Inategemea, matibabu ya kisaikolojia ni matibabu ambayo yanahusisha akili ya mwanadamu. Akili ya mwanadamu inafanya kazi ya kufikiri (Thinking), kutazama mambo (Perceiving) na kuamua (Deciding). Sasa endapo mtu akipata tatizo Fulani ambalo likaathiri hayo mambo matatu atahitaji afanyiwe restoration (Marekebisho) ya akili yake, kazi ambayo ni ngumu sana. Hebu chukulia mfano wa MTU aliyeachana na mchumba wake versus MTU aliyefiwa na mke/mume wake kipenzi, watu Hawa wawili watakuwa na uzito tofauti wa matatizo yao ya kisaikolojia, tiba ya kisaikolojia ni tofauti na tiba ya (Medicine) ambapo MTU anaweza kunywa dawa kwa maelekezo ya muda Fulani. Lakini kwenye tiba ya kisaikolojia inategemea na uamuzi wa MTU mwenyewe kukubaliana na hali inayomsumbua au kutokukubaliana (Denial). Kwa hiyo hakuna time frame katika matibabu ya kisaikolojia ila kuna muda wa matazamio.