona waliotengeneza mamillioni katika hii biashara ni aidha wamenunua vitabu, wameshiriki katika semina nchi tofauti duniani au wanasikiliza trainings zao kwa njia ya sauti (audio).

Kuhusu compensation system nakubaliana na wewe kabisa kuwa sio system zote zina faida sawa. System kama binary system inawapa chance ya watu kupata spill over na system nyengine haziwapi.

Ila kama mtu anaingia katika hii biashara kutegemea atapata watu kutoka kwa upline (sponsor) wake, ajue kuwa hatofanikiwa. Sijaona mtu hata mmoja ambaye ni mvivu akawa anatengeza pesa nzuri katika biashara hii.

I hope nime clarify some of the issues.

Dr. Said
 

Kaka gharama ni gharama tu, mtu unaangalia na kipato cha watu husika katika nchi husika na buying power ya watu.., ndio maana hata nikikupa mfano wa Kampuni kama Epson za Printer huwa wanatoa matoleo kulingana na nchi husika, wakitoa kwa Africa wanaweza wakaipa mashine jina tofauti ingawa ipo sawa na mashine ya nchi nyingine lakini bei ya huku inakuwa nafuu kulingana na buying power ya watu.

Sasa kwa Kampuni zinazotoa kwamba ni Health and Wealth..., alafu unajua kabisa mtu hata mkate wake wa siku ni kashehe inakuwa tabu kwa yule mtu kutumia.., alafu hizi suppliments nyingine na za kula kama chakula sio unakula kama dawa (its an everyday thing) Labda ungeniambia njia bora kama baadhi ya hizi kampuni wameshatengeneza pesa za kutosha wanaweza wakaweka baadhi ya viwanda vyao nchini (kukuza ajira as well as kupunguza cost ya importation), lakini kinachofanyika sasa is like Selling Ice to Eskimos.., kuna mtu unajua kabisa hizi suppliments zitamsaidia ila kumwambia atoe 95% ya kipato chake ili kuongeza virutubisho unaona kabisa haumsaidii bali unamuangamiza.



Point hii haikuwa kwamba nasema wanachofanya ni kibaya..., bali ni katika kuelezea faida ya stream ya downlines.., kuna watu kama kina Big Al.., huyu ni mmarekani mmoja kwa kutumia network marketing ameweza kujipatia kipato na kuongeza faida kwa kuuza information kuliko hata faida anayopata kwenye commission za downlines wake katika utumiaji wa bidhaa za Kampuni au anavyoitwa kutoa semina za jinsi alivyofanikiwa n.k.

Hii point nimeitoa kama opportunity kwa watu ambao tayari wana mtandao, kwamba watumie mtandao huo kujinufaisha zaidi kwa kuuza kile wanachokielewa kuliko kusubiri commissions peke yake.
 

Ni kweli kuwa watu wengine watashindwa kununua hizo bidhaa. Lakini haimanishi kuwa hizo bidhaa ni 'expensive'. Kuna tofauti kubwa kati ya kitu kuwa ghali na kutokuwa na uwezo nacho. Nanukuu tena msemo wa Jim Rohn, "don't say it's expensive, say I can't afford it."

Kama mtu uwezo wake ni baisikeli hatakiwi kulalamika kuwa gari ni ghali. Ughali wa kitu unatokana na faida ya kile kitu ukilinganisha na kiasi ulichokitoa.

Ikisha kitu chengine cha kuzingatia ni kuwa, "je unataka kuwa mnunuzi tu au unataka kufanya biashara?".
Kama una nia ya kufanya biashara, ukizingatia mtaji wa kufanya biashara ya Network Marketing ni mdogo sana (kupita kiasi) ukifananisha na biashara yoyote ya kawaida. Hata biashara ya kiosk itakugharimu hela nyingi zaidi (kwa makampuni mengi ya Network Marketing) na potential ya faida yake ni ndogo sana ukifananisha na biashara ya Network Marketing.

Mimi nilivyoanza biashara hii ya mtandao nilikuwa mwanafunzi. Nilikuwa nimechacha, sina hela. Hohehahe. Badala ya kulalamika kuwa kianzio ni kikubwa nilikuwa sana naangali ROI (return on investment). Nilivyoina kuwa kurudisha pesa inawezekana, nilikopa hela nikaanza bila ya kusita. Baada ya miezi michache nikawa nimerudisha mtaji wangu na mpaka leo nafanya hii biashara bila matatizo yoyote.

Tukija kwenye uweza wa watu kushiriki katika biashara ya mtandao lazima tuelewe kuwa kila kampuna inakuwa inalenga watu wa kundi maalum (Class ya chini, kati na kati na upper class) ingawa makampuni mengi sana (zaidi ya 80%) inalenga middle class. Kuna makampuni yenye vianzio vya $25 na makampuni yenye vianzio vya $20,000. Sasa itategemea wewe upo wapi na ungependa kujenga biashara yako kwa kulenga kundi lipi?

Kwa upande wa faida ya kibiashara, makampuni yanayouzi products ghali (High Ticket Direct Selling Companies), zinaingiza faida kubwa na uhakika wa kuingiza faida ni mkubwa zaidi kuliko makampuni yanayo promote promote product za bei ya chini.

Kuna misconception kubwa ya watu wengi kuwa biashara nzuri ni ile ambayo utapata kuwauzia watu wengi.

Imeonakana kuwa ni rahisi zaidi kumpata mnunuzi 1 atakayenunua bidhaa itakayokuingizia $5000 (high ticket sales) kuliko wanunuzi 200 ambao watanunua bidhaa ya $25. Ni rahisi zaidi kumpata huyo mnunuzi 1 kuliko 200.(unless kama una sales and marketing strategies za bakhressa).

Sababu kubwa kwanini makampuni mengi yanalenga middle class ni kwa kuwa class ya kati ndio wameonekana ni wachapa kazi kuliko class ya chini na hata mara nyengine ya juu.

Na hao wanaotozwa 95% ya kipato kufanya biashara hii wanamiliki magari? How come waweze kumiliki magari na wasiweze kuwekeze katika biashara?

Hayo ni maoni yangu. I hope it's clear.

Thanks for the nice discussion KeyserSoze

Dr. Said
 
Kuna tofauti ya mimi kununua Ferrari yangu binafsi na mimi kufungua duka la kuuza Ferrari katika nchi ambayo matajiri ni watu wa kuhesabika, au kufungua duka la high end products Kariakoo badala ya kwenda Mlimani City. Kumbuka hapa siongelei kwamba mimi taweza au wewe uliweza, bali katika biashara hii inayotegemea leverage na nguvu za downlines kufanya kazi ana kwa ana inafikia wakati ambapo pool ya watu (wanunuzi) inabidi iwe kubwa sasa ndio hapo majority ya watu mitaani they can't afford the prices

Investment ya mtu its not only monetary, hata mtu investment ya nguvu zake nayo ni investment tosha.., sasa kuna watu anaangaika kwa udi na uvumba hadi kuwatolea membership fee watu ili nao wajiunge, lakini changamoto zinazowakuta watu wa chini, ambao wengi company yao ni watu wa chini wanajikuta wanakata tamaa sababu kazi yao inakuwa ngumu.

Birds of a feather flock together, inawezekana kabisa wewe majority ya watu waliokuzunguka wakawa kwao hii pesa sio tatizo ila your 4th level ikawa kwao ni kazi kupata watu kama hao, and as the business becomes saturated hata ukitamka jina tu watu wanakuwa wameshatambua hii fursa (recruitment becomes harder and harder).., Na sababu kubwa watu wengi wanaingia kufanya biashara na sio kutumia bidhaa.., angalau bidhaa zingekuwa affordable kwa kila mwananchi (au majority) basi hili lisingekuwa tatizo kubwa, sababu hata ungekuwa na downlines watano tu ila wanatumia bidhaa za kumwaga its better kuliko downlines mia mbili waliokaa na kuangaliana.

Mkuu alafu mimi siongelei sana membership fees au investment fees..., bali naongelea wateja, people we sell products to, je majority of them tena wengi wagonjwa na wanaziitaji, wanaweza waka-afford ?, au ni a chosen few ? and if that's the case unakuta salespeople ni wengi kuliko hata wateja.

Again siongelei membership fee kwa sana, bali kile kinachouzwa.., mfano kama Kikombe cha Babu kingekuwa bado kina-hit kama kipindi kile alafu akasema hata kujiunga mtu utoe milioni mbili, ingekuwa ina-make a lot of sense sababu tunajua fika demand ya kile kikombe and with no time ile pesa itarudi, hata kama 50% ya watanzania wote wangekuwa wanauza hiki kikombe bado pool ya wanunuzi ingekuwa ya kutosha.

Kwa upande wa faida ya kibiashara, makampuni yanayouzi products ghali (High Ticket Direct Selling Companies), zinaingiza faida kubwa na uhakika wa kuingiza faida ni mkubwa zaidi kuliko makampuni yanayo promote promote product za bei ya chini.
Ndio pale pale nikasema kama nauza Ferrari peke yangu Tanzania huenda ikawa biashara nzuri sababu hata wale matajiri kumi wakinunua tu huenda ikawa ni faida tosha kwa mwaka mzima, ila kama tayari kuna watu wanne wanauza hizo Ferrari alafu na mimi nikawa watano nadhani utaona competition iliyopo..., It is Better to Sale a Lot to a Few People than to Sell Less to a Lot of People, Huo ndio ukweli lakini kwenye hii biashara ya Network people are also a product, kwahio ni lazima uangalie hio product yako (watu/salespeople) je kazi yao ni ngumu au rahisi kiasi gani. Na kwenye nchi ya wengi wenye kipato cha chini utaona kwamba hii ni challenge.


Mfano wako kwenye hii case ni very misleading.., moja kwanza lazima ufahamu kwamba kwenye hizi products nyingi commission inayopatikana kwenye every sale of every product sio nyingi kivile, mbili utaona kwamba Network inavyokuwa saturated hence competition inaongezeka na ugumu wa kumpata yule mteja mmoja inavyozidi kuwa ngumu. Tatu angalia culture ya Mtanzania ni price conscious kwahio anything ikishakuwa na bei kubwa inakuwa tatizo. Nne hapa tunaongelea product ya mtu kutumia continuously kila mwezi (kitu consumable) which means mtu anayekinunua sio mara moja kwa mwezi bali ni mara kwa mara.

Alafu kumbuka hapa your major product is a person who needs to find a person who needs to find a person ili nyote mfanye kazi ya kutafuta watu wa kutafuta watu huku wanatumia bidhaa..., sasa kama bidhaa kwa majority ya watu hainunuliki faida itapatikana kwa wachache na wengi watakata tamaa.


Naam sasa nadhani nimepata mzizi wa kwanini mimi na wewe hatujaelewana..., mimi siongelei membership fee peke yake..., naongelea bei ya bidhaa / products za kampuni husika. Sababu this is the heart of the company, Ndio huenda 10% ya wanaojiunga wanaweza kununua bidhaa bila shida.., ila katika kutafuta watu ili watafute watu itafika wakati itabidi kuingia kwenye pool la watu wa kawaida / watu wa mitaani. Na mwisho wa siku hapa using products must go hand in hand with finding people, sababu hata watu wanaotafutwa ni ili mwisho wa siku wanunue product sio tu ili watafute watu.., sasa kama majority ya watu mtaani hawawezi kununua hizo bidhaa huoni kwamba kuna flaw kwenye system ? Unakuta watu walioingia mwanzo ni wanafaidika kwa kupata watu wanaochelewa kazi yao ya kupata watu inakuwa ngumu na hata wale wachache wanaowapata hata kutumia products hawatumii sababu ya gharama
 
Wow! This is getting more interesting. 😉

Kutokana na majibu yako ya mwisho, napata hisia kuwa
  1. Focus yako ipo katika makampuni ya wellness (kama forever living, tianchi, GNLD, Oriflame na wengineo) kampuni ambazo unanunua wholesale na unauza retail. na unatafuta wateja na watu wa kuwa recruit kwenye biashara. Na hujazingatia makampuni yenye mfumo tofauti.
  2. Vile vile unaongelea makampuni yanayohitaji wewe kuuza products zenye volume kubwa kwenye market na kuhitaji kujenga network kubwa ili ufanikiwe.
  3. Una assumption kuwa this is a ZERO SUM game kuwa watu wengi wakijiunga kwenye market itakuwa saturated na itakuwa ngumu watu kujiunga.
  4. Nahisi kuwa hujua kuwa kuna makampuni ya Network Marketing (direct sales) wanaolipa commision kubwa (zaidi ya 70%) kwa wanachama wake kwa kila mauzo ya bidha zao.

Elewe kuwa
  1. Makampuni yapo aina nyingi na sio yote yanayofata mfumo huo wa kununua na kuuza na kutafuta wateja. Hata hivyo, bidhaa zao zina market segment fulani na wapo watu wanaopenda hizo products, wanaonufaika nazo na wanazinunua kila mwezi, japokuwa sio wote watafanya hivyo (but the same case is for all products in every industry). 20% ya wananuzi watanunua 80% ya bidhaa. Hiyo ni law ya economics (Pareto's principle) ambayo hatuwezi kuiepuka. Wanachama wa Network Marketing wanatakiwa kujifunza skills za ku target hao 20% na sio 80%. Marketing is all about targeting.
  2. Kuna makampuni yanayofuata mifumo tofauti. Mfuma ambao hata kwa Network ya watu kumi unaweza kuingiza zaidi ya $1000 kila mwezi. Huhitaji kujenga Network kubwa kama makampuni mengi.
  3. Tukija kwenye issue ya saturation, it's usually an illusion. Kwenye karatasi saturation inaonekana inaweza kutokea. Lakini in reality sijaona kampuni ambayo imefikia saturation. Ingekuwepo basi Amway (kampuni ya 1959) ingekuwa ishakuwa saturated. Biashara zote zinafata law of demand and supply. As long as hizo product zitakuwa kwenye demand watu watanunua tu hata miaka 100 zijasho.
  4. Zipo kampuni ambazo wanalipa commission kubwa mwanzoni (hata zaidi ya 70% per sale) ili kuwa motivate watu waone pesa nyingi mapema na wa maintain business yao. Kwa wanaochapa kazi vizuri, inakuwa inawasaidia kupata kipato kizuri mapema na ku maintain network yake.

Hope that's clear. 🙂
 
  1. Ofcourse Mkuu najua kwamba MLM ni mfumo na sio bidhaa ya kampuni inayouzwa.., ila kumbuka hapa naongelea Tanzania na kampuni nyingi zinazokuja hapa ni za wellness na home products kulinganisha na soko (watanzania) to me these are perfect products..., ingawa chochote kile kinaweza kuuzwa kwa mfumo huu, pia kitu kizuri cha kuuzwa kwa mfumo huu ni recurring products/consumables ili ukimpata mteja leo atakuja mara kwa mara kununua bidhaa. Kwahio hata kama vitu kama voucher za simu watu wanaonunua mara kwa mara pia ni perfect kutumika
Ofcourse it goes without saying lets say mfano wa Forever au GNLD ilipoingia Tanzania, mwanzoni watu walikuwa hawatambui ni nini even recruitment was easier as the time goes more and more people join recruitment becomes harder na watu inabidi waende mpaka vijijini na ndani ndani kabisa kupata watu zaidi. Now don't get me wrong ili sio tatizo iwapo product zitakuwa zinamove kwa wingi.., ila utakuta kwamba sababu ya prices kuwa juu products zinamove slower due to the fact that the products can only be afforded by a certain class of people. Therefore even if the commission was 80% or 95% kama products ni za wachache (or few can buy) obviously ni wachache watakaofaidika. Pia am not saying all the MLM companies products zao ni expensive (nimeongelea kutokana na kipato cha mtanzania) sababu America, UK na hata South kuna kampuni ya Avon ambayo products zake ni very cheap even comparing with retail shops na quality yake ipo juu vilevile, and what is expensive for Tanzanians Citizens might be very cheap for an American market.


  1. Ofcourse sio kila mtu ananunua kila kitu.., ila kampuni ya MLM inapokuwa na a Big team of Sales Representatives lazima ina-focus kwenye products ambazo ni za mass consumption, yaani kila mtu au watu wengi wanahitaji au wanaweza kutumia, vitu kama vyakula, home products, health products n.k. kama product yako ni for a chosen few basi MLM sio njia ya kuuzia labda tafuta affiliates au watu wakuuzie uwape commissions. Lakini kama ni MLM ambapo the goal is to have a team of sellers, then it makes sense kwamba even the buyers wawe ni wengi na sio chosen few, unless otherwise watu tutakuwa tunagongana kugombania wateja (the competition becomes stiff..., and this is all I meant about saturation)

    Kuna makampuni yanayofuata mifumo tofauti. Mfuma ambao hata kwa Network ya watu kumi unaweza kuingiza zaidi ya $1000 kila mwezi. Huhitaji kujenga Network kubwa kama makampuni mengi.
    Ofcourse inategemea na buying power ya watu, alafu unaongelea hao watu kumi ambao wewe umewapata ila practically wale kumi watakaowapata kumi watakaowapata kumi baada ya muda kupatikana hao kumi inakuwa ngumu.., ila hili sio tatizo kama products zinauzija sana na ku-move kwa wingi.., ila kama haziuziki (kutokana na bei kubwa kwa available customers) kupata hizo pesa kunakuwa easier said than done
    Ofcourse Amway ipo mpaka leo na baada ya conquering America imekwenda mpaka China na nchi nyingi na Forever and GNLD zitaendelea kuwepo maisha.., that's not a dispute..., Saturation yangu ni kwamba within a given area (kumbuka hapa tunaongelea recruitment) baada ya muda recruitment becames harder as more and more people join hio ndio ninayomaanisha ya saturation, na hapo umeongelea suala zuri la demand.., ndio maana nikasema demand sio kubwa sababu ya bei (ni wachache ambao wana-afford the given products) sio kwamba hawaitaji/hawapendi products hizo. Hata hivyo kuna kipindi kilifika Amway ikawa saturated America ndio maana wakaanza ku-move kwenye nchi na sehemu nyingine. Ili kupata more sales representatives.

Kwa ufupi ni kwamba yaani ubishi wangu mimi na wewe ni kwenye Point kwamba Suala la Bei ya Bidhaa kuwa kubwa kuliko uwezo wa wananchi wengi ni kikwazo kikubwa sana kwa hizi kampuni hapa Tanzania...., Hapo Tuuuu
 
Kwa ufupi ni kwamba yaani ubishi wangu mimi na wewe ni kwenye Point kwamba Suala la Bei ya Bidhaa kuwa kubwa kuliko uwezo wa wananchi wengi ni kikwazo kikubwa sana kwa hizi kampuni hapa Tanzania...., Hapo Tuuuu​

Inawezekana upo sahihi sikupingi. Yapo makampuni mengine zenye products ambazo ni cheap kuliko zinazouzwa kwenye soko. Ila uelewe vile vile kuwa cheap products = low commission = makes growing the business even difficult.

Tutaingia kwenye dilemma ya kuku na yai. Low products haitotatua matatizo ya Networkers. Issue ni je wapo watanzania ambao wanafanikia na biashara hizi na Network Marketing yaliokuwepo Tanzania? Kama wapo wanafanya nini?

Nitamalizia kwa kutoa Quote ya Eric Worre:

"Network Marketing isn't perfect. It's just better"

Dr. Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…