Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wakati wa Uhai wake, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuishi katika nyumba hii ikiwa ni baada ya kurejea nchini akitokea masomoni nchin Uingereza.
Huko alihitimu masomo yake na kutunukiwa shahada ya uzamili katika masomo ya uchumi na historia kwenye Chuo Kikuu Cha Edinburgh, akiwa ni mtanzania wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini humo.
Licha ya kuitumia nyumba hii akihudumu kwa kazi ya ualimu kwenye shule ya Sekondari Pugu, hapa ndipo palifanikisha kwa asilimia kubwa kutungwa kwa katiba ya TANU.
Mkazi wa nyumba hii kwa sasa ni Mwalimu Andrew Cheyo wa shule ya Sekondari Pugu ambaye anasema akiwa hapa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitumia muda wake wa ziada kukutana na wazee wa chama cha TANU na kuandaa mipango iliyofanikisha kwa kiasi kikubwa kutungwa kwa katiba ya chama hicho.
"Hapa alikuwa anakutana na Wazee waTANU, hatua iliyopelekea kupigwa marufuku na uongozi wa shule wakati ule, na ndipo alipoamua kuwaelekeza Wazee waliokuwa wakija nyumbani kwake nendeni kajiungeni na ofisi iliyokuwa eneo la Pugu na hapo ndipo palipozaliwa Pugu Kajiungeni," ameongeza Mwalimu Cheyo.
UKWELI WA HISTORIA YA TANU
Katiba ya TANU ilinakiliwa neno kwa neno kutoka katiba ya Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah.
Sababu ya kufanya hivi ilikuwa kukwepa kukataliwa katiba yao endapo wangepeleka kwa msajili.
Kwa kuwa katiba ya CPP ilikuwa imepita Waingereza wasingeweza kuikataa katiba ya TANU.
Hakuna mzee yeyote aliyekwenda kwa Nyerere Pugu kwa ajili ya shughuli za TAA au TANU.
Mikutano yote ya TANU na kuanzia TAA mwaka wa 1950 ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Kuna kibao kimewekwa miaka mingi nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi ikidaiwa kuwa hapo ndipo ilipozaliwa TANU: