Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Ummy Mwalimu aliteuliwa kuwa Waziri Nov 2015, ndani ya miezi 7 akaamuru Bodi ya NHIF iwafukuze kazi Wakurugenzi/ Wakuu wa Vitengo wote pamoja na DG wao kwa tuhuma za uwongo.
Katika hiyo timu ya Wagurugenzi 9, nusu yao walikuwapo kuanzia NHIF ilipoanzishwa mwaka 2003, wamekuwa na Mfuko hadi ukawa mmoja wa Mifuko Bora ya Bima ya Afya kwenye Bara la Afrika.
Unapowatimua Wakurugenzi wote unapoteza experience na institutional memory ya NHIF.
Hizo sababu zote wanazosema sijui madeni ya Serikali, forgeries za service providers etc ni visingizio tu. Tatizo kubwa lilikuwa ni Ummy Mwalimu mwenyewe. Aliwatoa hao Wakurugenzi ili akafanye UFISADI wake kupitia watu wataotekeleza maagizo yake. And she is super rich woman as of now
Pia soma: Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?
Mytake:
Jenista Mhagama/ Irene Kisaka; (1) Usirudie makosa ya Ummy Mwalimu kuondoa maafisa waliokuwa chini po ya DG wa zamani Benard Konga
(2) Watumieni hao wazoefu kupata ushauri (siyo kuwarudisha kwenye ajira) wa namna ya kuboresha mfuko. Najuwa wengi bado ŵapo na wana akili nzuri. Wapo akina Emmanuel Humba, Hamis Mdee, Frank Lekey, Michael Mhando, Mwamoto, Lobulu etc
Tusiogope hili mbona TASAC iliimarishwa kwa kutumia wafanyakazi wa zamani wa NASACO!!