Mathayo 7:13-14 SRUV
[13] Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. [14] Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.