Kimsingi yapo matatizo yanayoweza kusababishwa na kutumia computer kwa muda mrefu, kutopata matatizo haina maana kuwa hayapo bali inategemea na set up ya mwili wako. Mtumiaji wa computer kwa muda mrefu anaweza kupata maumivu ya kichwa na macho yake kuuma,. Hii ni kwa sababu ya kukodoa macho kwenye computer kwa muda mrefu BILA KUPWESA. Kitendo cha kutopwesa kina madhara kiafya na mara nyingi mtu akitumia computer huwa anakodoa macho directly na hapwesi. Ili kuondoa madhara hayo inashauriwa mtu awe anapwesa kila baada ya muda fulani.