otimbiotimbi
Senior Member
- Dec 12, 2019
- 132
- 230
Hivi karibun kumeibuka wimbi la watu wengi wakiuza gari hii kwa gharama ya chini sana na baadhi ya watu wakiogopa kununua na wamiliki nao wakiwa wanayachukia magari yao.
NISSAN X TRAIL
Ina block ya aluminium inawahi mno kupata moto kama injin ya Noah voxy 1az. Hivyo ukizembea kidogo tu katika mfumo wa upozaji wa injin basi gari hii itakusumbua sana. Hakikisha hawatoi thermostat. Hakikisha rejeta haina uchafu yani kutu, kuwa na kawaida ya kufanyia service rejeta. Ukifika carwash usioshe injini kwa pressure ya maji.
Gari hii usipo zingatia nilichokuelekeza hapo juu itaanza kusumbua na Ikisumbua ukipeleka kwa mafundi wa mtaani wakishindwa kurekebisha tatizo wanaanza kuwaambia wamiliki kuwa gari hizo mbovu na ndio kawaida yake mmiliki atatoka ataenda sehemu nyingine atakutana na mafundi wa mtaani tena maneno yatakuwa ndio hayo utasikia wanasema gari hii ni jini. Haya sasa ukimuuliza ambazo sio majini ni zipi?
Watakutajia gari ambazo wao wanaweza kubahatisha kutengeneza ndio kwao wanaona bora wakati tatizo sio gari tatizo ni wao wameshindwa kutengeneza na ukiangalia wanaoongoza kwakusema hivyo na kuwakatisha tamaa ni wale wanaoitwa mafundi wakuu.
Sasa akishasema hivyo mpaka wanafunzi wake wote wimbo ni mmoja majini hayo! Kama jana nilienda sehemu nikakuta Nissan Xtrail haibadili gia, fundi kapima na mashine ina mwambia kuna sensor imekufa kanunua nyingine kafunga tatizo liko pale pale nafika namuhoji ananiambia Mimi hiyo gari imenishinda yani nilikaa kimya tu mana huyo ndie fundi ambae anategemewa na vijana anafundisha.
Sasa hapo wamekaa pembeni na vijana wake unasikia wana sema hizi gari ndivyo zilivyo yani hawana muda wakuumiza kichwa fikra na maarifa yamefungwa ndani ya mashine anayo itegemea ikifika kikomo na yeye hana muda wakujifunza zaidi wala kutafuta maarifa kazi yao nikutisha wamiliki wa magari tu.
Nissan Xtrail ina sensor nyingi mno sasa mafundi wa mtaani somo la sensor hawalijui lazima wasumbuke na pia kwenye injin huwa ikianza kuchemsha hawajui wafanye nini.
Ni hayo tu kwa leo🙏🙂