The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 594
Wanabodi,
Tujifunze kitu hapa......Karibuni !
KATIKA kuyapuuzilia kwa mbali madai ya Waislamu imedaiwa kuwa matatizo ya Waislamu 'ni ya kihistoria'.
Ni kweli ni ya kihistoria. Historia ambayo Maaskofu waliziamrisha serikali za kikoloni - Ujerumani na Uingereza zisiwape elimu Waislamu na zikatii.
Hazikufanya ajizi, wala kubagua katika ukusanyaji wa kodi. Lakini shule chache zilijengwa na fedha nyingi zikatolewa kwa Makanisa. Kwa fedha hizo na misaada mingine Makanisa yakapewa uwezo wa kuendesha mashule mengi zaidi ya yale ya serikali, ili kuwalazimisha wananchi wengine wakabatizwe kwanza ndio wasome.
Hiyo ndiyo historia ya matatizo yetu. Ambapo serikali ya kikoloni iliweka sera maalum ya kufuga nguruwe katika maeneo ya Waislamu ili kuwaudhi na kuwatimua katika maeneo yao. Tazama Waraka wa serikali Na. 40 kuhusu agizo la Gavana wa Kijerumani kwa watendaji wake wa tarehe 13 Oktoba, 1913.
Ni kwa historia hiyo leo Rais anasema yeye ni Rais pia wa wala nguruwe, hivyo hatawagusa (hata kama wanaingilia haki na uhuru wa Waislamu) ila hatopuuza maoni ya Wakristo inapokuja sala la OIC.
Moja ya sababu ya wazee wetu kupigania uhuru wa nchi hii ilikuwa kuondoa historia hiyo ya kibaguzi. Lakini tumeshuhudia serikali ya awamu ya kwanza ikiimarisha utii wake kwa Kanisa kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
Ikavunja jumuiya za Kiislamu zilizokuwa zinasimamia ustawi wao katika elimu, afya na jamii. Na wakati huo huo kuzipa uwezo zaidi zile za Kanisa zizidi kujiimarisha.
Waislamu walizuiwa kuanzisha seminari. Wakristo wao wakapewa kila msaada ikiwa ni pamoja na kulifanya somo lao la 'divinity' kuwa moja ya somo linalokubalika kuingilia Chuo Kikuu.
Waislamu walipogundua udhalimu huu, na kufunga azma ya kuanzisha shule zao, ukatolewa Waraka wa kutozitambua shule hizo. Lakini nguvu za dola zilipotumika kuzivunja Waraka haukutumika tena kwa shule za Misheni.
Rais Mkapa anapodai matatizo ya Waislamu ni ya kihistoria, tunasema sadakta; na hii ndiyo historia yenyewe. Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam enzi za ukoloni wa Ujerumani, Askofu Cassian Spiss aliwaambia Wajerumani, msiwape elimu Waislamu. Na ikawa amri. Tazama Tanganyika Notes and Records No. 62/63, 1964. Kwa historia hiyo hiyo kujirudia kuwa kauli ya Kardinali au Askofu kwa serikali ni amri takatifu, hatushangai.
Wakati wa utawala wake, Rais, Alhaj Ali Hassan Mwinyi hakupuuza historia hiyo. Aliiendeleza; alimleta Pope, akaamrisha nguvu zote za dola ziwaangukie wale wanaowabughudhi wanaofuga nguruwe na kuweka bucha za nyama hiyo hadi kwenye vibaraza vya Misikiti.
Pia akaleta 'Memorundum of Understanding' ambapo sasa, serikali inawajibu wa kuzipa mabilioni ya fedha hospitali za Kanisa, kuyatafutia makanisa misaada na kuwapa upendeleo katika kusomesha wataalamu wao.
Lakini wakati akifanya yote hayo, kiongozi huyo wa awamu ya pili hakupuuza shinikizo la Maaskofu kwamba hakuna 'rukhsa' Tanzania kujiunga na OIC! Si hivyo tu, viongozi hao pamoja na kuujua ukweli huo wa "kihistoria" unaowanyima Waislamu haki ya kujiunga na OIC, kuvunja jumuiya zao na kufisadi mali zao za Wakfu, baadae hugeuka na kuwalaumu Waislamu eti hawana dira wala mipango ya kuendeleza jamii yao. Wakati mwingine kuwaambia Waislamu kuwa "wenzenu" wanaletewa misaada na "ndugu zao toka nje, nyie mbona hawaji kukujengeeni mahospitali makubwa". Mtadhani hawajui kuwa OIC ndio iliyotaka kuleta mahospitali hayo!
Zipo habari pia zinazosemekana kuwa Sheikh Mohamed bin Zayed wa Falme za Kiarabu alijitolea kujenga shule ya kisasa ya sekondari ya ufundi katika kisiwa cha Mafia, wakati wa kipindi cha serikali ya awamu ya pili, lakini serikali hiyo ilifanya ajizi baada ya kugundua kuwa wananchi wa Mafia ni asilimia 90 Waislamu. Kama ni kweli, nini kisa cha kuwalaumu Waislamu kuwa hawasaidiwi na ndugu zao?
Kinachofanyika leo kuna dalili zote za kuendeleza historia hiyo hiyo isiyowatakia kheri Waislamu. Ni jambo la kusikitisha na pengine kushtua kuona awali Mhe. Rais Mkapa aliyapokea madai ya Waislamu katika mazingira ya maelewano. Mazungumzo yaliyofuata pamoja na Halmashauri ya Waislamu yalidhihirisha pia kuwepo kwa maelewano, na zaidi kukubaliana katika mambo ya msingi yaliyotambua kuwepo kwa kasoro dhidi ya Waislamu.
Hali hiyo ya maelewano ndiyo bila shaka iliyowatia moyo Halmashauri ya Waislamu kumuandikia barua Rais Agosti 28, 1999 kuthibitisha muafaka wao na kupendekeza njia bora za utekelezaji wake.
Lakini majibu ya Rais katika barua yake ya Desemba 17, 1999 kwa Halmashauri hiyo ni kitendawili kikubwa. Ni nini kilitokea baada ya mazungumzo yale kiasi cha kumfanya Rais abadili msimamo wake wa awali. Barua yake imeonesha mgeuko mkubwa. Ni mgeuko wa U (U-turn). Hivyo tumelazimika kurejea kule kwenye historia yetu.
Kupiga marufuku EAMWS, kuzuia Chuo Kikuu cha Chang'ombe, kilichotaka kujengwa na Waislamu kwenye miaka ya 1960, kuzuia OIC, kukamata na kuwafunga Masheikh kwa mashinikizo ya Kanisa, na Padri wao (akina Lwambano) pamoja na kupiga hatua kidogo, kuua na kutojali sheria alimradi kiongozi wa Kanisa kaunga mkono kwa simulizi za Goliath.
Katika hali hiyo, ipo haja kwa Waislamu kuyarejea upya madai yao kama yalivyowasilishwa kwa Rais kwa maandishi na kuyatafakari upya majibu yake.
Jambo moja litadhihiri kuwa msamiati udini, umekuwa ukitumika kwa maana mbili tofauti lakini zote zikilenga kuuangamiza Uislamu na kuufanya Ukristo uwe dini rasmi.
Kwa upande mmoja, Muislamu hasa kiongozi wa serikali anayeonekana kuijali dini yake na kutoa haki sawa kwa wote bila kujali dini zao, huyu amekuwa akishutumiwa kuwa ni mdini.
Lakini kilicholengwa katika shutuma hizo ni kumfanya Muislamu huyu (asiyejiamini) aikane dini yake kimatendo, na kuifanya jambo la siri.
Awakimbie na kuwaona maadui Waislamu wenzake wanaoutekelezaa na kuupigania Uislamu wao. Lakini kubwa zaidi aungane na Wakristo kuona Ukristo ndio ustaarabu na ustaarabu wa Kiislamu ni jambo la kupigwa vita.
Ni Waislamu wachache katika masiku ya nyuma waliokuwa wameelewa mbinu hii iliyoasisiwa tangu enzi za awamu ya utawala wa Mwalimu Nyerere.
Na kwa sababu hiyo Waislamu wenyewe wakawa mstari wa mbele kumuunga mkono katika kuitumia mbinu hiyo dhidi ya Waislamu.
Ni kwa ajili hiyo walitumika pasipo kujua, na hivyo kumsaliti mwanaharakati, mpigania uhuru mzee wetu Shaahid Almarhum Sheikh Suleiman Takadir.
Aidha, bila ya kuelewa wakakaa kimya na kufumbia macho Masheikh Hassan bin Amir na wengineo walipokamatwa na kufungwa, kuteswa na baadhi yao kuhamishwa nchini mwaka 1964.
Wakati Waislamu walioko serikalini na kwenye uongozi wa siasa wakishughulishwa na propaganda za uzalendo huo, wenzao wa Kanisa Katoliki walikuwa wakiendelea na harakati zao za kihistoria. Waliendelea kukutana na kutekeleza maelekezo ya Kanisa na kisha kupeleka taarifa za utekelezaji Rome. Tazama Sivalon Uk. 15, na rejea yake Uk. 82 ambapo barua kumb. 15/9/9/173 ya Septemba 24, 1963 to Padri Welsh, Rome toka ofisi ya Mkurugenzi, Vice-President office. Tazama pia maoni ya Padri Welsh kwa wakoloni kuhusu Mwalimu Nyerere (Sivalon Uk. 21) na mikakati ya Padri Paul Crane (Sivalon Uk. 25).
Hapana shaka ni jinamizi hilo hilo la propaganda ndilo lililo wafumba macho baadhi ya Waislamu hususan waliopo serikalini wasiuone ukweli na hivyo wasitoke kwa nguvu zote kumhami Shahiid Prof. Kighoma Ali Malima alipoandamwa hadi kifo chake cha kutatanisha.
Kiwango cha kuzugwa na kurogwa bongo za Waislamu, kilidhihiri kupea kwake mwaka 1995, wakati wale wale waliyemuangamiza Sheikh Takadir na kina Sheikh Hassan bin Amir walipowafanya waone kuwa kila anayefuata mila ya Nabii Ibrahim ndiye mdini.
Ila aliye mzalendo ni anayefuata maelekezo kutoka Vatican na aliye mcha Mungu kwa vigezo vya Kadinali Pengo.
Hatujui wazalendo hao leo wanajisikiaje wanapogundua kuwa wao ndiyo walio tuundia serikali ambayo imepokea amri ya Paroko wa Kanisa Katoliki.
Msikiti ukavamiwa, Masheikh wakakamatwa, wanawake wakadhalilishwa na watu wakauliwa.
'Wazalendo' hao 'wasio na udini' wanajisikiaje leo wanapogundua mchango wao unakandamiza katiba na sheria isitumike kuhukumu kadhia ya Mwembechai.
Hapana shaka umati uliokusanyika Diamond siku ya Eid una ujumbe wake muhimu.
Kule watu kuacha mabaraza yao, na kuwa na Baraza moja, ile kukutana watu wa ngazi zote, Masheikh, Maustadh, wazee, wafanyabiashara ndogo ndogo na wafanyabiashara wakubwa, waajiriwa serikalini na katika sekta za umma wa ngazi za chini na juu na watalaamu mbalimbali wakiwemo wanasheria, wote hawa wakijadili madai ya Waislamu kuwa ipo dhulma na ubaguzi dhidi yao na hatimaye kulaani dhulma hiyo na kuahidi kupambana nayo, ni dalili njema.
Ni ishara tosha kuwa ile siri ya lile 'bangi' la kuwazuga Waislamu imefikia hatma yake.
Kila Muislamu sasa anajua, anayeshutumiwa kuwa na udini ni Muislamu yeyote anayependa dini yake na anayechukia dhulma dhidi ya Waislamu.
Kwa upande mwingine anayedaiwa kutokuwa mdini ni yule ambaye yupo tayari kulihami kanisa lake kwa gharama yoyote bila kujali katiba ya nchi, sheria na haki za binadamu.
Hilo tunaamini Waislamu wengi wamelielewa. Ila magugu na chuya hazikosekani. Hao ndio wale ambao Qur'an inasema:
"Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahanamu wengi katika majini na wanaadamu (kwa sababu hii): Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo (Hawataki kufahamu kwazo), na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama; bali wao ni wapotofu (wapotevu) zaidi. Hao ndio walioghafirika". (7:179)