NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Mtu aliyezaliwa mwaka 1959 kwa sasa ana miaka 62. Kama alianza kidato cha kwanza mwaka 1975 ina maana amemaliza kidato cha nne mwaka1978. Kama amesoma kozi mathalani ya uuguzi kwa miaka minne maana yake amemaliza1982. Ajira ameanza mwaka1983.
Ukipiga hesabu hapo hadi mwaka 2019 atakuwa amefikisha miaka 60 ndio anastaafu na atakuwa amefanya kazi ya utumishi kwa miaka36.
Huyu muuguzi amefanya kazi kwa uadilifu mkubwa mno miaka yake yote amejitoa mhanga na amekumbana na hatari nyingi sana kukoswa koswa na kuambukizwa magonjwa mbali mbali siyataji ila kwa sasa ugonjwa wa changamoto za kupumua kama unavoitwa siku hizi wakati mwingine hata Ebola.
Muuguzi huyu amekutana na madhila wakati mwingine hata kuhatarisha ndoa yake kwa kufanya kazi usiku akiacha watoto wake na mumewe shauri ya kuingia night. Muuguzi huyu anapokwenda kazini usiku kwa usalama wake hata kuvamiwa na vibaka aidha akienda au akirudi. Muuguzi huyu wakati mwingine anakutana na wagonjwa waliokengeuka akili kumuambia maneno machafu. Muuguzi huyu hata pia amehatarisha maisha yake maana amekutana na wagonjwa wenye akili pungufu wanaweza kumdhuru. Hivi karibuni kuna mgonjwa alimchoma kisu muuguzi akafariki dunia. Muuguzi huyu kazi yake alikuwa hana siku kuu ilimradi kama ni zamu yake hakuna sikukuu mfano hizi za pasaka.
Muuguzi huyu sisi masikini, wanasiasa, watu wakubwa sana wa serikali, mashirika, vyama vya siasa, maraisi, wafalme, malkia n.k unapozidiwa anageuka anakuwa kama mama au mke wako anakuogesha na kukulisha chakula. Hapa hata aibu yako anaiona anakutunzia siri hata kama una kovu mahali flani.
Kimbembe sasa ngoja kinakuja siku ya kustaafu pamoja na wema woote na kujitolea maisha yake yote anaonekana kama vile tinga tinga linalochimba barabara linatengeneza barabara vizuri sana lakini barabara ikiisha halitakiwi tena kuikanyaga hiyo barabara na hata likipita litaambiwa linabomoa barabara. Na sana sana likionewa huruma sana litapita kwa ungalizi maalum likiwa limebebwa na Trailer lingine.
Basi mfanyakazi wa umma,sekta binafsi ndio inakuwa hivyo mtu akistaafu hatakiwi tena.Mfuko wake mwenyewe aliojinyima maisha yake yote anaupata kwa shida sana au kwa mateso makubwa mno hii hata mbele ya mungu ni machukizo makubwa taifa linaingia kwenye laana bila kujua nasikia eti laana inaweza kwenda hadi kizazi cha nne labda atokee mjanja mmoja ashtuke kwa kufanya tambiko au maombi.
Hii mifuko ya jamii nauliza inamsaidia vipi mstaafu au ni siasa maana kipindi unapoanza kazi wanavyokuja kukubembeleza ni sawa na konda ukipanda gari anakubembeleza anakuambia kuna siti za kulala ila gari likifika kituo cha mwisho hataki hata kukuona usoni afadhali kwenye ndege. Hapa nimetoa mfano huu afadhali kwenye ndege nikiamanisha baadhi ya nchi hasa zilizoendelea mtu akistaafu anaishi maisha raha mustarehe japo sio ya kifahari hadi kifo chake kwa sisi ni tofauti.
Naandika haya kwa uchungu dada mmoja amefanya kazi miaka niliyoianisha na amestaafu december mwaka2019 kwa maana hiyo anatafuta mwaka wa pili sasa achilia mbali kinywa mgongo chake hajapata hata senti tano.
Kama ni faili na mahesabu ni mahesabu gani yanapigwa kwa muda wa miaka miwili? inauma sana hii kitu. Last few months kuna askari walistaafu mhe Marehemu John Pombe Magufuli(Mungu amuweke pema) aliweka biti flani kuwa waliostaafu hao askari wapewe mafao yao haraka nina uhakika hili lilifuatiliwa na marehemu inaonekana anajua kuna mizengwe kwenye kulipa wastaafu. Je, huyu Muuguzi, daktari, mfamasia, mkutubi, mwalimu n.k ni nani anayewalilia?
Nimeshapata jibu kuna usemi unasema mtu akistaafu anaishi maisha mafupi sio kweli ni kwamba angeishi lakini kwa frustration kama hizi lazima kweli mtu atakufa na tena nachelea kusema wengine wanakufa kabla hata ya kuchukua mafao yao.
Mimi binafsi ingekuwa ni choice mtu aamue mafao yake yaingie wapi nisingechagua mfuko wowote wa kijamii ila sana sana ningefungua akaunti maalum benk ambayo naweka sharti siruhusiwi kuchukua ili angalau wakati nachukua wakati huo kutakuwa tayari na faida kuliko mifuko yetu hii inayozingua zingua sana. Naelewa mifuko iko tofauti ila samaki mmoja akioza ni wote.
Mimi ningependekeza kitu kimoja mtu anapokaribia kustaafu mwaka mmoja kabla taarifa inatolewa mahesabu yanaanza kupigwa kabla muda wa kustaafu ukifika analipwa muda huo huo.Wakati wa utawala wa JK kuna chombo kiliwekwa kusimamia hii mifuko yote je hicho chombo kinasemaje kwenye hili? Mimi nina uhakika kabisa kuna baadhi ya kada za kazi humu nchini hizi shida haziwagusi wanasiasa wakiwepo ambao ndio watunga sera hizo hizo za mafao.
MAMA SAMIA NAKUOMBA SANA MAMA YETU NAJUA UNA KAZI NYINGI NA CHANGAMOTO NYINGI MNO KAZI YA URAISI SIO RAHISI KAMA WATU WANAVYOFIKIRIA NAOMBA UCHUNGULIE HUKU KWENYE HIVI VYUNGU VINAVYOWEKA HELA ZA WATU HAZITOKI KULIKONI.