Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,208
- 14,143
Ulikuwa unajitambua miaka ya ngoma imeshika hatamu.Asikwambie mtu wengine walikuwa wanaenda kumshuhudia mgonjwa jinsi alivyo konda kisha kwenda kusambaza umbea.Ni upuuzi kuona anaekuja kukuona wakati unaumwa anakuja kukuchunguza or mbea. Ugonjwa ni suala mtambuka hakuna anaependa kuumwa.
Anaekuja kukuona ni vile anakujali na kukuthamini ndio mana anakuja kukuona. Ukiumwa na ukatembelewa na MTU inakupa faraja mgonjwa na pia kukupa hata unafuu fulani mana kinga za mwili zinaimarika.
Binafsi huwa nawaona washamba na watu katili sana wenye tabia hizo za kutoa Maneno ya hovyo linapokuja suala na maradhi.
Sisi ni binadamu tumeumbwa tofauti na wanyama kujuliana hali ndipo tofauti yetu na wanyama ilipo.
Umenikumbusha mbali sana bwana bwana kipindi hiko huo ugonjwa ndo watu wanabaki kichwa tu na mbavu walikua wakali hatari hatariii hata kama mtu alikua mstaarabu lakini akishaanza kuumwa tu anakua na mikwara dunia hakunaUlikuwa unajitambua miaka ya ngoma imeshika hatamu.Asikwambie mtu wengine walikuwa wanaenda kumshuhudia mgonjwa jinsi alivyo konda kisha kwenda kusambaza umbea.
Wagonjwa wa ukimwi walikuwa wakali kweli halafu hata kuinua mkono hawawezi ila sauti ya ukali kubwa !!
Kuna watu wa ajabu sana duniani. mtu anaumwa, kumuona hawaendi na taarifa zako wanasambaza. shukuru Mungu unaruhusiwa hawajui wanaendelea kusambaza uko mahututi. ghafla wanakutana na wewe, mnasalimiana wakupa pole, wanasema tulipata taarifa kwa fulani uko mahututi (aliyewapa taarifa hakuja kukuona wala hakuwasiliana kwa simu) ndio utajua kuna wasemaji wa familia wakujitolea na wengine wanatoa huduma hiyo online tena bure.