MATATIZO YA YANGA NDIYO YALIYOWAPA UBINGWA SIMBA, HILO WALITAMBUE

MATATIZO YA YANGA NDIYO YALIYOWAPA UBINGWA SIMBA, HILO WALITAMBUE

yamindinda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
1,581
Reaction score
1,318
MATATIZO YA YANGA NDIYO YALIYOWAPA UBINGWA SIMBA, HILO WALITAMBUE



Yanga imekuwa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa misimu mitatu mfululizo na pia ni mabingwa wa kihistoria wakiwa wametwaa taji hilo mara 27.

Watani zetu Simba leo wamefanikiwa kutwaa ubingwa wao wa kwanza baada ya kukaa 'juu ya mawe' kwa misimu mitano, huo pia ukiwa ni ubingwa wao wa 19.

Nyakati kama hizi huwatokea mabingwa wote kwani hakuna timu ambayo imewahi kuwa bingwa miaka yoooote.

Kwa changamoto iliyopita Yanga msimu huu hakika wachezaji pamoja viongozi wanastahili pongezi kubwa kwa hapa walipoifikisha timu.

Bila ya umoja na mshikamano wao pengine Yanga ingekuwa na hali mbaya zaidi ya hii tunayoiona sasa.

Licha ya mazingira magumu waliyopitia, wachezaji walijitoa kwa moyo mmoja kuipigania Yanga. Tutakuwa hatuwatendei haki kama tutawalaumu leo.

Sawa wamekosa ubingwa, lakini wameifanya Yanga kuwa ndiyo timu iliyotengeneza 'mkwanja wa maana' kuliko hata Simba iliyotwaa ubingwa.

Baada ya changamoto zote, msimu huu umetoa funzo kubwa ambalo hakika litafanya Yanga imara izaliwe.

Ilikuwa ni lazima Yanga ipitie changamoto hizi msimu huu ili iweze 'kuzaliwa upya' ikiwa na misingi imara na bora zaidi.

Naamini baada ya Mkutano Mkuu wa Wanachama mwezi ujao (Juni 17) Yanga itazaliwa upya ikiwa imara mara dufu.

Kwa sasa msimu umeisha naamini uamuzi wa uongozi wa Yanga kutilia mkazo michuano ya kombe la Shirikisho ni wa maana kwani hakukuwa na namna kwa Yanga kutwaa ubingwa wa VPL.

Yanga kama itafanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho itavuna pesa zaidi zitakazosaidia kutatua matatizo mbalimbali.

Michezo iliyobaki ya VPL na wapewe nafasi vijana ambao hawakuwa wakitumika michezo iliyopita kama walivyofanya leo.
Daima mbele nyuma mwiko

Credit:[HASHTAG]#yangasoka[/HASHTAG]
 
Yanga kama itafanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho itavuna pesa zaidi zitakazosaidia kutatua matatizo mbalimbali.
:
Una roho ngumu sana. Yaani unawaza Yanga hii kuingia robo fainali?
 
Mpira ni mchezo wa makosa ya kiuongozi au kimbinu uwanjani. Ukikosea mwenzako anakuzidi. Ikumbukwe simba pia misimu mitano iliyopita wamekuwa na ukata wa kifedha. Pia simba wameimarika zaidi. Linganisha idadi ya alama walizofikia msimu huu na alama walizofikia mabingwa wa zamani na pia mpaka sasa hawajafungwa na timu yoyote. Kama yanga imeshuka na timu zingine je? Simba haishindani na yanga tu.
 
Back
Top Bottom