Matofali yanayozalishwa siku hizi siyo imara, mamlaka ziingilie kati

Matofali yanayozalishwa siku hizi siyo imara, mamlaka ziingilie kati

lalie

Member
Joined
Jan 6, 2024
Posts
26
Reaction score
34
Hii inamhusu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mheshimiwa watu wako wataangamia kwa kukosa maarifa!

Kuna watu wanafanya biashara ya kutengeneza na kuuzwa matofali kila mahali. Ni biashara nzuri na wanatoa huduma. Lakini mheshimiwa hili ni bomu kubwa la miji na vibanda vyetu!

Mfuko mmoja wa cement hutoa mpaka tofali 55! Matofali haya yakipata unyevu yanavimba, yakikauka yananyea. Ikijirudia kwa muda fulani yanapukutika. Nyumba inakatika kiuno.

Hakuna udhibiti wa ubora wa matofali haya. Tutalia muda si mrefu! Mheshimiwa huo ni mtonyo mdogo tu, ingilia kati.
 
Back
Top Bottom