Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 891
Rafiki yangu mmoja huko TZ alikuwa shabiki nambari wani wa Jakaya na wanamtandao wake.Leo amenitumia e-mail kuniambia kuwa mwelekeo wa serikali hii unatia wasiwasi mno.Hadi sasa haijulikani mshahara wa wafanyakazi serikalini utapatikana vipi lakini kama lilivyoandika gazeti la Mwananchi uwezekano mkubwa ni kwa serikali kukopa BOT.Wachumi wanaelewa madhara ya hilo,lakini kwa mie ambaye nilikwepa somo la uchumi kwa vile hesabu hazipandi nachofahamu tu ni kwamba kwa serikali "kuazima" fedha BOT itailazimu benki hiyo kuchapisha noti kibao na hivyo kuleta mfumuko wa bei.
Mimi nina wasiwasi kwamba JK alisukumwa zaidi na ambitions kuliko ability wakati anatangaza vita kuhakikisha piga uwe lazima aingie Ikulu.Wajuvi wa mambo wanasema kutamani kuoa ni kitu kimoja,kumudu gharama za ndoa ni kitu kingine,na kuimudu ndoa ni kitu kingine kabisa.JK alitamani urais.Akakusanya fedha za kutosha kutoka kila angle.Alichosahau ni kujiuliza kuhusu uwezo wake kama JK kuwa rais wa nchi masikini na yenye matatizo kama Tanzania.
Sio siri,rais tulokuwa tunamhitaji ni mtu mwenye uchungu wa dhati na nchi yake.Ni mtu ambaye angekuwa a dictator for the people,mtu ambaye asingeweza kuwaambia wala rushwa kuwa anawajua lakini anasubiri wabadilike.That was the first sign kwamba huyu jamaa ni mbabaishaji flani.Nilikuwa TZ wakati JK anahutubia bunge.Niliisikia hotuba yake na kuipenda japo nilikuwa na wasiwasi kwamba isije ikawa ni porojo tu badala ya mwelekeo wa serikali yake.Kingine kilichonivunja moyo kuhusu JK ni pale alipotangaza baraza lake la mawaziri.Kwangu tatizo halikuwa ukubwa wa baraza hilo bali hao walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali.Hivi kweli watu kama Kapuya,Mramba,Mungai,Dr Msabaha,na Wassira (to mention only a few) walistahili kuwemo kwenye timu inayopaswa kuwa na kasi mpya?Hawa ni viwete wa kisiasa na kibaya zaidi wengine wanajiona wana uzoefu wa uongozi kuliko bosi wao.Ndio maana utamsikia Mramba anakurupuka kusema serikali itanunua ndege nyingine ya rais licha ya matatizo lukuki yanayoikabili nchi yetu.
Nirudi nyuma kidogo.Kabla JK hajapitishwa na CCM kugombea urais,alikuwa the least of my favourite candidates.Hofu yangu ya kwanza ilikuwa ni tabia yake kama JK.Kuna jamaa nilikuwa nawafahamu pale Foreign Affairs na kila nilipowasiliana nao kuhusu possibility ya bosi wao kuwa rais walikuwa wanacheka.Why,bcoz walikuwa wanamwona kama mtu ambaye hawezi kuwa serious ktk lolote lile.Mmoja wa jamaa hao alinambia kuwa JK ni msanii,mtoto wa kijiweni kama Ditopile,na kama akipata urais basi wabongo watakuwa wanaishi kwenye tamthiliya flani ya vichekesho.Unajua ule utoto wa mjini wa kutumia madaraka kupata wanawake warembo halafu wanawake hao wanaishia kusema "ah,jamani...yani nimelala na kibosile halafu kaniacha patupu/kanikopa?"Ndio za JK katika enzi zake.
Rafiki yangu mwingine mwanahabari aliwahi kuwamo kwenye msafara wa Mkapa kwenda China ambapo JK alikuwamo pia.Mwanahabari huyo alinambia kwamba hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa karibu na JK,na aliyoyaona yalimfanya ashikwe na mshtuko siku JK alipotangazwa kuwa ndio candidate wa CCM (ambaye kimsingi ndio huwa anakuwa rais).Mwanahabari huyo alinambia kuwa JK alikuwa anafanya utoto flani ambao ulimwacha jamaa yangu huyo kujiuliza mara mbilimbili kama kweli TZ wana waziri wa mambo ya nje.Tulipokutana TZ baada ya JK kupata urais jamaa huyo alinieleza bayana kuwa Tanzania imeingia kwenye mtihani mkubwa zaidi ya ule wa vita ya Kagera.
Kuna mtu mwingine amenambia kuwa kimsingi serikali inaendeshwa na Lowassa kwa madai kuwa between the two of them yeye ndiye angalau ana "akili" kidogo.Tatizo la Lowassa ni hizo ambitions zake za kitoto za kuingia kwenye vitabu vya historia kama "Sokoine wa pili".Amekuwa mtu wa kukurupuka katika maamuzi yake,na ukimwangalia kwa makini sana utagundua kuwa staili yake ya uongozi haina tofauti sana na ya Lyatonga (sio kiufanisi bali kulipuka).Kila anakoenda anatoa siku saba,21 au miezi sita kutaka ufumbuzi wa matatizo.That's fine,kama orders hizo zingekuwa za dhati na si kujitakia sifa kwenye majukwaa ya kisiasa.Kuna haja gani ya kumuumbua Mkuu wa wilaya au mkoa hadharani badala ya kumwajibisha ofisini iwapo ana makosa?Hivi wenzangu mshajiuliza zile deadlines alizotoa rais wakati anatembelea wizara zimeishia wapi!?Nadhani nyingi ya deadlines hizo zilikuwa ndani ya miezi sita,na sasa jamaa amebakiwa na kama miezi miwili tu kabla hajatimiza mwaka madarakani.Viwanja bado vinauzwa na kugawiwa ovyo,hao maafisa wa ardhi waliodaiwa kuwa watatimuliwa na nafasi zao kuchukuliwa na wahitimu wa UCLAS bado wanaendelea kupeta,mikataba feki imeendelea kudumu huku kingine ya ajabu ajabu ikizidi kusainiwa including huu wa mitambo ya umeme wa kampuni ya Richmond.Kitendawili cha IPTL bado hakijateguliwa hadi leo na hakuna dalili ya uteguzi huo tukiwa na Waziri aliyechoka kama Msabaha.
Unapomteua mtu kama Mapuri au Adadi kuwa mwakilishi wa nchi sehemu flani unategemea nini.Mahita naye kapewa uenyekiti wa bodi ya TANAPA or something (pengine akauze mbuga zetu na wanyama waliosalia).
Kama alivyosema mwanzisha mada,inaweza kuchukua mwaka mzima kueleza disappointments za serikali hii ya awamu ya nne.Na hapa hata mwaka haujakatika.Nimseme ukweli,mimi nina wasiwasi sana na huko tuendako kuliko tutokako.JK ni mhuni flani ambaye haitokuwa ajabu akichemsha kuendesha nchi hata kabla hajamaliza awamu yake ya kwanza.Serikali yake haionekani kuwa na mwelekeo wowote,na Mungu nae ameamua kutoihurumia pale alipoleta ukame.Pengine alikuwa anatusaidia kutueleza jinsi gani tujiandae kukabiliana na kiama chetu baada ya kuchagua kiongozi kwa vile tu handsome wakati ni mchafu kimaadili (hivi ukiweza kusaliti ndoa yako unaweza kweli kuwa na uadilifu kwa nchi yako?)
Kama kuna kosa kubwa analofanya JK na wababaishaji wenzie basi ni hili la kuendelea kutoa ahadi wakati hata zile alizotoa wakati wa kampeni hajaanza kuzitekeleza.Asidanganye mtu kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani.By the way hata kisiwa kinaweza kuzamishwa na tsunami.JK kwa kutumia mtandao wake ametengeneza maadui wa kutosha tu.Hao wanaweza wasiwe na madhara kwake as long as ana support miongoni mwa wananchi.Lakini once hao maadui wake wa kisiasa watakapokimbilia kwa wananchi,basi si ajabu yalotkea Thailand yakatukumba na sie...