Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Hata wewe fuatilia hiyo number kuhusu kuongezewa hayo masomo kwenye matokeo
 
Fuatilia huyo wa 01197/0173kwenye matokeo uone kama kuna ukweli wa kuongezewa hiyo bookeeping na commerce kuhusu ufanyaji wa mitihani wa huyo mwingine mpaka muhisika ndio athibitishe

Anatupa mashaka hata hayo mengine aliyosema kama ni ya kweli!
 
Kweli hapo sasa ni hatari ngoja tusubiri wahusika mbona wametajwa direct wananfunzi washule husika na walimu wapo na pia hata wizara ipo watumajibu yaliyojitosheleza
 
Wajinga sana nyinyi hamkujiandaa imekula na kulala kwenu! Hamna kitu kama hicho.
Mimi sijamaliza mwaka jana! Nilisoma Mzumbe - o level, Songea Boys - a level na UDSM,BSC na sasa nasoma Master OUT
 
Huyu Mkurugenzi ni fake na hajui anachozungumza. Inawezekana kuna mwanafanzi ameweka namba ya mwenzake kutokana na ukilaza ulitarajia baraza la mtihani lifanye nini? Si wakati mwingine wanaleta watu kuwafanyia ndio amechanganya namba! Mkurugenzi anapokuwa na upeo mdogo sijui wanafunzi watakuaje.
 
warudie kusahihisha. wakigundua kuna kuchakachua matokeo waadhibiwe vikali wahusika
 
Watz bana! Mnashangaza sana, mtu alimradi situation imemfavour yeye, basi kwa mwenzie ambaye either haikuwa favourable au kuna dhuluma huwa hatujali. Shule na wazazi wanafahamu sana uwezo wa mwanafunzi kuliko mtu yeyote, so mtu anapotoa hoja yake iangaliwe kwanza. Labda wengine mko mbali sana na jamii, mi ni mara nyingi nimeshuhudia malalamiko ya wazazi juu ya kufeli watoto wao, especially mwanafunzi ambae unakuta uwezo wake ni mkubwa tu, na kuna wengine wanafaulu lakini hawakuwa na uwezo darasani kama matokeo yao yanavyoonyesha.

kuna wachache wako lucky, wana uwezo na matokeo yao yanatoka kama yanavyotarajiwa. matokeao ya wale waliofaulu bila haki wanaishia kutokuwa na uwezo wa kutosha katika masomo ya juu na ndipo mnaposhusha viwango sasa. mbona waalimu wengi wa chuo huwa hawaishi kushangaa div 1 ambazo hazilingani na uwezo wa darasani? Baadhi hawana uwezo kama ufaulu wao unavyoonyesha.

Ni lazima tukubali kuwa kuna tatizo mahali, itafutwe hata mbinu mbadala ya usahishaji wa mitihani, inawezekana udhaifu unatokea kwa kutokuwepo na umakini kwenye usahishaji na upangaji wa matokeo. Kiwango cha makosa ni kikubwa mno.

Hivi mtoto asiye na uwezo darasani ana muda wa kukasirika na wengine kudiriki kunywa sumu huku akijua kabisa kuwa hawezi! mbona huwa wanatangulia wenyewe tu kukataa shule? wenye uwezo akifeli ndio anachanganyikiwa kweli, maana hajui afanye nini tena, na zaidi ukute hana wazazi watakaoweza kumtoa hapo, wanaishia wakati mwingine kutaka kujiua. uchunguzi ukiwepo lazima kuna madudu yatagundulika huko baraza, ila tu watz tuna jadi ya kunyamazia mambo hata kama yanatuumiza.

Kwa mfano mi nina swali kuhusu private candidates; hivi wanafunzi wote wanaorudia mitihani (wengi ni wale walioamini kuwa hawakupewa matokeo sahihi) wakitaka kurekebisha ili wasonge mbele, huwa wanashindwa kweli? au kuna biashara hapo ya kukusanya hela za warudiaji kila mwaka?
 
Hata mimi bado naendelea kuamini kuwa kuna hujuma katika usahihishaji wa ile mitihani
 
Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.
Sasa huyu naye wanamtafutia nini? Au wanataka tu kutuchekesha tulionuna?
 
uje na data kamili na uache uongo. Grean acres nani hakufanya mtihani na kawekewa maks. Tupe namba


HUwa nashangaa sana tatizo lenu huwa hamsomi unakurupuka kujibu tu ahahhaaaa


Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.
 
[table="width: 70%"]
[tr]
[td="width: 6%"]s1197/0148
[/td]
[td="width: 4%"]m
[/td]
[td="width: 6%"]24
[/td]
[td="width: 4%"]iii
[/td]
[td="width: 58%"]civ-d hist-d geo-c kisw-d engl-c phy-d chem-c bio-c b/math-d
[/td]
[/tr]
[/table]
 
Naamini haya matokeo ya mwaka huu hayapo sawa. Ama yamelipuliwa, kukosewa kwa bahati mbaya au kuhujumiwa kwa makusudi.

Kuna data nafanyia kazi, I will come with more arguable observation later...
 
[table="width: 70%"]
[tr]
[td="width: 6%"]s1197/0148[/td]
[td="width: 4%"]m[/td]
[td="width: 6%"]24[/td]
[td="width: 4%"]iii[/td]
[td="width: 58%"]civ-d hist-d geo-c kisw-d engl-c phy-d chem-c bio-c b/math-d[/td]
[/tr]
[/table]
 
Ingekuwa nafuu hata kama huo utafiti tungekuwa tunaufanya, Ndalichako anasema wamefeli eti kwa sababu clouds walimpa promo aliyeandika mashairi mwaka jana. Ndo utafiti wetu huo

Inaonekana pana tatizo katika kunukuu mtu alichosema. Ndalichako amesema watoto walioandika madudu (bongo fleva; katuni, n.k - nime2mia madudu kwa kuwa sivyo walivyotakiwa kuandika) wameongezeka kwa sababu clouds fm walimpa promo yule wa mwaka jana.
Hakusema wamefeli kwa sababu hiyo
 
Mungu wangu!!!!
nchi inaisha hii,
huyo waziri anangoja nini huko kwenye ofisi zetu?
 
Tanzania hatuko serious, huyo msemaji anatoa maelezo mepesi kama hayo, na wala haoni kama ni tatizo kubwa.
Sasa kama mwanafunzi A hakufanya mtihani akawekewa majibu ya mwanafunzi B, je mwanafunzi B kawekewa majibu ya nani? Kama mwanafunzi B alikuwa na uwezo mkubwa akawekewa majibu ya kilaza si atakuwa ameshahadhirika kisaikolojia? Je mkurugenzi asingetoa malalamiko ingekuwaje? Kama baraza lina matokeo ya mwanafunzi ambaye hakufanya mtihani, kuna uwezekano pia wangempa cheti chenye hayo matokeo.
Yatakuwepo makosa mengi tu kama hayo, hilo ni moja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…