Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Hayo ni matokeo ya "GIGO-GABBAGE IN GABBAGE OUT". Ukijaza matokeo kwenye namba ya mtu ambaye hakufanya mtihani, komputa haitakataa.
 
Habari wakuu
Nimeshangaa kusikia kuwa matokeo ni feki na mkurugenzi wa shule ya green acres akisema matokeo ya kidato cha nne yamechakachuliwa kwan kwenye shule yake kunawanafunz hawakufanya mitihan lakn wamejaziwa alama na ni za kufaulu maana mmoja wapo ana III 24.Pia jamaa amesema anashangaa kuona watoto waliokuwa wakifanya vzur kuanzia kidato cha kwanza wakifeli wakati wale waliokua hawana uwezo wakifaulu akasema anaomba wasahihishe tena kwani matokeo yamechakachuliwa.
Wadau mnasemaje
TANZANIA DAIMA
 
Anatafuta umaarufu kisiasa, kwani haiwezekani hicho kitu kikatokea zama hizi za digital.
 
Kama ni kweli na mimi nita"appeal" kwa matokeo yangu ya miaka 15 iliyopita inawezekana nilipata 1 ya 7, yenye A's 9 kama Mbunge wangu Hon. Mnyika..lol
 
Kati ya shule zilizokuwa zinaongoza kwa udanganyifu wa aina zote hapa Bongo, ni hii ya Green Acres. Mmiliki wake Bujugo ni msanii wa kufa mtu. Miaka yote huwalipa walimu wake posho maalum ya kusolve mitihani darasani wakati wa mitihani, then wanafunzi wanafanya kukopi solution ubaoni na kupesti kwenye karatasi zao za majibu. Waliovujisha hizo ni wanafunzi wenyewe wanufaika wa huo mpango, si unajua huwezi kuvundika embe kwa kificho na watoto kwani watatoa siri tu kuwa pale tumevundika embe! Habari zilipovuja kwa sana akadhibitiwa effectively kuanzia last exams. Wanafunzi wake chali. Anaibuka na tuhuma hizi, akate rufaa sasa ili shule yake isahihishwe upya mbona simpo tu!
 
Hiyo kashfa siyo ndogo hata kidogo! Wahusika watoe ufafanuzi wa kueleweka na siyo bulaha bulaha!! na ushabiki usio na mashiko kwa ujenzi wa Taifa letu! NB: Kawabwa asipotatua masilahi ya walimu basi hata asipo jihuzulu mwaka huu basi ajiandae kujihuzulu mwakani. Kimsingi walimu kwa sasa wanapongezana kwa wanafunzi kufeli na wanatiana moyo kuwa hali itakuwa hivyo hadi kilio chao kitakapo sikika na serikali. Ni hayo tu.
 
Ni ukweli usiopingika matokeo yamechakachuliwa. Mdogo wangu alifanya masomo ya Arts lakini yaliyotoka ni ya Sayansi i.e. Phsics na Chemistry ambayo hakufanya. There is no seriousness. Ni vyema matokeo yahakikiwe na doubts ziwe cleared
uje na data kamili na uache uongo. Grean acres nani hakufanya mtihani na kawekewa maks. Tupe namba
 
najaribu kufuatilia matokeo kama alivyosema mkurugenzi wa green acres-shule yake inatumia jina lipi mbona kwenye necta nimefyngua shule siioni?au wameiondoa?kama wameiondoa ndio basi itathibitika kuwa ni wizi
 
watoto wa siku izi hawasomi wanakalia kuchat fb nakwenda maclud watoto na wenyewe wanachangia
 
Tutapata lini mawaziri Tanzania wenye kuwajibika kuhakiki mambo sio kuletewa na maswali yakianza hana jibu la kulijibu taifa? wanafanya fyoongo na wakipigiwa sim kuthibitisha hawapokei kana na sipika bungeni anawakumbatia?
nina hasira na serikali hii basi tu.
 

[TD="width: 6%"]
S1197/0173​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
M​
[/TD]
[TD="width: 6%"]
34​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
FLD​
[/TD]
[TD="width: 58%"]
CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F​
[/TD]

Huyu anasema ameongezewa Book Keeping na Commerce hebu jamani nisaidieni mbona mie sioni hayo masomo hapo juu?
 
Napata wasiwasi na huyo Bujugo anaposema kwamba walimsimamisha mwanafunzi masomo, hivyo hakufanya mtihani. Je alimfukuza akiwa kidato cha ngapi? Nasema hivyo kwa kuwa, serikali imekataza wanafunzi walio vidato vya mitihani ya taifa kufukuzwa. Ikiwama kama wamefanya kosa kubwa, wanaweza kusimamishwa kutoendelea na masomo, ila wataruhusiwa kufanya mtihani.
Nasubiri Dr. Ndalichako, labda anaweza, kutolea ufafanuzi. Sina imani na Bujugo kwa kuwa ni mdhulumishi wa kutupwa (yupo kwenye harakati za kudhulumu eneo la wzi ilnalotakiwa kujengwa serikali ya mtaa - Mbezi Jogoo), amekuwa akiiba mitihani.
 
Ndg makamanda,

NIMESHANGAZWA NA TAARIFA NILIYOSIKIA KUTOKA CLOUDS FM KWENYE KIPINDA XXL KUWA KUNA MWANAFUNZI WA FORM FOUR MWAKA JANA KAFAULU NA KUPATA DIVISION THREE WAKATI HAKUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE MWAKA JANA,

MY TAKE:NAPENDA KUXEMA KUWA HII YA LEO NA ILE YA MWAKA JANA YA KUFAULU WAKATI HUJUI KUSOMA VINATAKIWA KUINGIZWA KWENYE KITABU CHA MAAJABU YA DUNIANI

PIA HII INATOSHA KUMWONDOA KAWAMBWA NA AMIMU{MULUGO},

NI MUDA SASA WA CCM KUACHIA NCHI KIULAINI COZ IMEKUWA TOO MUCH SASA.

Source:XXL YA CLOUDS FM.
 
Mbona unashangaa hiyo wakati naibu waziri mwenyewe alisema hajui kama hata huo mtihani kama ulishawahi kufanyika au la!
 
For sure tutaendelea kumuenzi baba wa taifa,enzi zake Kawambwa angechezea stick na kutakiwa kuripoti kwa VEO kwa miaka10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…