Matatizo ya Tanzania yaliasisiwa na waliopigania uhuru wa Tanganyika

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Salaam kwenu.

Ni kweli lengo la kupigania Uhuru wa Tanganyika, lilikuwa kuwafanya wananchi ama raia kuwa huru kuchagua aina ya uongozi na viongozi wanaotaka, kujiamulia mambo yao ya Kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni bila kuingiliwa na kikundi ama mataifa ya nje.

Lakini tujiulize hapa, baada ya uhuru kupatikana. Nini kilitokea?
  1. Je Watanganyika walikuwa huru kufanya shughuli za siasa ama waliamuliwa aina ya siasa ya kuifuata?
  2. Je Watanzania walikuwa huru kuchagua mfumo wa namna nchi itakavyoendeshwa? Au waliundiwa Katiba kwa utashi wa viongozi?
  3. Je Watanganyika walikuwa huru kujiamulia namna ya kuuendesha uchumi wa nchi yao au waliamuliwa namna uchumi utakavyoendeshwa?
  4. Je elimu ya Tanganyika ilikuwa kwa minajili ya kuwanasua watu dhidi ya ujinga?
Leo tunashuhudia chama kilichoasisi uhuru wa Tanzania kikisema wazi kupitia viongozi wake wakuu kwamba, hakitokubali kutoka madarakani hata kama Tanzania nzima wakisema NO!

Tujiulize, je tambo hizo ndizo zilizopelekea kumfukuza mkoloni ili tutengeneze kikundi cha wahuni watakaojimilikisha nchi kama wameiokota jangwani?

Tusipozinduka leo, tutaendelea kusubiri hisani za Rais ambapo ndiye anayeonekana kumiliki kila kitu bila kuhojiwa na yeyote.

I rest my case
 
Shida ilianza na list hii ya hapa ya wana TAA na baadae TANU
1. Master Forojo Ganze
2. Primus Julius Mubanga
3. Shekhe Yahya Hussein
4. Shaibu Kalole
5. Mfaume Goro
 
Baada ya uhuru na hiyo ya Tanganyika ikapotea hadi leo. Kuna haja ya kufungua kesi UN kuwadai waingereza ile nchi waliyoipa uhuru wakabidhi wananchi wa sasa sio wale wahuni
 
Kuna wazee maarufu mnawajua kwa majina. Hao wazee enzi za ujana wao walidai Uhuru wakasema they mature enough.
Hiyo mature enough iko wapi ikiwa mpaka sasa tunasaidiwa na watu ambao nchi zao hazina rasilimali nyingi zaidi ya akili?
Miaka mingi ya Uhuru kiongozi anasimama kuchukua credit kwenye vyoo vya shule vilivyojengwa kwa pesa ya msaada. Choo unajengewa kwa msaada.
Leo hii Afrika ukiwa chama pinzani ni kosa la jinai
 
Tafuta historia ya kweli ya uhuru usome. Kichwa chako kimejazwa uongo ndiyo maana unawalaumu.
 
Kuna wazee maarufu mnawajua kwa majina. Hao wazee enzi za ujana wao walidai Uhuru wakasema they mature enough.
Hiyo mature enough iko wapi ikiwa mpaka sasa tunasaidiwa na watu ambao nchi zao hazina rasilimali nyingi zaidi ya akili?
Miaka mingi ya Uhuru kiongozi anasimama kuchukua credit kwenye vyoo vya shule vilivyojengwa kwa pesa ya msaada. Choo unajengewa kwa msaada.
Leo hii Afrika ukiwa chama pinzani ni kosa la jinai
Huyo kiongozi, ni wewe ndiye umezembea kwa kumfanya awe kiongozi wako. Na ameenda kuomba pesa za kujengea choo, kwa sababu wewe au ndugu zako, hamtaki kujenga choo. Mabadiliko yanaanza na wewe, kuanzia kwenye maisha yako hadi kwenye sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom