Msafiri Haule
Member
- Aug 6, 2018
- 28
- 18
Ndugu Watanzania,
Ni wazi kwamba tangu tupate uhuru 1961, chama kimoja tu ndiyo chama tawala.[emoji21]
Mantiki ni kwamba, ndicho chama kilichoshiriki aidha dhuluma au faida kwa watanzania, maana ni chama kinachounda serikali kwa nyakati hizo zote.
Vilio vya mtanzania, ni sehemu tu ya kicheko kwa wenye nchi ambao ndiyo wanaounda Serikali. Kinyume na katika kabisa inaposema "wenye mamlaka ni watu..." nami nadiliki kusema nchi yetu haina mamlaka ya watu wake (public), zaidi ni chama kinachotoa ilani ambayo hitumika kama MKATABA baina ya watawala na watawaliwa kwa miaka yote hii.
Ni wazi kuwa, watanzania wachache wameendelea kutambua uozo wa chama kilichoongoza tangu mimi bado sijafikiriwa kuzaliwa, lakini, wananyakuliwa na walewale ambao nimewataja hapo juu kama ni tatizo.
Wakoloni, hawakutuachia Tz ya uchama wala ukabila kama ilivyo Kenya na Nigeria, lakini sisi, ni mazonge yetu wenyewe tukakubali kuhalalisha kila jema na baya kwa chama tawala.
Wahenga hunena "money begets money", na ndivyo naona kwa chama tawala, kitafanya LOLOTE lile ili utawala wake usidhurike. Nyakati zasonga, watanzania wengine tangu tupate uhuru bado hawaoni thamani ya uhuru wao maana wananyimwa hata "uhuru wa kufikiri" baada ya kutungiwa sheria kadha wa kadha ili tu kudhihaki yaliyomo vinywani mwao.
Wakulima hawaoni thamani ya mazao yao (nikiwemo), na wenye itikadi huendelea tu kuwaita wazalishaji hao kuwa ni WANYONGE. Unyonge wetu unaendelea kutudidimiza wenyewe.
Kuna wakati, kula sana nyama nako kunaleta "SHOMBO", ni muhimu walau kuwaza mbadala wa kubadili mfumo huu wa chama kimoja ulioota mizizi mpka hivi sasa unatazamia kutotoa "VILEMBWE".
Maendeleo hayana chama, yes. Lakini tunakumbuka kipindi cha kampeni hata pale KILWA? Je, dhima ya maendeleo kutokuwa na chama ndo hii kujipigia upato?
Ni kweli, maendeleo huanza na adhma ya dhati nafsini kwa mtu. Lakini, nimeshuhudia mamia na maelfu ya watenda kazi haswa, but return ya kile walichofanya ni asilimia 20. Hii ni hasara kubwa, sasa kwa mantiki hiyo tumlilie nani kama siyo mifumo mibaya ya chama? Je, hatutoshi kusema nao pia hawatoshi kuendelea kutuongoza kwa kipindi chote hiki?
Sioni faida ya siasa ya UVYAMA. Inawezekana tunakwama kila sehemu, the problem ni kuhitaji kuhifadhi "matarajio yao" (interests), na hapo hutuacha wengine tuking'oka meno.
Haiwezekani kila ukigusa eneo la kufanyia reform, jibu huwa mara ooh siyo kipaumbele cha chama! Haipo kwenye katiba ya chama! Siyo itikadi yetu! Na madudu kibao.
Itoshe kusema, tunahitaji kufanyia kazi MFUMO WA SIASA YA CHAMA KIMOJA.